Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 116
- 260
Na Lukumay M.
Ufinyu wa taarifa sahihi ni janga jipya katika Dunia ya sasa. Wanasiasa wanautumia mwanya huu kubeba ajenda zao binafsi bila kuzingatia ukweli. Kwanza kabisa niweke wazi mimi ni mzaliwa wa kijiji cha Enduleni ndani ya NCA hivyo naandika ili kukupa uhalisia na si vinginevyo.
Kuanzia mwaka 2000 zimefanyika tafiti zaidi ya 94 kutoka Taasisi mbalimbali za elimu ya juu na mashirika ya ndani na nje ya nchi. Mara nyingi matokeo ya tafiti hizi yamekuwa yakishahabiana katika vipengele vya uhai wa NCA na ustawi wa wakaazi wa eneo hili.
Baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijirudia mara nyingi na wakaazi wa Ngorongoro tunafahamu ni kama zifuatazo;
1. Ongezeko kubwa la idadi ya watu kwa mwaka. Mfano mpaka mwaka 2015 katika kijiji cha Nainokanoka ongezeko la watu lilikuwa karibu 40% kwa mwaka.
2. Uharibifu wa uoto wa asili (Nature vegetation). Hii kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ongezeko la mifugo kama vile Ng'ombe kwa kiasi kisicho stahimilivu kwa eneo la NCA. Ukifika Enduleni leo hii si Enduleni ile ya mwaka 2002, hamna kabisa uto wa asili.
3. Kusambaa kwa magonjwa ya wanyama wa kufugwa na wale wa porini kutokana na muingiliano usio dhibitiwa. Hii ni moja ya mambo yaliyoonyeshwa na kila tafiti niliyowahi kuisoma hapa Ngorongoro na tunashukuru Mungu kuna jitihada zimefanyika lakin bado hali inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku.
4. Wimbi kubwa la wahamiaji ndani ya NCA. Watu tunaofahamu historia ya NCA tunaweza kuwatambua wavamizi lakini kimsingi ni ngumu kuzuia watu wasihamie NCA, wengine wanakuja kama watumishi na na baada ya kustaafu wanaweka makazi yao hapa.
5. Ukosefu wa huduma bora za jamii. Binafsi natambua kuwa wazawa wa hapa Ngorongoro ni kama walivyo watanzania wengine hivyo haki ya huduma bora za Afya ni lazima lakini swali kubwa ni kwa namna gani miundombinu itajengwa ikiwa tunahitaji kutunza uasili wa eneo la NCA?
6. Mahitaji ya kisiasa na maslahi binafsi. Kati ya mambo yanayoondoa uhalali wa baadhi ya viongozi wetu hapa Ngorongoro ni kila mmoja kujaribu kuchukua changamoto za NCA kujijenga kisiasa, wapo watu wanajifanya wenye haki kuliko wengine ili mradi tu waweze kutimiza haja zao kisiasa.
Nini kifanyike? Nashauri serikali iendelee kuchukua hatua za kina zenye kulenga kujenga ecosystem endelevu. Wanasiasa wapuuzwe kwa kuwa hawajui uhalisia bali wanafanya wanayoyafanya kwa maslahi yao. Wanaonufaika na NGO's tunawafahamu kwa majina na ukweli ni kwamba mipango yenu haina maslahi kwa Taifa letu.
Nawapongeza walioamua kuhama kwa hiari ndani ya Hifadhi ya NGORONGORO na pongezi kwa serikali kwa kutoa nyumba mpya na viwanja. Maeneo ya malisho ya kutosha, huduma za jamii ni baadhi ya mambo yanayoonyesha dhamira njema ya serikali.