Wanabodi,
Nami niko hapa viwanja vya Karimjee katika kumuaga Ruge Mutahaba.
hivyo tunapomuaga kaka wa Taifa, Ruge Mutahaba, nimewasikia wengi wakisema pengo lake halitazibika, sii kweli, kwa sisi tuliomfahamu Ruge kabla ya umaarufu huu, tunaweza kuwadokolea kidogo usiyoyajua kuhusu Ruge, alikuwa ni Simba mwenda kimya mwenye damu kali, hivyo zaidi ya kuacha Alama kwenye maisha ya wengi, kufuatia ukali wa damu yake, pia ameacha alama za ukweli za Ruge Mutahaba, hivyo you never know, Pengo lake linaweza kuja kuzibika huko mbeleni.
Mimi nimemfahamu Ruge na Jo enzi za Mawingu Studio hata kabla Clouds Radio haijazaliwa, enzi hizo, wao wakiwa na tenda za maandalizi ya Miss Tanzania za Mikoani na mimi nikila tenda za u MC.
Ruge Mutahaba ana jicho fulani hivi la kuangazia warembo wenye vipaji vya kutwaa taji ya miss Tanzania.
Kwa kawaida kwenye events zozote, steering wa even kuangazia ma miss, huwa ni MC. Hivyo mimi ndio nilikuwa najiona steering, hivyo hata katika panga pangua za nani aukwae u Miss, MC huwa amemspoti nani ataukwaa umiss. Kwa kawaida Ruge huwa ni mkimya hata mrembo awe ni mrembo wa kutisha vipi, Ruge hakuwahi kubabaika, yuko kama vile haoni, kumbe jicho la Ruge limeisha ona kitu hicho saa nyingi.
Mimi kama MC, jicho langu linaona kila mrembo no mzuri anaweza kuwa ndie miss wetu, kumbe jicho la Ruge linaona kuliko jicho la kawaida, pale jicho la Ruge linapoona, hapo ndipo miss atakapoibukia.
Kwa kawaida kabla ya shindano, ma miss wote huwekwa kambini na kufundwa namna ya kuwa miss bora, katika kambi, zaidi ya kufunzwa namna ya kushinda umiss, pia hufunzwa, maadili, lakini ile siku ya mwisho ya shindano, mara baada ya shindano kukamilika, hufuatiwa na pilika pilika za vijana na ujana katika kuwapongeza mamiss walioshinda au kuwapooza na kuwafariji mamiss walioshindwa.
Mimi kama MC, nilikuwa ndie mpongezaji Mkuu na mfariji Mkuu, na kuna pongezi na pongezi, kuna faraja na faraja. Ikawa kila nikilenga mahali ili nikapongeze au kutoa pole, nakuta hapoingiliki, pongezi hazipokelewi na pole hazihitajiki. Ndipo mimi nikawa najiuliza, kama mimi ndio MC, nimepanga nitoe pongezi au pole, nawezaje kukataliwa?. Nani ni zaidi ya MC?. Ndipo nikaelezwa kuwa katika mashindano ya umiss yanayoandaliwa na Clouds, hata mwisho wa shindano, hakuna kujiwahia ma miss, kwenda kujipongezea au kujifarijia, ni nidhamu mwanzo mwisho, hakuna Miss kupongezwa privately wala kufarijiwa privately, ni nidhamu, heshima adabu hadi mwisho.
Leo katika heshima za mwisho za Ruge pale nyumbani kwa Prof. Mutahaba, nimeona viji copy copy kadhaa ambavyo wala huhitaji kuuliza, hivyo usikute licha ya ulinzi wote ule, mimi na kelele zangu za U-MC, nilitoka kapa, nikaambulia patupu, kumbe kuna "Simba mwenda kimya" kimya kimya...huwezi kujua, huwezi kuona, very private, very discreet, leo kwenye msiba, ndio unashangaa kuona viji copy huwezi kuuliza.
Hivyo kwa wapenzi wa Ruge, poleni sana, tutam miss Ruge, na ni kweli pengo lake halitazibika, lakini maadam ameacha copies, then Ruge, japo amekufa kimwili tuu, kiroho tuko nae, na maadam copy zake zipo, kwa mtu mwenye damu kali, some of the copies, are not copies, they are the originals kabisa, hivyo Ruge yupo, na Pengo lake litazibika. Ila pia kwa hawa ma celebs wetu, kuna walio ondoka, wakawa wameondoka jumla, kama Kanumba, kaondoka na Bongo movies yake, pengo lake bado halijazibika, na sikuwahi kusikia kama ameacha copy yoyote.
Taarifa hii ya Ruge kuacha copy msiitafsiri vibaya, bali aminini msiamini, hata watu wamlilie vipi Ruge, na mambo makubwa yote aliyoyafanya, yatapita na yatasahauliwa, faraja pekee ya kumbukumbu ya Ruge itakabaki ni hizi copy.
RIP Mwili tuu wa Ruge Mutahaba, Ruge Mutahaba mwenyewe yupo na roho yake ipo, tunaishi nae milele ndani ya mioyo yetu.
Paskali