Usitegemee nguvu za Kidini, Kijeshi, Kisiasa, Au Kibinadamu zikusaidie Mambo ya Kiroho

Usitegemee nguvu za Kidini, Kijeshi, Kisiasa, Au Kibinadamu zikusaidie Mambo ya Kiroho

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Yer 46:11 SUV
[11] Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.

Hukumu hii ilikuwa kwa Misri, nikimwanisha andiko hili linaonyesha hukumu dhidi ya Misri, taifa hili lilikuwa linajivunia nguvu zake za kijeshi na kisiasa.

Hii Gileadi inayotajwa hapa ilijulikana kwa jina lingine la "zeri", hii zeri ilikuwa ni dawa ya kuponya, changamoto ya dawa hii ilikuwa haiponyi majeraha ya kiroho na hukumu ya Mungu iliyokuwa juu yao.

Wakati mwingine tunaweza kutegemea sana nguvu ya kisiasa tuliyonayo, nguvu ya jeshi, nguvu ya dini, tukaona tunayo zeri ya kutusaidia kujikinga na hatari zozote zitakazoibuka juu yetu.

Tunasahau zeri ya kweli, inayoweza kutuponya na mambo mabaya ni Yesu Kristo, Yeye ni daktari mkuu, anaponya majeraha ya dhambi na uasi wetu.

Lk 4:18 SUV
[18] Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

Kutafuta uponyaji au usalama nje na Mungu, tunaweza tukawa salama kwa muda mchache sana, lakini mwisho wetu ukawa wa aibu na fedheha kubwa.

Dini zetu ni nzuri, nguvu ya kisiasa ni nzuri, hekima ya kibinadamu au ya dunia hii ni nzuri, ila kama tutagemea vitu hivi na kuona haina haja ya kumtegemea Mungu, tuwe na uhakika tumetangaza jambo baya kati yetu na Mungu.

Hupaswi kutegemea njia za kidini au kibinadamu, ukiona kuna mahali hujaenda sawasawa na Mungu tubu haraka na tengeneza uhusiano wako na Mungu. Elewa bila Yeye huwezi chochote, na huwezi kushinda vita vya kiroho kwa nguvu ya dini yako, au jeshi, utaishia kupigwa tu.

Huwezi kutibu tatizo la kiroho nje ya Kristo, huwezi kumtenda Mungu dhambi alafu dini yako nzuri na kubwa ikakuepusha na hukumu ya Mungu wako, na huwezi kuepuka hukumu ya Mungu kwa kuwa na nguvu kisiasa.

Mdo 4:12 SUV
[12] Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Tunaweza kutafuta tiba za mwili kwa gharama kubwa kama walivyofanya Misri, kumbe tatizo ni la kiroho. Tunaweza kutafuta wataalamu wa saikolojia, bila kujua shida hiyo ni ya kiroho na inapaswa kushughulikiwa kiroho.

Hatuwezi kupata msaada nje ya Kristo, hakuna mfumo wowote mzuri wa dunia hii, wala hakuna mafanikio yeyote makubwa, wala hakuna dini yeyote inayoweza kutuponya au kutuokoa na dhambi, ama kuokoa roho zetu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom