Smart Gang
JF-Expert Member
- Nov 16, 2022
- 2,013
- 3,406
Senegal
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa mkuu unasema magari ya umma Ni Yale kuuu kuu na huku unasema watu Wana magari latest mbna hatariMziki wao ni mzuri sana ukichagizwa na namna wanavyocheza....
Mji wa Dakar una matajiri haswa. Barabara zao zimejaa magari ya kifahari latest. Majumba ni ya kifahari kwenye sehemu za kishua....
Wasenegal wanapenda kuendeleza vya kwao.
Wawekezaji wengi ni wazawa.
Jamii za wahindi, wachina si wengi kama Tanzania.
Wasenegal hawapendi kulipwa kidogo. Wao kazi ndogo hela nyingi....
Hapana mkuu.Sasa mkuu unasema magari ya umma Ni Yale kuuu kuu na huku unasema watu Wana magari latest mbna hatari
Kuna documentary nimeonaga offcoz magar karibia yote Ni kuu kuu tu pia ya kizamani Sana [emoji38]
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
VIP Zanzibar inamaana hao 2 parcent Ni wakristo ndio panya rodnchi nyingi zenye waislam wengi uhalifu ni mchache sana,, Somalia huko wanakosema kuna vita unaweza kulala hata mlango wazi,, kifupi panya road wakutafuta kwa tochi kama si hakuna kabisa
Huyo rais wao Mack Sally Ni muislamu au mkiristoHali ya hewa ni mchanganyiko...
January mpaka march kuna baridi kiasi.
April - July joto linapanda
July - October ni mvua hivyo vipindi huchanganyika.
Dec ni joto....
Kiwango cha umasikini si sawa na Tanzania. Wametuzidi kiasi kidogo kwenye uhalisia wa maisha sijui kwenye makaratasi.
Mpangilio wa nyumba inategemea na maeneo lakini kwa kiasi wametuzidi.
Tunachowazidi kwao mji mkuu Dakar umejaa. Hvyo ukimiliki kiwanja ni unajenga chote hakuna cha parking wala eneo la kupumzikia. Nyumba zimeungana kabsa. Ila mitaa ipo vyema.
Ni taifa lenye waislamu wengi ila si taifa la kiislamu. Dini kwao ni tamaduni yao. Utaratibu ni wa mfaransa kama mkoloni wao aliyepita. Kumpuzika weekend.
Hawa watu kwa rangi tu ni weusi. Weupe wachache sana ila wapo....
Acha uongo mkuu na jesi wee inamaana umeenda na jesi za timu mbili mbna ubaanda kuwa muongo muongo acha hzoHahaha mkuu....
Simba wanaijua kwa sababu kuna wachezaji wa Senegal wamepita hapo. No less no more.....
Hawa hawafuatilii hata mpira kivile.
Nimevaa jezi ya Yanga sana na wengi husema ni jezi ya Brazili.
Ila ya Simba wanaijua.
Sina data kamili ila narejea msemo wa mheshiniwa JK, akili za kuambiwa changanya na za kwako, bei ya kondoo mmoja inalingana na mradi wa Zahanati????Wana kondoo wao wanaitwa Ladoum kipindi cha sikukuu za Eid bei zake zinaweza kufika mpaka $80,000. Hiyo ni zaidi ya 187M Tshs
View attachment 2560778
Mkuu nidanganye nipate nini?Acha uongo mkuu na jesi wee inamaana umeenda na jesi za timu mbili mbna ubaanda kuwa muongo muongo acha hzo
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Nauli ni kama Bei gan Kwa chopaHabari,
Nchi nyingi zina utaratibu, mila na desturi za maisha. Kutokana na kuzunguka sehemu mbali mbali leo nmeonelea nikuambie yale yahusuyo Senegal ambayo ni tofauti kidogo na nchi yetu ya Tanzania.....
VISA ya Senegal kwa Mtanzania ni on arrival. Ukishaingia Senegal hamna anayekufuatilia ilimradi uwe na passport yako. Visa ikiexpire haubugudhiwi na yeyote. Labda uchokoze mamlaka....
Ila ni vyema kugonga VISA ikiisha.
1. DINI
Upande wa dini waislamu ni asilimia 90 na wakristo ni asilimia 10.
Hii kwa kiasi kikubwa ni nchi iliyojaaliwa kuwa na waislam wengi pamoja na kuwa ilitawaliwa na wafaransa.
Tamaduni za waislam hapa ni tofauti sana na kwetu.
●Wana mji wao mtakatifu unaitwa Touba. Huko asilimia kubwa ya huduma ni bure na ni mji unaojitawala. Huko wanapatikana masheikh wakubwa na watu wanaoitwa Marabuuu... Wanamiliki madrasa ambazo watoto kuanzia wadogo wanalelewa huko.
●Uislam ni mtindo wa maisha kwao ni utamaduni wao. Wanauishi uislamu na uislamu unaishi ndani yao.
●Wanaswali sehemu yoyote muda wa kuswali utakapomkutia. Si barabarani, beach, kituo cha daladala au sehemu yoyote. Usishangae kukuta sehemu wanawake wanajiuza halafu kuna mtu katandika mswala wake anaswali bila bugudha.
●Wanawake waislamu hawavai hijab, nkabu wala chochote wao vazi lolote twende. Ikifika muda wa swala atatoa mtandio wake na kanga atajisitiri anaswali.... Same kwa wanaume. Senegal mpaka wahuni wanaswali....
●Asilimia kubwa hamna ubaguzi wa dini.
2. AMANI
Ni nchi yenye amani kwa kiasi kikubwa na utulivu siasa zao za kistaarabu ingawa kwa sasa Rais aliyepo anamtia kashkashi mpinzani wake Osuman Sonko kashapewa kesi za kutosha.... Siku wakiandamana wapinzani ujue shughuli zinafungwa town....
3. UHALIFU
Kuna asilimia ndogo sana ya uhalifu unaweza kusahau simu yako maeneo kama kariakoo au club au gym na ukaikuta pale pale. Sisemi hakuna wizi ila ni asilimia chache sana.
4. MAKAZI
Mji mkuu Dakar ni mji wa gharama kubwa sana. Bei ya ardhi haikamatiki. Mji umejaa wote na nyumba zinazojengwa ni maghorofa tu. Ukiwa na kiwanja unajenga chote mpaka kwenye mpaka na mwingine anakuja kuunga nyumba yake. Asilimia 95 ya nyumba hazina fense wala parking. Kiwanja kinajaa nyumba.
Kukodi nyumba ni gharama sana kwa Senegal ukifananisha na TZ.
5. VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI.
Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani na raia. Hawana shida na yeyote. Ukikosea wanakurekebisha. Usipowagusa hawana habari na yeyote. Unaweza kukaa miezi hata kusimamishwa na traffic usisimamishwe. Unaweza safiri Dar to Mbeya hakuna wa kukusimamisha.
Usishangae kukuta mwanajeshi na raia wote wamevaa gwanda wanapiga story.
Au konda kavaa gwanda za jeshi (si za nchi yao) na hakuna shida.
6. MIUNDOMBINU.
Barabara za mjini zimejengeka vilivyo. Kuanzia flyover, bypass n.k ujenzi unafanyika kila sehemu.
Umeme na maji ni nadra kukatika.
7. MICHEZO
Wananchi wa Senegal wanapenda kufanya mazoezi sana. Usishangae beach zao kujaa watu wanafanya mazoezi. Barabara zimejaa watu wanafanya mazoezi. Wao ni mazoezi na mazoezi na wao.
Tofauti yao ni kwamba hawaendi viwanjani kuangalia michezo. Pamoja na kuwa na viwanja vingi. Wachezaji wengi wanatoka kwny academies... Hata ligi zao si maarufu kwa wasenegal wengi...
Ndio maana timu ya taifa inafanya vyema kuliko klabu....
8. VYAKULA
Bora umnyime chochote msenegal kuliko mkate. Ukienda mgahawani cha kwanza ni mkate kabla ya kula. Mkate ni deal...
Wana vyakula vingi maarufu kama Chepujam n.k.
Hakuna ugali na wanaushangaa
Kitunguu kwao kipo kwenye kila mlo.
Wanapenda kahawa sana na sukari.
9. STAREHE NA POMBE
Hivi vinapatikana sehemu zinazokaliwa na watu wa nje. Sehemu kama almadies, mji wa St. LUOIS.
Sehemu kubwa ya Senegal hawauzi pombe.... Klabu zao zinafunguliwa saa 6-9 jumatatu asubuhi saa 1 unakutana na makundi ya vijana wanatoka klabu.
sigara zake makasha yana picha za kutisha sana .
10. LUGHA
Waliosoma wanajua kifaransa, wananchi wengi wanaongea WOLOF ingawa si wote.
Lugha ya ofisini ni kifaransa...
11. UWEPO WA WATU KUTOKA EAST AFRICA.
Jamii ya watu kutoka East Afrika ni wachache sana. Unaweza kukaa miezi 6 ukakutana na mmoja. Watanzania almost hakuna bora wakenya...
msanii maarufu wa East Afrika ni Diamond Platnum. Na watu wanamjua Shilole na nyimbo yake ya Chura kuliko hata Ali Kiba.
Wanamkubali sana Magufuli.
Zanzibar ni maarufu sana.
Sheikh Sharif anajulikana sana na ni maarufu mno.
Simba inajulikana kuliko Yanga kwanza Yanga hawaijui kabsa... Big up kwa Simba wanawakilisha.
12. UVAAJI WA HIRIZI,SHANGA VIUNONI WAZIWAZI NI KAWAIDA.
Usishangae kukutana na mtu kajitwisha hirizi yake na hana muda na mtu. Hii inanikumbusha yule mchezaji wa Simba Pape N'daw kutoka Senwgal alikutwa na hirizi kwenye moja ya mechi. Kwao ni kawaida kama bangili.
Au mwanamke kavaa shanga zake kiunoni na top na wala hamna muda na watu hawashangai.
Pia ni nadra kuona mwanaume anapishana na mwanamke na kumuangalia.
13. KAZI MWISHO IJUMAA
Ni nadra sana kukuta ofisi imefunguliwa jumamosi yani hata kwa ofisi za madalali weekend wanafunga tofauti na kwenye real state agencies wao weekend ndio biashara inanoga.
14. SHULE
Wanafunzi wa shule nyingi hawavai uniform ni mara chache sana.
Shule hufungwa kipindi cha mvua. Yani kuanzia july mpaka September.
Sijawahi ona watu wanaogopa maji kama wasenegal. Dereva akiona kadimbwi anageuza na hawapiti hapo. Sijui nini kiliwahi wakumba...
N.k n.k n.k
15. USAFIRI WA UMA NA BINAFSI.
USafiri wa uma kwa Senegal yani daladala na Tax ni magari yaliyochoka. Unaweza kushuka airport pale ukakuta Tax zimechoka hatari usifikiri utatafuta na kupata mpya hizo ndio zilizopo, atleast sikuhizi uber yao (YANGO) wanaingiza gari mpya.
Daladala ndio usiseme.
Wanatumia pia farasi kama usafiri anafungwa tela.
Magari binafsi huwezi kuingiza gari kuu kuu mwisho miaka mitano.
Brand za magari ni EUROPEAN. Toyota ni za kutafuta na pia ni ghali kwa kuwa zinatoka Japan Mbali.
Magari yao ni LHD.
AJALI
Senegal hata ukinunua gari leo kesho unaweza kuwa umechubuliwa. Raia hawajali kuhusu magari wao magari kuchubuana ni kawaida na sio kesi. Watu wanaweza gongana magari waaishia kusem INSHALLAH. Hao wanasepa hakuna kesi....
Madereva wa Senegal wanapenda kukimbiza sana magari. Sijui wanawahi wapi speed 120 kwao ni kawaida.
*************************************
Dakar na omba omba ni kama chanda na pete....
Nikiendelea kukumbuka nitaendelea kujazia kadri ya uwezo maana ni muda umepita tangu nipite pale.
Wastani wa dola 1000 kwenda na kurudi....Nauli ni kama Bei gan Kwa chopa
Macky Sall ni muislamu.Huyo rais wao Mack Sally Ni muislamu au mkiristo
Nae nasikia wanamtakaa asitawake kwa temu ya tatu
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wanauza na wanafuga kwa wanaoamini.Huko nguruwe wanauza kwani😳
Vipi kuhusu fursa za kiuchumi zipo,Wanauza na wanafuga kwa wanaoamini.
Nilipata kwenda mkoa mmoja unaitwa KAOLACK kule nguruwe wanaachiwa tu wanazagaa kama mbuzi....
Dakar nilihudhuria mgahawa mmoja yule mpishi wa kitimoto si mkristo.....
Fursa za kiuchumi zipo nyingi....Vipi kuhusu fursa za kiuchumi zipo,
Yaan Kwa wasomi na sie Watumia nguvu.
Uhakika WA kutusua upoo.
Hahahahawale jama zetu wanadhani unazungumzia saudi arabia wamenuna
Sasa kwa akili yako zanzibar kuna panya road??? Na hiyo Tanzania uliyoutolea mfano kwani nchi ya kiislam??VIP Zanzibar inamaana hao 2 parcent Ni wakristo ndio panya rod
Mbona magerezani na police kote nchini kumejaha waislamu tupu
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kitunguu kwenye kila chakula nimewaza uji wa kitunguu