Vipi maisha yako ya ndoa?
Niliwahi kuishi na mume wangu wa ndoa,
tukafanikiwa kupata mtoto mmoja , lakini
baadaye ilibidi nidai talaka. Niliishi kwenye
ndoa ya manyanyaso sana . Mume wangu
alikuwa akinisaliti waziwazi kiasi kwamba
alifikia hatua akawa anatoka na marafiki zangu
wa karibu.
Nilishindwa kuvumilia , nikaomba talaka.
Nashukuru tuliachana salama . Kwa sasa
mwanetu anakaa ukweni (kwa wazazi wa
mume ) na mimi naendelea na maisha yangu .
Baada ya kutengana naye nilikutana na
mwanaume mwingine ambaye naye nilizaa
naye mtoto mwingine .