Usitoe ofa bila sababu unapoteza wateja badala yake tumia mbinu hii

Mr_mkisi

Member
Joined
Sep 24, 2024
Posts
15
Reaction score
47
Mara nyingi huwa nakutana na matangazo Mtandaoni yanatangaza bidhaa na kunadi ofa ...

Unakutana na Tangazo linasema OFA OFA OFA jipatie ......kwa bei ya ofa ,lakini ukiangalia sababu za yeye kutoa ofa hana . Hili ni kosa kubwa wanalofanya wafanya biashara wengi bila wao kujua .

Dunia ya sasa imebadilika ,na hakili za wateja zimebadilika GEN Z (hasa kizazi kilichopo) wanahitaji zaidi sababu ....yaani ukifanya kitu kwa upande wako wanajiuliza kwanini unafanya hivo kabla ya kufanya maamuzi .

Hii imekaaje ? Swali zuri ..... Tuendelee.
Kila mmoja anajua madhara ya vitu vya bure au bei rahisi (tatizo la kisaikolojia) hivyo mteja anatafsiri neno Ofa kama ni kitu rahisi rahisi au cheap hata kama unauza bei sawa na wengine .

Hivyo ataanza kujiuliza maswali ...! Kwanini anatoa ofa ya bei la Punguzo .
Unajua nini huwa kinamjia kichwani ? ......

Soma hapa 👇 👇
1. Vitu / bidhaa hizi zimekaribia mwisho wa matumizi yake hivyo anataka viuzike haraka.

2. Vitu/ bidhaa hizi zimeshuka thamani hivyo anataka kuvitoa visimfie yeye mkononi .

3. Bidhaa hizi ni mbovu ,kwahiyo nikienda kununua havitanisaidia .

Sasa maana yake nini ? Mfanya biashara 0-5 mteja 😅 tayari wewe kama mfanya biashara umekosa wateja .

Je ,Ufanye nini ?
Ofa katika biashara sio mbaya kutoa na ni mbinu inayotumiwa na wengi ili kuharakisha mauzo ya bidhaa zao.
Lakini kinacho kosewa ni njia sahihi za kutoa ofa kwa mteja .

Kabla ya kujua jinsi ya kuandika Tangazo linalotoa ofa ili mteja asistukie kuwa umemtega ,... kwanza tujue sifa ya ofa
1. Ofa ina muda maalumu
2.Ofa ina idadi maalumu
3. Ofa lazima kuwe na sababu maalumu

Kumbuka hapa naamanisha TANGAZO linalozungumzia Ofa (Copywriting ya tangazo) kwa maana rahisi Tangazo lenye maneno ya OFA OFA OFA.

Kwanini nimetoa huo ufafanuzi ? Katika kamusi / kibiashara Ofa ni kitu kikubwa/ kipana sana ...

Maana ya ofa ni Jumla ya mambo yote unayo ahidi/ kutaka kumshawishi mtu au taasisi fulani ili ufanye naye biashara mafano . Kwenye mpira ... Utasikia Wydady wametuma ofa kwa Yanga ili kumnunua Mzize .

Sasa tuachane na ofa kama hizo tutazungumzia siku nyingine ...leo tuzungumzie ofa ya Kibongo bongo ya Tangazo linalo zungumzia ofa.

Katika siku 365 za mwaka kuna matukio mbali mbali unayoweza kutumia wewe kama mfanya biashara kumpa ofa mteja wako .

Unaweza kutumia siku ya wanawake duniani ,siku ya wakulima ,siku ya baba ,siku ya kuzaliwa ,Kristmas ,Ramadhani nk.

Mfano :
OFA, OFA, OFA ...
Leo utajipatia ofa ya simu za aina ya Samsungu kwa bei ya Punguzo la asilimia 10 nk ❌❌❌❌

Sema ...
Leo ni siku ya wanawake Duniani , ili kuonesha upendo kwa wanawake ,....Natoa ofa kwa wanawake 10 tu. Ili wajipatie Simu aina ya Samsung kwa punguzo la asilimia 10. Hii itadumu kwa masaa 48 tu .✅✅✅✅

Au.
Leo ni siku yangu ya kuzaliwa ,kutokana na siku hii muhimu napenda kufurahi pamoja na nyie wateja wangu. Kwa wateja 20 wa mwanzo watapata punguzo la asilimia 50 .✅✅

Hapo mteja 0-5 mfanya biashara .
Utaona wateja watakavyo miminika , sio lazima ushushe bei ya bidhaa, tumia saikolojia ya mteja tu.

Hapo mteja ataona kuna sababu za yeye kuchukua bidhaa kwako kwa sababu atahitaji awe miongoni mwa hiyo limited idadi na pia asivuke deadline maana anajua akichelewa zaidi atanunua kwa bei kubwa zaidi na pia hata jiuliza mara 2 kwanini huyu anatoa ofa leo.

Njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100.

KUHUSU MIMI .
Naitwa MKISI
Mtaalamu wa mawasiliano, kutengeneza Brand mtandaoni ,pia mtaalamu wa matangazo yanayo uza zaidi Mtandaoni.
Mhitimu wa chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) (BA IN PUBLIC RELATIONS AND ADVERTISING).

Je, ungependa kujifunza zaidi ?
Nimefungua group Jipya la WhatsApp natoa mafunzo bure kwa wafanya biashara .
Save namba yangu... 0628210865
Kisha nitumie ujumbe WhatApp wa jina lako , kama unahitaji kujiunga na group Tuma neno Biashara.

Unaweza kunifuatilia kwenye mitandao yangu ya kijamii
Intagram , Facebook na Tiktok
Mr_mkisi

Kumbuka madarasa yangu yote ni Bureee kabisa.
 
Na wewe unatoa HUDUMA BURE kwanini? … yaleyale unayopinga ndiyo unafanya
 
Toa link tujiunge chap bila kufata process nyingi mixa namba ya Nida
 
Back
Top Bottom