Usitoe sadaka, umeshatoa

Usitoe sadaka, umeshatoa

Nakaribia kukuelewa kumbe biblia huikubali, Kama huiamini itanisaidia namna ya kujadiliana, nilidhani naongea na mkristo asiyejua umuhimu wa kupelekea sadaka madhabahuni
Biblia kuu ni akili yako ya kuzitambua kazi na ukubwa wa Mungu. Jiangalie namna ulivyoumbwa na kazi zako, na hata mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, hutaacha kusema Mungu ni Mkubwa kama una akili timamu. Biblia haitoshi kuandika ukubwa, sifa na kazi zote za Mungu. Hata bila kuwepo kwa Biblia Mungu yupo. Mungu hategemei uwepo wa biblia, iwe umewahi kuiona au kuisoma Biblia lazima maisha yako yatafuata Uumbaji, nguvu na kazi za Mungu. Usijibane sana na vijitabu ukadhani Mungu yuko kwenye vijitabu hivyo ambavyo wengine wanasema walishushiwa, wengine wanadai walioteshwa, wengine waliamrishwa kusema na kuandika, ilimradi tu asitokee mtu wa kumdai ushahidi wa alichokiandika humo kwenye vijitabu. Lakini Mungi ni giant, kuandika habari zake zote utahitaji milima na milima ya vitabu na mapipa kwa mapipa ya wino na utahitaji karne na karne kumaliza kuziandika. Acheni mchezo wenu na Mungu. Mungu tangu lini akahitaji sadaka yako wewe? Yaani akupe 2000 yeye ili akunyang'ane 500 yeye tena. Atakuwa Mungu mjinga sana huyo. Kama anataka 500 kutoka kwako kwanini asikupe 1500 na kujibakishia 500 kabisa hukohuko?

Ndugu zangu Mungu anatujua na alitujua hata kabla hatujazaliwa, anazo remote zetu, huwezi kugeuza kile alichokupangia, sadaka mpe mzazi wako, yatima na mjane na kila mwenye uhitaji wa dhati. Mtu mwenye uhitaji wa dhati ni kama vile mgonjwa asiyejiweza kutoka kwenda kutafuta, mama anaejifungua au aliyejifungua au mtu mwenye shughuli inayotaka watu wengine wamsaidie kama kuzika, harusi, kujenga, nk.
 
Back
Top Bottom