Millionaire Mindset
Member
- Apr 19, 2018
- 83
- 115
Njia ya watembea kwa mguu kuielekea safari ya mafanikio na ukwasi
Watembea kwa mguu watachukua muda mrefu sana kufika mwisho wa safari yao. Umbali kati ya Mwanza mpaka Dar ni kilometa karibu 853. Kwa umbali huu, mwenda kwa miguu anaweza kutumia zaidi ya masaa 420, sawa na siku 17; yaani hapo akiwa hajala, hajapumzika wala kulala popote pale. Ni mwendo wa haraka ule wa kijeshi. Wote tunaweza tukakubaliana kwamba, mtu huyu hatafika huko aendako, lazima tu atafia njiani.Maisha ni safari ndefu ni miongo kadhaa tangu mtu anazaliwa na waliobahatika humaliza zaidi ya karne, lakini watu wengi wanataka watembee kwa mguu kwenye safari hii. Ukimwambia mtu, ni afadhali utumie muda mwingi kutengeneza chombo cha usafiri (taaluma au biashara fulani), ili safari yako iwe rahisi; hakuelewi na wakati mwingine anakuwa mbishi.
Watembea kwa mguu wengi hawafiki mwisho wa safari yetu hii ya mafanikio. Wanawajua tu na kuwasikia akina Bakhresa, Mengi(Marehemu) na Moh Dewji, lakini kufikia viwango kama hivyo kwao ni ndoto. Walio wengi kwenye njia hii wanakufa hata kabla ya kuonja utamu wa Ukwasi.
Hebu tuangalie mfano wa chombo cha usafiri cha “udaktari” ili uupate udaktari inakuchukua zaidi ya miaka 7 ya shule ya msingi, kisha miaka mingine minne ya sekondari ya chini(o-level), kisha miwili ya sekondari ya juu(A-level), na kumalizia na miaka mitano ya chuo kikuu. Jumla ni miaka kama 18, na hapo hatujazungumzia miaka ya kurudia au Breaks zilizotengenezwa na mfumo wa elimu wa nchi yetu.
Kukipata chombo cha “Udaktari” ni gharama kubwa ya muda, jitihada na mali, lakini wote tunaweza tukakubaliana kuwa, kukisafiria chombo hicho kuelekea mafanikio ni nafuu kubwa kuliko vyombo vingine (ajira nyingine) au hata kwenda kwa mguu. Yaani safari kuyaelekea mafanikio kwako inakuwa ni rahisi ukilinganisha na mwenzako aliyemaliza darasa la saba na kuachana na habari za kuhangaika na shule kama wewe.
Kutumia miaka karibu 20, kukitengeneza cheti cha udaktari, ni muda mrefu na kazi nzito. Lakini ni afadhali kwa sababu kusafiri miaka mingine karibu 50 mbeleni, kwako inakuwa ni rahisi sana. Lakini watembea kwa mguu wengi hawatakubali kutoa miaka hiyo 20, kufanya kazi ya kukiandaa cheti cha udaktari.
Sisemi kwamba wanauona udaktari kama hauna maana; hapana!, asilimia 99 ya watembea kwa mguu watakukubalia kwamba “Kazi ya udaktari ni nzuri sana” lakini hakuna hata mmoja atakaye kukubalia kuufuata mchakato (Process) ya kuufikia udaktari. Watembea kwa mguu kwenye hii safari ya mafanikio ama ukwasi, watachagua kuanza safari bila chombo cha kusafiria, kuliko kukaa miaka hiyo mingi wakikitengeneza chombo hicho.
KUTUMIA VIGEZO VITANO(5) ILI KUICHUJA NJIA YA WATEMBEA KWA MGUU, KWENYE SAFARI YA KUELEKEA UKWASI.
Kigezo#1: Mahitaji ya watembea kwa mguu
Mahitaji ya watembea kwa mguu kwenye safari ya kuuelekea utajiri, ni ya kujitazama sana wao (Selfish). Wengi hawataki kabisa kutoa mchango kwenye jamii inayowazunguka au taifa kwa ujumla. Na ndiyo maana sifa yao kubwa ni kuilaumu serikali, ndugu au jamii inayowazunguka.
Watembea kwa mguu, wanapenda sana kupokea kuliko kutoa na kisingizio chao kikubwa huwa ni; “Sina hela”. Wamesahau kwamba Mungu alimuumba kila mtu kuwa na kipaji fulani ambacho kinatakiwa akitumie kuwanufaisha wengine siyo yeye binafsi. Lakini pia wanasahau kuwa kila mtu alizaliwa akiwa uchi na hakutoka na kitu chochote tumboni mwa mama yake, vitu vingine vyote vimetafutwa. Na kutokana na ubinafsi wa watu wa njia hii; wengi wao wanawachukia sana Matajiri, na pia wengi wao wanaamini kuwa matajiri wamezipata pesa zao kwa njia zisizo halali.
Waenda kwa mguu, hawaamini kuwa pesa inaweza kupatikana kwa njia za halali kama bidii na maarifa. Jambo hili linawapelekea wengi kulitolea nje suala la kujishughulisha, (nimetoa mfano wa miaka mingi aliyohangaika nayo daktari hapo juu), na wanaamua kutafuta njia zingine (Short-cuts) ambazo mwisho wake huwagharimu sana.
Mtazamo wao waenda kwa mguu ni; ili upate pesa lazima uwe na Ngekewa, uzaliwe kwenye familia ya kitajiri au Ufahamiane na mtu wa matawi ya juu. Hawana mtazamo wowote wa kutoa mchango kwa jamii inayowazunguka, ili jamii iwazawadie pesa, wanazozihitaji. Wamesahau kwamba;
“Pesa ni matokeo ya idadi ya mahitaji na matatizo ya wengine, uliyoyatatua”
Kigezo#2: kungia kwenye njia ya watembea kwa mguu
Hakuna kitu rahisi kama kujiunga na watembea kwa mguu kuelekea kwenye mafanikio. Kuingia njia hii ni rahisi sana, yaani unachofanya ni kujiachia, unakaa na kusubiri ndugu na serikali ndiyo watakao shughulika na maisha yako.
Kutokana na urahisi huo, ndiyo maana njia hiyo ina waumini wengi sana, haswa vijana wa kizazi hiki cha sasa. Wanakaa kusubiri, wazazi au ndugu, wawatoe kwenye shida zao, kazi yao ni kukaa vijiweni mchana kutwa, wakilaumu. Wanalaumu ndugu, Wanalaumu Mungu, Wanalaumu serikali, Wanalaumu, wanalaumu, wanalaumu is that simple!
Ukiona unachelewa miaka mingi kuipata taaluma....................................................................................INAENDELEA!