Huu ni uzi tu wa kukumbushana. Kuna wale wenzetu wanaojifanya wakristo kuliko kristo mwenyewe nawasihi muache ujinga. Kusaidia sio jambo baya ila unaposaidia kiasi cha kutaka kujiyumbisha kiuchumi inakuwa sio sahihi. Saidia kulingana na uwezo wako na usisaidie hovyo hovyo. Watu wasikuzoee.
Kumbuka kabla ya kukuomba msaada watu walikuwa wanaishi maisha yao. Kwahiyo hata usiposaidia watapata jinsi ya kujinasua. Epuka kuwekewa alama kama mtoa misaada. Ukifilisika watakuhama na kutafuta mhanga mwingine. Watasahau kila kitu ulichowasaidia na wengine watakucheka na kukuona mpuuzi.
Hata ukiwa kanisani usibabaike na mchungaji anavyosema "toeni ili madirisha ya mbinguni yafunguliwe baraka kwenu"... pale church wanakuwekea na vijana wazuri kukuimbia nyimbo tamu ili utoe hiyo hela. Tafadhali chukua tahadhari.
Linda uchumi wako kwa wivu mkubwa.