Usitumie nywila (Password) moja kwenye mitandao yako tofauti ya kijamii

Usitumie nywila (Password) moja kwenye mitandao yako tofauti ya kijamii

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu, natumai nyote mpo salama.

Nywila (Pasword) imekuwa ni sehemu muhimu ya ulinzi wa akaunti zetu za mitandao ya kijamii pamoja na vifaa vyetu vya kidijitali. Katika kuendelea kuhakikisha matumizi ya mitandao ya kijamii inakuwa salama, wataalamu wa mitandao wanahimiza kuunda password imara ili kujiepusha kushambuliwana wadukuzi wa mitandao.

Aidha, pamoja na matumizi ya password hizi zipo Kesi kadhaa za watu kudukuliwa akaunti zao kwa namna tofauti.

Kwakuwa Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya msingi ya maisha yetu, inabeba mambo yetu mengi ya wazi na ya Siri ambayo pengine kuna tunayotaka watu wayaone na mengine tusingependa wengine wayaone.

Hivyo, Ili kuendelea kuwa salama unashauriwa kutumia password tofauti tofauti kwa mitandao yako ili ikitokea kwa mazingira mdukuzi au mtu mwingine amejuwa nywila yako ya akaunti yako Moja nyingine zibaki salama.

Zaidi soma> Ili kuilinda Password yako unapaswa kuzingatia yafuatayo
 
Back
Top Bottom