Usishangae;Fans wa Diamond walikuwa blood Fans wa Alikiba

Usishangae;Fans wa Diamond walikuwa blood Fans wa Alikiba

Lengo kuu la uzi huu ni kuweka historia sawa.Naomba sana mods msiunganishe na uzi mwingine.
Nadhani wote tunakubaliana kuwa EX hawaachani bali wanatengana tu kwa muda endapo mmoja akiamuwa kuliamsha dude basi kurudiana ni rahisi kama kumsukuma mlevi

Nimeamuwa kuweka sawa historia kwa sababu kumezuka katabia siku za karibuni naweza sema"kakijinga"Eti wanasema mashabiki/fans wa Alikiba ni wale ambao wanamchukia Diamond kwa sababu ya mafanikio yake na mashabiki wengine wanamchukia kutoka kwa waliokuwa ex wake.Hii ni kauli ya kujifariji na Coward. Kama umeanza kusikiliza mzika start 2010's sitashangaa uku support hiyo kauli....

Labda niwakumbushe.Alikiba alianza mziki rasmi mwaka 2005 kwa kupata collaboration kutoka kwa wasanii waliomtangulia kama Dully Syksi,EB by skills na wengine wengi.Mwaka 2006 aliaachia wimbo wake mwenyewe official song ulioitwa Cinderella,nyimbo was a mega hit kwani àliweza kuingia kwa miguu miwili katika tasnia ya bongo fleva. Baada ya hapo nyimbo zilizofuta zilikuwa ni hit songs kama vile Nichumu,Msela,Nakshi Nakshi,Njiwa,MacMuga,n.k.mwaka 2008 ilikuwa ni bahati kwake hakuna msanii ambaye hatamani kufanya kazi na legend kama R.Kelly hivyo kupitia project ya One 8 msanii alikiba alifanya kazi na Wasanii waliokuwa wanafanya vizuri kipindi hicho.Project hii iliweza kumtambulisha Alikiba kimataifa zaidi kuanzia Afrika and Europe,US. Nyota ya alikiba iling'aa sana miaka hiyo kabla ya kuachia ngoma ambazo zina hit hadi leo kama vile,Mapenzi yana run dunia,Single boy,My Every thing,na Dushelele.
Late 2009's aliacha mziki/kupumzika katika tasnia ya bongo flava.Kuanzia mwaka huu ndipo kizazi kipya cha bongo fleva kiliibuka wasanii kama vile Marlow,Barnaba,Amini na Diamond n.k waliibuka.
Kwa upande wa Diamond ni msanii anayejituma sana kwani tangu alipoanza rasmi mzika mwaka 2010 graph yake inapanda siku hadi siku.Ni msanii ambaye amepata mafanikio makubwa tofauti na alionza nao.
Kumbuka tangu Alikiba anaacha mziki kulikuwa na malalamiko ya chini kwa chini kwa blood fans wake.Kuna wakati alisikika akisema kati ya moja ya interview zake kuwa"kizuri kikikosekana kibaya kitakuwa kizuri"mwisho wa kunukuu.Hivyo tangu amerudi rasmi katika tasnia ya bongo fleva ameweza kurudisha heshima na uwezo wake wa awali.
NOTE;
Mashabiki wa Diamond walikuwa mashabiki wa Alikiba kabla ya kuacha kuimba so sishangai leo kurudi katika asili yao ya awali.Alikiba na Fans wake ni mtu na Ex wake.
Asante

great thinker
Nahisi hili gazeti propaganda zake no mfu kabisa
 
Mbona bill gates hawamchukii? Na izo hela anazo peke ake? Acheni blah blah

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena wee ndo utakua unamchukia kweli,..hawamchukii bill sababa sio ligi yao,wanamchukia mond sabab wanaona kabsa yan huyu dogo alikua boya tuu hana kitu na katusua si tumebak tunamshangaa,..ukizingatia pia ngoz nyeus,.
 
Hakupendwa Yesu, pamoja na mazuri yote aliyoyafanya hapa duniani na bado watu wakamsurubu na kumtundika juu kama nyama buchani sembuse huyo bwana wako Almas. Kila mtu ana uchaguz wake nini cha kupenda na nini cha kukichukia usifos wote tumpende yeye.
 
Peleka namba ya simu WBC wakupatie mpunga mkuu
Mkuu mi naingiza 5mil na ushee a month wala sihitaj pesa ya WCB,mi nimewambia ukwel,yaan ukiona unamchukia diamond,ujue we ni mhanga wa hayo niliyosema kule juu..y umchukie mtu for no reason?.hakujui,humjui,hamlishi,hakulishi,..get a life bro
 
Hakika mkuu watanzania hawapendi mafanikio ya wenzao.Ukiwa tajiri mtaani utaskia mwizi au mchawi.Ukiwa na pesa utachukiwa bila sababu za msingi.
Mi hapa mtaani kulikuwa na jamaa ana duka lake na alikuwa anatukopesha vitu.Sasa juzi kati kaunguliwa na nyumba yake watu wanacheka eti alikuwa anajishau.
Hivi mtu kutumia pesa zake inawahusu nini nyie?Mlimsaidia kutafuta kweli???
Wapo watu leo kesho wanaomba wenye nacho warudi kuwa kama wao.Huu ni zaidi ya uchawi
 
Back
Top Bottom