Usiwaonee huruma wateule wa Magufuli kwani ni chujo la viongozi waliokosa ubunifu na baraka kwa vijana wenye ubunifu wa uongozi waliokuwa wakibaniwa

Usiwaonee huruma wateule wa Magufuli kwani ni chujo la viongozi waliokosa ubunifu na baraka kwa vijana wenye ubunifu wa uongozi waliokuwa wakibaniwa

Hisha Sorel

Senior Member
Joined
Dec 27, 2017
Posts
192
Reaction score
140
Mh. Magufuli ameanza mizunguko yake kote nchini, na kama kawaida viongozi wengine wamekuwa wakipata shida kwa maswala anuwai, lakini zaidi ni uzembe.

Na kama kawaida, watu wamekuwa wakilalamika kwamba Rais ni mkali sana jambo ambalo nimeshangazwa nalo.

Kwa maoni yangu, rais anapaswa kuwa mkali zaidi akizingatia ni wapi tunataka nchi yetu iwe katika kipindi kifupi.

Malengo ya Taifa ni ya juu sana na yatabaki kuwa hivyo ikiwa uongozi hautakuwa wa ubunifu.

Hatuwezi kuwa na ubunifu wa uongozi na watu wale wale, tunahitaji fikra mpya.

Hatuwezi kuwafuta kazi watu kwa sababu wamekuwa katika nafasi kwa mda mrefu Zaidi; kwani wanaweza kuwa wamebaki hapo kwa sababu ya uwezo wao.

Kwa hivyo, hapa ndipo Rais Magufuli anapokuja viwango vya juu: Matarajio ya juu huweka shinikizo kwa viongozi kubuni na kubadilika, na kuacha kuongoza kwa mazoea.

Wale ambao watashindwa, watafukuzwa kazi, na hivyo kufungua nafasi kwa wale ambao wanaweza.

Kuna vijana wengi wa Kitanzania wenye talanta na ubunifu ambao wanapuuzwa kwa sababu wanakosa connection za kupata kazi ya juu.

Huu ni wakati wao kwani watainuka kuchukua nafasi tupu zilizoachwa.
 
Upungufu wa Ubunifu ni janga la taifa! Elimu yetu inatuandaa kuwa marobot tu. yaani tunaandaliwa kufuata maekezezo tu na sio nje hapo! Umemsikia kiongozi wa baraza la wafamasia ambaye akili zake bado zinaamini ili usimamie duka la dawa ni lazima uwe chumba cha pili kutoka hapo lilipo duka wakati mimi hapa nipo nafanya kazi za usekretari za mtu aliyepo New Jersey- Marekani...yaani napokea oda za wateja wake, nawapa maelekezo ya bidhaa zake mpya, naandaa ripoti za mauzo yake kwa siku,nk

Mtoto wa darasa la tatu kwa elimu za wenzetu ana uwezo wa kuja na wazo wenyewe wanaita "project" ya jinsi ya kutatua moja ya kero zilizopo darasani, mtaani, nyumbani, nk wakati huku kwetu kijana anahitimu chuo kikuu hajawahi kuja na ubunifu hata wa kusaidia familia yake tu!
 
Back
Top Bottom