Usiyoyajua kuhusu Ruge, licha ya kuacha alama kwenye maisha ya wengi, Ruge alikuwa ana damu kali, alama zipo

Usiyoyajua kuhusu Ruge, licha ya kuacha alama kwenye maisha ya wengi, Ruge alikuwa ana damu kali, alama zipo

Watoto watano mama separately? Kifupi alizaa na wanawake wanne (Zamaradi ana watoto wawili). Hakuweza kuishi hata na mmoja wao. AU hata kuoa kwa umri ule ili naye leo aagiwe nyumbani kwake? Daaah ni kazi sana sana. Anyway kizuri hakikosi kasoro. A man is respected by the kind of family he managed to raise but not the wealth he created.
 
Wanabodi,

Nami niko hapa viwanja vya Karimjee katika kumuaga Ruge Mutahaba.
hivyo tunapomuaga kaka wa Taifa, Ruge Mutahaba, nimewasikia wengi wakisema pengo lake halitazibika, sii kweli, kwa sisi tuliomfahamu Ruge kabla ya umaarufu huu, tunaweza kuwadokolea kidogo usiyoyajua kuhusu Ruge, alikuwa ni Simba mwenda kimya mwenye damu kali, hivyo zaidi ya kuacha Alama kwenye maisha ya wengi, kufuatia ukali wa damu yake, pia ameacha alama za ukweli za Ruge Mutahaba, hivyo you never know, Pengo lake linaweza kuja kuzibika huko mbeleni.

Mimi nimemfahamu Ruge na Jo enzi za Mawingu Studio hata kabla Clouds Radio haijazaliwa, enzi hizo, wao wakiwa na tenda za maandalizi ya Miss Tanzania za Mikoani na mimi nikila tenda za u MC.

Ruge Mutahaba ana jicho fulani hivi la kuangazia warembo wenye vipaji vya kutwaa taji ya miss Tanzania.

Kwa kawaida kwenye events zozote, steering wa even kuangazia ma miss, huwa ni MC. Hivyo mimi ndio nilikuwa najiona steering, hivyo hata katika panga pangua za nani aukwae u Miss, MC huwa amemspoti nani ataukwaa umiss. Kwa kawaida Ruge huwa ni mkimya hata mrembo awe ni mrembo wa kutisha vipi, Ruge hakuwahi kubabaika, yuko kama vile haoni, kumbe jicho la Ruge limeisha ona kitu hicho saa nyingi.

Mimi kama MC, jicho langu linaona kila mrembo no mzuri anaweza kuwa ndie miss wetu, kumbe jicho la Ruge linaona kuliko jicho la kawaida, pale jicho la Ruge linapoona, hapo ndipo miss atakapoibukia.

Kwa kawaida kabla ya shindano, ma miss wote huwekwa kambini na kufundwa namna ya kuwa miss bora, katika kambi, zaidi ya kufunzwa namna ya kushinda umiss, pia hufunzwa, maadili, lakini ile siku ya mwisho ya shindano, mara baada ya shindano kukamilika, hufuatiwa na pilika pilika za vijana na ujana katika kuwapongeza mamiss walioshinda au kuwapooza na kuwafariji mamiss walioshindwa.

Mimi kama MC, nilikuwa ndie mpongezaji Mkuu na mfariji Mkuu, na kuna pongezi na pongezi, kuna faraja na faraja. Ikawa kila nikilenga mahali ili nikapongeze au kutoa pole, nakuta hapoingiliki, pongezi hazipokelewi na pole hazihitajiki. Ndipo mimi nikawa najiuliza, kama mimi ndio MC, nimepanga nitoe pongezi au pole, nawezaje kukataliwa?. Nani ni zaidi ya MC?. Ndipo nikaelezwa kuwa katika mashindano ya umiss yanayoandaliwa na Clouds, hata mwisho wa shindano, hakuna kujiwahia ma miss, kwenda kujipongezea au kujifarijia, ni nidhamu mwanzo mwisho, hakuna Miss kupongezwa privately wala kufarijiwa privately, ni nidhamu, heshima adabu hadi mwisho.

Leo katika heshima za mwisho za Ruge pale nyumbani kwa Prof. Mutahaba, nimeona viji copy copy kadhaa ambavyo wala huhitaji kuuliza, hivyo usikute licha ya ulinzi wote ule, mimi na kelele zangu za U-MC, nilitoka kapa, nikaambulia patupu, kumbe kuna "Simba mwenda kimya" kimya kimya...huwezi kujua, huwezi kuona, very private, very discreet, leo kwenye msiba, ndio unashangaa kuona viji copy huwezi kuuliza.

Hivyo kwa wapenzi wa Ruge, poleni sana, tutam miss Ruge, na ni kweli pengo lake halitazibika, lakini maadam ameacha copies, then Ruge, japo amekufa kimwili tuu, kiroho tuko nae, na maadam copy zake zipo, kwa mtu mwenye damu kali, some of the copies, are not copies, they are the originals kabisa, hivyo Ruge yupo, na Pengo lake litazibika. Ila pia kwa hawa ma celebs wetu, kuna walio ondoka, wakawa wameondoka jumla, kama Kanumba, kaondoka na Bongo movies yake, pengo lake bado halijazibika, na sikuwahi kusikia kama ameacha copy yoyote.

RIP Mwili tuu wa Ruge Mutahaba, Ruge Mutahaba mwenyewe yupo na roho yake ipo, tunaishi nae milele ndani ya mioyo yetu.

Paskali
We we jamaa uje uandike kitabu bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto watano mama separately? Kifupi alizaa na wanawake wanne (Zamaradi ana watoto wawili). Hakuweza kuishi hata na mmoja wao. AU hata kuoa kwa umri ule ili naye leo aagiwe nyumbani kwake? Daaah ni kazi sana sana. Anyway kizuri hakikosi kasoro. A man is respected by the kind of family he managed to raise but not the wealth he created.
Kwani familia NN mkuu ? Si wale watoto anao ? Nafikiri alishawahi kuishi na zamaradi
 
Kwani familia NN mkuu ? Si wale watoto anao ? Nafikiri alishawahi kuishi na zamaradi
Mkuu kwa mila na tamaduni za kiafrika bila kuficha hata wazazi wake huyu kijana marehemu walitamani kwa umri wa karibia 50 years angekuwa na nyumbani kwake kwenye mke na watoto. Tofauti hii imegusa wengi kwa hakika. Kuwa na watoto kila mmoja na mama yake maana yake hakuna malezi ya pamoja hapo hivyo ile sense ya familia inapotea. In Africa voice a nuclear family consists of father, mother and children living together I.e under one roof or living together in principle but separated by social and economic affairs (utengano wa muda kwa kazi au jambo la kijamii).
 
Watoto watano mama separately? Kifupi alizaa na wanawake wanne (Zamaradi ana watoto wawili). Hakuweza kuishi hata na mmoja wao. AU hata kuoa kwa umri ule ili naye leo aagiwe nyumbani kwake? Daaah ni kazi sana sana. Anyway kizuri hakikosi kasoro. A man is respected by the kind of family he managed to raise but not the wealth he created.
Mkuu kwani kuwa na familia hadi uishi na mume au mke,pia sijaona sehemu iliposemwa kwamba alishindwa kuimudu hiyo au hao watoto wake watano. Tuache kukariri.
 
Back
Top Bottom