ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Kuna kitu watu wengi wanakidharau mpaka siku wanapokikosa hasa vitu vya ndani
Utakuta kijana alikuwa na gheto safi kabisa. Kitanda kipo, godoro lipo, sofa ipo, TV ipo, kabati lipo, vyombo vya jikoni vimejaa. Ghafla anapata dili mkoa mwingine. Kwa kuwa anahama haraka anasema aah, hivi vitu navitupia tu bei yoyote, nitafika huko nitanunua vingine. Akifika huko anakutana na vipengele Kitanda alichouza laki 2 anakuta laki 4.
Godoro alilouza bei ya hasara anakuta bei yake inamfanya aanze kudata. Kabati alilodhani ni jambo dogo anakuta ni nusu mshahara wa miezi kadhaa. Baada ya miezi sita unamkuta bado analalia godoro chini, huku akijiambia kumbe nilikuwa tajiri bila kujua heri hata utumie nauli kusafirisha kwenye lorry utumie hata laki 5 kusafirisha sawa tu..
Kama vijana anapanga kuoa mwakani asione vitu vya ndani ni jambo dogo. Heri kununua kitu kimoja kimoja. Unaweza ukampata mwanamke na hela ya kununua hivyo vitu usiwe nayo na kumbuka wanawake wanapenda wakute vitu ndani sebule iwe nzuri na chumbani pawe na vitu na jikoni angalau.
Hapo ndipo unagundua kwanini wazazi wengine huwapa watoto wao zawadi za harusi kama friji, sofa au vyombo. Sio kwamba wanapenda kuonyesha uwezo, bali wanajua maumivu ya kuanza nyumba kutoka sifuri.
Siku hizi kijana akitaka kujaza nyumba ya kawaida tu anaweza kutumia karibu milioni 3 au zaidi bila hata kugusa vitu vya anasa.
Ndio maana usimcheke mtu anayenunua sufuria leo, mwezi ujao chupa ya chai, baadae ananunua TV. Huyo anajenga ufalme wake taratibu.
Vitu vya ndani ni kama meno, ukiwa navyo huvioni thamani yake. Ukivikosa ndipo unajua maisha yanavyochangamka