Usitoe mahari, epuka mila potofu

Usitoe mahari, epuka mila potofu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Nasisitiza, vijana kama ulikuwa ni mpango wako kutaka kuoa mwaka huu kwa kutoa mahari. Sitisha! Usitoe mahari. Ila ni vizuri kwenda kujitambulisha kwao na kwenu. Kama kuna uwezekano fanyeni sherehe ndogo kulingana na uwezo wenu.

Kamwe Usitoe mahari. Mahari ni kununua binadamu ambaye ni mnyama. Mtu kamwe hanunuliwi.
 
Mahali ni shukrani
We utamchukua binti wa mtu akuzalie watoto wa u bin wako bure
Akupikie bure
Akufulie bure
Utelezi bure kadri unavojisikia
Mwanaume lijali unalipa mahali kwa shukrani kwa familia ya mkeo
Hivi huko Dar wanaume wameisha?
Yaani mwanaume lijali unaona ushujaa kutolipa mahali ya mkeo
Basi olewa wewe utolewe mahali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahali ni shukrani
We utamchukua binti wa mtu akuzalie watoto wa u bin wako bure
Akupikie bure
Akufulie bure
Utelezi bure kadri unavojisikia
Mwanaume lijali unalipa mahali kwa shukrani kwa familia ya mkeo
Hivi huko Dar wanaume wameisha?
Yaani mwanaume lijali unaona ushujaa kutolipa mahali ya mkeo
Basi olewa wewe utolewe mahali

Sent using Jamii Forums mobile app


Shukrani?
Hivi unajua maana ya shukrani?
Kwa hiyo shukrani ndio unapangiwa unaowapa? Kweli bado kuna Watu wanaakili primitive.

Akupikie Bure? Kwani mwanaume hawezi kupika? Hivi unafikiri kila familia Mwanamke anapika, hujui kuna wanaoajiri wafanyakazi?

Kufua, hujui kuna mashine?

Kwa hiyo unalipa mahari ili upate mfanyakazi wa jumla jumla? Alafu mkiambiwa mnanunua binadamu mnakataa.

Sasa kuna tofauti ipi kununua punda kwaajili ya kubebea mizigo au ng'ombe wa kukupa maziwa na hiyo mahari?

Kuna Watu mpo karne hii kimakosa.
 
Mimi haya yote naamini yanasababishwa na umri,kila kitu kina wakati wake ukifika hakikwepeki.

Kuna umri ukifika automatically unajikuta unajaa kwenye mfumo yaani kila kitu duniani kilishafanyika na kitaendelea kufanyika tutake tusitake,kuna vitu binafsi nikiwa na umri fulani nilikuwa nikimuona mtu anavifanya nilikuwa namuona wa ajabu but leo nipo ktk umri ule mimi mwenyewe navifanya na tunaolingana umri wananiona nipo sawa madogo wananiona bro nazingua.
 
Bas mi mbwa au ng'ombe nionaye thamani ya kununulia kuliko kuchukuliwa tu na zigo linalohitaji huruma....ninunue unimiliki utakavyo..

Ndio maana nikasema kuwa kuna tofauti ya mtu na mnyama, mtu hamilikiwi ila mnyama anamilikiwa.

Faiza anasema huko shuleni mnaenda kusomea ujinga.
Kisheria hata mahakamani hakuna statement ya kumiliki mtu.

Ila kizamani kwa vile Mwanamke hakuwa mtu bali alikuwa sawa na mnyama ndio maana alinunuliwa na ndio kuna kauli kama hizo za kumilikiwa.
 
Mimi haya yote naamini yanasababishwa na umri,kila kitu kina wakati wake ukifika hakikwepeki..

Kuna umri ukifika automatically unajikuta unajaa kwenye mfumo yaani kila kitu duniani kilishafanyika na kitaendelea kufanyika tutake tusitake,kuna vitu binafsi nikiwa na umri fulani nilikuwa nikimuona mtu anavifanya nilikuwa namuona wa ajabu but leo nipo ktk umri ule mimi mwenyewe navifanya na tunaolingana umri wananiona nipo sawa madogo wananiona bro nazingua.

Kwa upande wa mahari ni hapana.
Hapa Tanzania na nchi zingine wapo mamilioni ya Watu wanaishi kama mke na mume na hawajatoa mahari.
 
Kwema Wakuu!

Nasisitiza, vijana kama ulikuwa ni mpango wako kutoa kuoa mwaka huu kwa kutoa mahari. Sitisha! Usitoe mahari. Ila ni vizuri kwenda kujitambulisha kwao na kwenu.
Kama kuna uwezekano fanyeni sherehe ndogo kulingana na uwezo wenu.

Kamwe Usitoe mahari.
Mahari ni kununua binadamu ambaye ni mnyama. Mtu kamwe hanunuliwi.
Hapa umepuyanga leo MAHALI siyo kuuza Bali ni mpango dhabiti ili mwanaume ajue kuwa huyo mkewe hakutokea tu from no where Kuna watu walipigana mpaka kufikia hapo alipo .

Kumlea mtoto wa kike na kufikia hatua akaonwa na kufaa kuwa mke siyo jambo la lelemama na dogo

Mahali ilipwe hii pia inadhihirisha kama wazazi hawamtaki mwanaume wanaweka mahali ya juu ashindwe ili aolewe na mwingine basi


Vijana lipeni mahali mke asiyelipiwa mahali ni mwepesi sana na hata ukweni mume asiyelipa mahali ni mwepesi mno

Lipa mahali jipe daraja la juu

Mke siyo bidhaa kama bidhaa zingine ila ni bidhaa Bora Kwa matumizi
 
Back
Top Bottom