Usiwe king'ang'anizi...soma alama za nyakati!!

ni kweli lizzy lakini mambo si marahisi kama ulivoandika laiti ingekuwa ivo...................!
 
Babu sidhani kama mtu akiwa na kasoro ndo anastahili kunyanyaswa!!!Mtu ambae anakukomoa kwa kwenda nje...kukupiga...kukutusi...kukudharau eti kwasababu una kasoro sio mtu anayekufaa.Mtu mzuri ni yule atakaejaribu kukurekebisha kama inawezekana au kukuvumilia kama haiwezekani.

Binafsi sijasema wala siwezi kusema ni rahisi kuamua tu kwamba naondoka....ila haina maana kwamba HAIWEZEKANI or it shouldn't be done!!
Mtu wangu wa karibu yalimkuta...alidanganywa akadanganywa na kudanganywa zaidi na akavumilia.Hapo ni baada ya kumtunza huyo mnaume kwa zaidi ya miezi sita baada ya kupata ajali.Shukrani yake ilikua hiyo.Kama mnavyosema maamuzi yanatakiwa kutoka kwa mtu binafsi nakubaliana na nyie....ila wakati mwingine inabidi mhusika asukumwe kidogo ili apate ujasiri.Mwanzoni sikutaka kuingilia mpaka alipokuja kumsukuma kwenye ngazi mdada akiwa mjamzito wa miezi mitano....nusu saa baadae alikua anatokwa na damu bila kikomo na maumivu yasiyoelezeka juu.Pale sasa ndio ulikua muda sahihi wa kumuonyesha kwamba kwa kujidanganya anamvumilia ampendae HAJITENDEI YEYE HAKI maana hasara atakayopata itakua juu yake yeye na sio huyo mwanaume.Ingetokea akafa huyo mwanaume angepata mwingine tu....ila yeye asingezawadiwa maisha mengine kwa uvumilivu wake.....wala ndugu zake tusingezawadiwa ndugu mwingine!!!Nashukuru Mungu alipata ujasiri wa kuachana nae maana kwa kuendelea kuwepo inawezekana leo hii ningekua nahadithia kitu tofauti kabisa.

Upande niliopo mimi ni kama nilivyoelezea tangu mwanzo.VUMILIA ndio ila ikishafika kile kipindi ambacho WEWE MKOSEWAJI NDO MBEMBELEZAJI jua muda wa mahusiano yenu yameisha!!Au kaa ukisubiria kifo iwe ni cha magonjwa au kipigo....kuchanganyikiwa na kuishi kama zombie!!!Ila kumbuka HUJITENDEI HAKI maana wewe ndo unatakiwa kufanya maamuzi juu ya maisha yako.
 
Ha ha ha Lizzy bana umeamua kunichana live (tangu nikupe story ya shem wako vile ananinyanyasa na nashindwa kumwacha).

Kuacha/kuachwa pale unapopendwa/unapopenda ni shughuli pevu aisee

Hahahahah.....bora nikubembeleze ukilia sasa hivi kuliko kulia ukitutoka!!!!

( Yani sitoacha upumzike mpaka uachane nae....alafu ikibidi utamwacha hata kwa lazima....hakufai kabisa huyo!! )
 
Lizzy,

Mama watoto wangu huwa anao usemi maarufu sana, naomba nimnukuu:

"..Mimi nilikuja kuolewa, sikuja kutembea.." mwisho wa kunukuu.

Kuna wanawake wengi wapo kwenye mahusiano kwa "dhati", no matter what!!!!
 
aya maneno unauza sh ngap?
nataka niyanunue jaman km ntaweza
umesema kweli
tangu mwanzo umenena kweli
pipo waache uwoga
utakiwi sepa fasta utapata mwingne nje atakupenda iweje ujifungie jela wakat kuna hotel ya movenpik inakusubiri apo nje?
lizzy mwaya umeongea kweli
nkwambia i like liberal style of living...unanipenda poa unipend nasepa full stop
mambo ya kuota mvi na miaka 30 sjui 27 yahuu?
yaan maisha ya siku izi inabidi tutembee na kitufe cha DELETE,UN DO au CANCEL ili kuepuka karaha na mishtuko ya moyo na mbavu km drama zenyewe zilivyo!!!
 
Lizzy,

Mama watoto wangu huwa anao usemi maarufu sana, naomba nimnukuu:

"..Mimi nilikuja kuolewa, sikuja kutembea.." mwisho wa kunukuu.

Kuna wanawake wengi wapo kwenye mahusiano kwa "dhati", no matter what!!!!

1 in milion
punguza drama na wewe ili mkeo aseme...MIMI NILIKUJA KUENJOY MAISHA NA KULEA WATOTO NA WEWE NA SIYO KULIZWA DAILY...
nawasilisha.:lol:
 
Hahahahah.....bora nikubembeleze ukilia sasa hivi kuliko kulia ukitutoka!!!!

( Yani sitoacha upumzike mpaka uachane nae....alafu ikibidi utamwacha hata kwa lazima....hakufai kabisa huyo!! )

kuna statement kidumu alisema kwenye ule mwimbo na JD ...ni bora nilie leo badala ya kesho....kupenda usipopendwa ni kama kujitia kitanzi....
 
Lizzy,

Mama watoto wangu huwa anao usemi maarufu sana, naomba nimnukuu:

"..Mimi nilikuja kuolewa, sikuja kutembea.." mwisho wa kunukuu.

Kuna wanawake wengi wapo kwenye mahusiano kwa "dhati", no matter what!!!!

Kwahiyo kwake kuolewa ni jukumu ambalo lazima litimizwe na sio kuishi maisha na mtu ambae anapunguza kila kilicho kibaya asibebe mwenyewe na kuongeza mazuri???Hongereni kwa hilo!!!!

''Dhati'' kwa maana ya kweli bila kipimo.....????Mtu asiyekuthamini na kukuheshimu hastahili huo ''udhati'' unaouongelea!!!
 
Hehehehehe....we ntakupa bure my dear!!!Mwenyewe nashindwa kuelewa kwanini watu wanang'ang'ania wasipotakiwa!!1
 
tangu ukuwe karib na mimi umekuwa na sredi za maana kweli lizzy. ving'ang'anizi hawakubaliki . full stop.

thread closed.
 
Babu siandiki tu kufurahisha jamvi....mwenyewe nimewahi kua na mtu ambae alikua haishi vituko.Baada ya kuona haelekei kula nnakotaka mimi nikamtolea uvivu!!Kitendo cha mimi kumuacha ndo kilikua ''wake up call'' yake.Baada ya hapo alibadilika akawa vile ambavyo alipaswa kua tangu mwanzo!!Kwahiyo watu wanaokaa wakisema atabadilika atabadilika.....kuna nafasi kubwa sana hatabadilika kwasababu anajua hata akufanye nini huendi popote!!!Watu waache kutumiwa kama mipira bwana.....kama mtu haonyeshi kukuthamini..jithamini wewe mwenyewe!!

Hhehehe babu bwana.....hamna kitu kisichotekelezeka hapa...ni maamuzi tu!!!Ndio ni ngumu ila inawezekana!!Kuachana na mtu hakuui....ila kumng'ang'ania kunaweza!!!
 
tangu ukuwe karib na mimi umekuwa na sredi za maana kweli lizzy. ving'ang'anizi hawakubaliki . full stop.

thread closed.

Heheheh kwanza si ulisema hurudi tena??
Ila nimefurahi kukuona maana busara zilikua zimeanza kupungua!!!!
:focus:Hamna kua king'ang'anizi...unless mnang'ang'aniana!!!!
 
My dear...life is all about taking risks!!!
Hata wakati unamkubali uliyenaye badala ya wengine kadhaa waliokua wanakumendea ulikua hujui kwa uhakika nini kingetokea mbeleni ila ulichagua kuamini kwamba ndie anaekufaa.Wakati mvua inanyesha na radi inapiga huwezi kusimama katikati ya barabara badala ya kujihifadhi chini ya mti kwa kuogopa radi....huwezi kukwepa tatizo usilolijua wala kuliona huku unakumbatia unalolijua tayari!Mapenzi sio kunyanyasana wala ndoa sio mateso......chukua hatua!!!!
 
I've come to realize kuwa wanawake wengi ni either "wamelizwa" au ni wako njiani "kulizwa"!
 
Hahahahah.....bora nikubembeleze ukilia sasa hivi kuliko kulia ukitutoka!!!!

( Yani sitoacha upumzike mpaka uachane nae....alafu ikibidi utamwacha hata kwa lazima....hakufai kabisa huyo!![/COLOR] )

Asante kwa kujali masilahi yangu ubarikiwe mama mchungaji
 
1 in milion
punguza drama na wewe ili mkeo aseme...MIMI NILIKUJA KUENJOY MAISHA NA KULEA WATOTO NA WEWE NA SIYO KULIZWA DAILY...
nawasilisha.:lol:

1 in a million? You are not serious and I'm assuming "umeachika" au uko njia moja!

Wanawake wenye HEKIMA na BUSARA hawakimbii ndoa zao! Labda yale "manungayembe" by default.. Mwanamke anapoingia kwenye mahusiano kwa hisia za "ku-enjoy" huyo hafai ni wa kuepuka mapema kabla ya kusimama altare!
 
My dear...life is all about taking risks!!!
Hata wakati unamkubali uliyenaye badala ya wengine kadhaa waliokua wanakumendea ulikua hujui kwa uhakika nini kingetokea mbeleni ila ulichagua kuamini kwamba ndie anaekufaa.Wakati mvua inanyesha na radi inapiga huwezi kusimama katikati ya barabara badala ya kujihifadhi chini ya mti kwa kuogopa radi....huwezi kukwepa tatizo usilolijua wala kuliona huku unakumbatia unalolijua tayari!Mapenzi sio kunyanyasana wala ndoa sio mateso......chukua hatua!!!!
 
Hatukuja Duniani kuteseka bana khhaaaa
 
sometimes you have to take risks in certain decisions
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…