Usiyoyajua kuhusu Senegal

Macky Sall kashasahau dhuluma alizofanyiwa na Wade, sasa na yeye anawafanyia wenzake.
 
Mimi huo ujamaa ulimfanya baba mzazi akawa bladfaken of ze faken. He wasted opportunities and fortunes zilizogharimu familia na jamaa. Sijawahi kuwa proud of him. Na alikua na ujuaji na ubishi wa kihaya faken of faken alimuona Nyerere kama muumba wake.
 
Uzuli wa nchi hiyo matajiri wengi pesa zao za kutafuta wao kwetu wazawa wenye pesa ni mafisadi wamekwiba serikalini
 
Si unaona sasa, ujamaa ulituharibu sana, tena nyie wahaya usingekua ujamaa mngekua mbali sana kimaendeleo ya kila kitu. Uliharibu hadi mentality za watu, ona sasa wachina wanakuja wanajichukulia tu vitu kirahisi rahisi shauri ya upole wa ujamaa.
 
Thread murua kabisa, watanzania tutenge bajeti ndogo ya kutembea hata nchi jirani.. Mpaka unaondoka duniani hata kufika mpakani kwa basi hujawahi. Muhimu kujua watu walivyo na tamaduni tofauti kwenye huu uso wa ardhi
Hume nilenga mimi powa nitajirekebisha nitajitahidi baada ya mavuno kutembelea afirika mashariki
 
Ulivyosema ni asilimia 100 nilikuwa Dakar kikazi mwaka jana mwezi wa Saba ..kuvaa hirizi kwao kawaida kabisa .daladala ni chakavu Sana nitaweka picha .Dakar pale ni magorofa tupu na hakuna fence kama ulivyosema nyumba zimebanana .kwenye msosi kitunguu ni Kila kitu Yani ni kama mboga kuu kwao .Barabara zao ni nzuri sana ..nk
 
Nimekaa pale muda mrefu. Hakika sikuwahi sikia wakiitana KAFIR hata kama ni dini tofauti.
Neno hili Tanzania tunapenda kulitumia.
Katika pitapita zangu niliwahi kusikia huko West Africa kuna msosi maarufu sana hapo na duniani kwa ujumla unaitwa "JOLLOF RICE" kuna Msenegal nilikuwa nae Nairobi nikamuuliza hili suala na igredients za msosi husika akaishia kuniambia nigoogle.Lakini nilivyogoogle nikaona viungo vinavyowekwa humo ni vya kawaida tu licha ya kuwa ni msosi maarufu duniani kutokea Africa,na baada ya kugoogoe zaidi nikaona nchi zote za west Africa zinatengeneza msosi huu lakini Niigeria na Ghana ndio kwa sana..Vipi uwepo wa msosi huu hapo Senegal na je ni kama pilau au biriani tunalokula huku Tabata!?
 
Achana nae huyo, hawa ndio watanzania halisi, wao kila kitu kwao ni fix na kila opportunity kwao ni scam, lolote ambalo hawajawahi kulisikia kwao ni uongo, inasikitisha sana sababu watu wa aina hiyo ndio tunao wengi.
 
na accomodation zao vipi?na hyo ni dakar?
Inategemea unafikia wapi....

Uswahili kupo
Mid town kupo
Town kupo
Kwa kishua kupo...

GUest nyingi ni 10k CFA mpaka 50k CFA inategemea na sehemu.

Nyumba za kupanga 50k CFA kwa studio mpaka 1m CFA kwa mwezi.

Muhimu unakuja kufanya nini..... Hukosi pa kulala.

1 CFA ni kama 4 Tshs.....

Tambua nchi zetu za kiafrica ukishafika hamtashindwana....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…