USITIBU DALILI TIBU CHANZO

USITIBU DALILI TIBU CHANZO

Joined
May 15, 2019
Posts
69
Reaction score
23
UNA MAUMIVU YA VIUNGO???
NA UNATUMIA DAWA HAUPONI?

Yawezekana kabisa unatibu DALILI kuliko chanzo cha tatizo hilo.

MAUMIVU ni matokeo ya athari ambayo imetokea katika msuli,mfupa,mshipa wa fahamu,sehemu ya ubongo na mengineyo.

Pindi matokeo haya yapotokea huashiria tatizo sehemu husika . na taarifa hutumwa mara moja kwenda kwenye ubongo ili kulitambua tatizo limetokea sehemu gani na kwa kiasi gani?. Taarifa hizi za tatizo hutafsiriwa na ubongo na kuleta hisia za maumivu sehemu husika mfano shingo,mgongo,mkono ,magoti,miguu.
wengi hukimbilia kumeza dawa kwanza kuondoa maumivu na bila kutambua maumivu hayo yanasababishwa na nini?

Hii hupelekea kulipa tatizo nafasi ya kukua na kusababisha madhara zaidi.

Pamoja na kupata madhara ya dawa husika.

EPUKA KUNYWA DAWA ZA MAUMIVU BILA KUPATA USHAURI/UCHUNGUZI WA DAKTARI
kwa ushauri wa bure wasiliana nami kupitia
0718 22 48 40
PSX_20190504_134412.jpeg
 
Lakini mkuu tuwekane sawa sawa your right hizo hizo dawa za maumiv zinatibu chanzo ambacho ni cox 2. Na postagrandins yanaingia humo.
 
karibu kaka.

maumivu yanayozungumziwa hapa ni yale ambayo yanatokana na mechanical factors mfano maumivu ya mgongo, magoti na shingo, nyonga na kadhalika.

haya ukiyatibu na dawa ,utayablock kwa muda fulani alaf baadae yatarudi mpaka uweke sawa chanzo chake mfano kubanwa kwa pingili za shingo au mgongo hutibiwa na traction yani kuvuta shingo au mgongo kuondoa mkandamizo. dawa haiwezi kuondoa mkandamizo huo.

itakachofanya ni kublock hayo maumivu.

lakin . maumivu ambayo chanzo chake ni systemic yani yanahusiana na hitirafu fulani katika damu. mfano infection . hayo yanaweza tibiwa na dawa mfank hizo cyclooxygenase 2 inhibitors ambazo zitaenda kuzuia inflammation process ambayo inasababishwa na vijidudu vilivyosababisha maambukizi fulani ya damu.

Natumai umenielewa sasa. au unaweza endelea kuuliza maswali tufahamishane zaidi.
karibu
Lakini mkuu tuwekane sawa sawa your right hizo hizo dawa za maumiv zinatibu chanzo ambacho ni cox 2. Na postagrandins yanaingia humo.
 
Back
Top Bottom