Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
Ndugu zangu wa thamani, Tunapoelekea sherehe za Pasaka ,tunapoadhimisha kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ,binafsi napenda kuwaachia maneno haya kwa tafakari na tathimini ya maisha kibinafsi kwa mmoja wetu ………!
“Kabla sijakuumba katika tumbo la mama yako, nalikujua…” (Yeremia 1:5)
Maneno haya hayajaandikwa kwa bahati mbaya. Ni kiapo cha Mungu mwenyewe kwamba kila mmoja wetu alikuwepo kwenye fikra zake hata kabla hajamleta duniani. Hakuna aliye hapa kwa makosa. Kila mtu ana kusudi lake, nafasi yake, thamani yake.
Wapo waliobarikiwa kwa mali, wengine kwa vipaji, wengine kwa uvumilivu, na wengine hata kwa majaribu. Haya yote ni sehemu ya mpango wa Mungu tukamilishane, si tushindane.
Lakini kwa masikitiko, wengi wameigeuza dunia kana kwamba ni ya milele. Wanazunguka na kujivuna, wakisahau kuwa hata mkivuta pumzi sasa, hakuna anayeweza kuhesabu ni ngapi zimesalia.
"Maisha ya mwanadamu ni kama mvuke, huonekana kwa kitambo kidogo tu, kisha hutoweka." (Yakobo 4:14)
Swali ni moja tu, Je, unaishi vipi sasa na unajiandaa kwa nini?
Ni kweli, unaweza kuchagua kula bata sasa, kufurahia kila raha ya dunia. Lakini tukumbushe, Maisha haya si mwisho.Ni mwanzo tu wa safari nyingine ndefu isiyo na mwisho.
Na ni heri uamini, ukajiandaa, ukakuta si kweli kuliko kupuuza, halafu ukakuta ni kweli... utakuwa umejuta sana.
“Kila kitu kina majira yake, na kila kusudi chini ya mbingu kina wakati wake.” (Mhubiri 3:1)
Leo naomba nikukumbushe kama ndugu!….
Maisha haya ni zawadi tusiyachukulie poa.
Tukamilishane, Tuheshimiane, Tujitayarishe.
Kwa upendo mwingi na heshima, nawatakia tafakari njema na kuishi vizuri tunu na vipawa tumejaliwa …!
Ndimi ndugu yenu nisie na faida
Chavalikungu.
18/04/2025

- Usimdharau yeyote.
- Usijione bora kuliko wengine.
- Usiishi kana kwamba milele ni hapa.