Peramiho yetu
JF-Expert Member
- May 25, 2018
- 5,303
- 14,983
Ukipata muda tuelezee bendi yao iitwayo AFRICANDO nawakubali Sana hao jamaa hasa wimbo wao wa AISHA
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
pesa ipo, pesa ikiwepo hua hakuna kuuliza bei tunaangalia ubora 😀Tunaomba maelezo ya hizo dola themanini kwa huyo Ladoum, ni hela nyingi sana aise.
Ana kitu gani special?
Usiishi kwa kuchagua cha kujifunza chief. Hata makosa nayo ni shule. Wewe umeandika ya Senegal tujifunze lakin hukuandika na mabaya yao.Mkuu siku zote ukitaka kutoboa, jifunze kwa waliotoboa. Lakini pia kila jamii ina mapungufu yake. Jitahidi kadri unavyoweza kuangalia yale mazuri. Focus on the positive aspects. Ya utapeli achana nayo. Hata kama yana ukweli hayana msaada.
Huku Dar panya road wanatoka uswahilini, na uswahilini wakazi wengi ni waislam.nchi nyingi zenye waislam wengi uhalifu ni mchache sana,, Somalia huko wanakosema kuna vita unaweza kulala hata mlango wazi,, kifupi panya road wakutafuta kwa tochi kama si hakuna kabisa
nimependa ishu ya mkate na biashara ya pombe nilikuwa nataka kujua kuhusu uraia kuupata au nikiamua kukaa huko opportunity zilizoko kwa wageniHabari,
Nchi nyingi zina utaratibu, mila na desturi za maisha. Kutokana na kuzunguka sehemu mbali mbali leo nmeonelea nikuambie yale yahusuyo Senegal ambayo ni tofauti kidogo na nchi yetu ya Tanzania.....
VISA ya Senegal kwa Mtanzania ni on arrival. Ukishaingia Senegal hamna anayekufuatilia ilimradi uwe na passport yako. Visa ikiexpire haubugudhiwi na yeyote. Labda uchokoze mamlaka....
Ila ni vyema kugonga VISA ikiisha.
1. DINI
Upande wa dini waislamu ni asilimia 90 na wakristo ni asilimia 10.
Hii kwa kiasi kikubwa ni nchi iliyojaaliwa kuwa na waislam wengi pamoja na kuwa ilitawaliwa na wafaransa.
Tamaduni za waislam hapa ni tofauti sana na kwetu.
●Wana mji wao mtakatifu unaitwa Touba. Huko asilimia kubwa ya huduma ni bure na ni mji unaojitawala. Huko wanapatikana masheikh wakubwa na watu wanaoitwa Marabuuu... Wanamiliki madrasa ambazo watoto kuanzia wadogo wanalelewa huko.
●Uislam ni mtindo wa maisha kwao ni utamaduni wao. Wanauishi uislamu na uislamu unaishi ndani yao.
●Wanaswali sehemu yoyote muda wa kuswali utakapomkutia. Si barabarani, beach, kituo cha daladala au sehemu yoyote. Usishangae kukuta sehemu wanawake wanajiuza halafu kuna mtu katandika mswala wake anaswali bila bugudha.
●Wanawake waislamu hawavai hijab, nkabu wala chochote wao vazi lolote twende. Ikifika muda wa swala atatoa mtandio wake na kanga atajisitiri anaswali.... Same kwa wanaume. Senegal mpaka wahuni wanaswali....
●Asilimia kubwa hamna ubaguzi wa dini.
2. AMANI
Ni nchi yenye amani kwa kiasi kikubwa na utulivu siasa zao za kistaarabu ingawa kwa sasa Rais aliyepo anamtia kashkashi mpinzani wake Osuman Sonko kashapewa kesi za kutosha.... Siku wakiandamana wapinzani ujue shughuli zinafungwa town....
3. UHALIFU
Kuna asilimia ndogo sana ya uhalifu unaweza kusahau simu yako maeneo kama kariakoo au club au gym na ukaikuta pale pale. Sisemi hakuna wizi ila ni asilimia chache sana.
4. MAKAZI
Mji mkuu Dakar ni mji wa gharama kubwa sana. Bei ya ardhi haikamatiki. Mji umejaa wote na nyumba zinazojengwa ni maghorofa tu. Ukiwa na kiwanja unajenga chote mpaka kwenye mpaka na mwingine anakuja kuunga nyumba yake. Asilimia 95 ya nyumba hazina fense wala parking. Kiwanja kinajaa nyumba.
Kukodi nyumba ni gharama sana kwa Senegal ukifananisha na TZ.
5. VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI.
Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani na raia. Hawana shida na yeyote. Ukikosea wanakurekebisha. Usipowagusa hawana habari na yeyote. Unaweza kukaa miezi hata kusimamishwa na traffic usisimamishwe. Unaweza safiri Dar to Mbeya hakuna wa kukusimamisha.
Usishangae kukuta mwanajeshi na raia wote wamevaa gwanda wanapiga story.
Au konda kavaa gwanda za jeshi (si za nchi yao) na hakuna shida.
6. MIUNDOMBINU.
Barabara za mjini zimejengeka vilivyo. Kuanzia flyover, bypass n.k ujenzi unafanyika kila sehemu.
Umeme na maji ni nadra kukatika.
7. MICHEZO
Wananchi wa Senegal wanapenda kufanya mazoezi sana. Usishangae beach zao kujaa watu wanafanya mazoezi. Barabara zimejaa watu wanafanya mazoezi. Wao ni mazoezi na mazoezi na wao.
Tofauti yao ni kwamba hawaendi viwanjani kuangalia michezo. Pamoja na kuwa na viwanja vingi. Wachezaji wengi wanatoka kwny academies... Hata ligi zao si maarufu kwa wasenegal wengi...
Ndio maana timu ya taifa inafanya vyema kuliko klabu....
8. VYAKULA
Bora umnyime chochote msenegal kuliko mkate. Ukienda mgahawani cha kwanza ni mkate kabla ya kula. Mkate ni deal...
Wana vyakula vingi maarufu kama Chepujam n.k.
Hakuna ugali na wanaushangaa
Kitunguu kwao kipo kwenye kila mlo.
Wanapenda kahawa sana na sukari.
9. STAREHE NA POMBE
Hivi vinapatikana sehemu zinazokaliwa na watu wa nje. Sehemu kama almadies, mji wa St. LUOIS.
Sehemu kubwa ya Senegal hawauzi pombe.... Klabu zao zinafunguliwa saa 6-9 jumatatu asubuhi saa 1 unakutana na makundi ya vijana wanatoka klabu.
sigara zake makasha yana picha za kutisha sana .
10. LUGHA
Waliosoma wanajua kifaransa, wananchi wengi wanaongea WOLOF ingawa si wote.
Lugha ya ofisini ni kifaransa...
11. UWEPO WA WATU KUTOKA EAST AFRICA.
Jamii ya watu kutoka East Afrika ni wachache sana. Unaweza kukaa miezi 6 ukakutana na mmoja. Watanzania almost hakuna bora wakenya...
msanii maarufu wa East Afrika ni Diamond Platnum. Na watu wanamjua Shilole na nyimbo yake ya Chura kuliko hata Ali Kiba.
Wanamkubali sana Magufuli.
Zanzibar ni maarufu sana.
Sheikh Sharif anajulikana sana na ni maarufu mno.
Simba inajulikana kuliko Yanga kwanza Yanga hawaijui kabsa... Big up kwa Simba wanawakilisha.
12. UVAAJI WA HIRIZI,SHANGA VIUNONI WAZIWAZI NI KAWAIDA.
Usishangae kukutana na mtu kajitwisha hirizi yake na hana muda na mtu. Hii inanikumbusha yule mchezaji wa Simba Pape N'daw kutoka Senwgal alikutwa na hirizi kwenye moja ya mechi. Kwao ni kawaida kama bangili.
Au mwanamke kavaa shanga zake kiunoni na top na wala hamna muda na watu hawashangai.
Pia ni nadra kuona mwanaume anapishana na mwanamke na kumuangalia.
13. KAZI MWISHO IJUMAA
Ni nadra sana kukuta ofisi imefunguliwa jumamosi yani hata kwa ofisi za madalali weekend wanafunga tofauti na kwetu kwenye real state agencies wao weekend ndio biashara inanoga.
14. SHULE
Wanafunzi wa shule nyingi hawavai uniform ni mara chache sana.
Shule hufungwa kipindi cha mvua. Yani kuanzia july mpaka September.
Sijawahi ona watu wanaogopa maji kama wasenegal. Dereva akiona kadimbwi anageuza na hawapiti hapo. Sijui nini kiliwahi wakumba...
N.k n.k n.k
15. USAFIRI WA UMA NA BINAFSI.
USafiri wa uma kwa Senegal yani daladala na Tax ni magari yaliyochoka. Unaweza kushuka airport pale ukakuta Tax zimechoka hatari usifikiri utatafuta na kupata mpya hizo ndio zilizopo, atleast sikuhizi uber yao (YANGO) wanaingiza gari mpya.
Daladala ndio usiseme.
Wanatumia pia farasi kama usafiri anafungwa tela.
Magari binafsi huwezi kuingiza gari kuu kuu mwisho miaka mitano.
Brand za magari ni EUROPEAN. Toyota ni za kutafuta na pia ni ghali kwa kuwa zinatoka Japan Mbali.
Magari yao ni LHD.
AJALI
Senegal hata ukinunua gari leo kesho unaweza kuwa umechubuliwa. Raia hawajali kuhusu magari wao magari kuchubuana ni kawaida na sio kesi. Watu wanaweza gongana magari waaishia kusem INSHALLAH. Hao wanasepa hakuna kesi....
Madereva wa Senegal wanapenda kukimbiza sana magari. Sijui wanawahi wapi speed 120 kwao ni kawaida.
*************************************
Dakar na omba omba ni kama chanda na pete....
Nikiendelea kukumbuka nitaendelea kujazia kadri ya uwezo maana ni muda umepita tangu nipite pale.
Sina interest na mabaya yao mkuu.Usiishi kwa kuchagua cha kujifunza chief. Hata makosa nayo ni shule. Wewe umeandika ya Senegal tujifunze lakin hukuandika na mabaya yao.
Jamaa wako poa mno. Hawana makuu.
Sea plaza sijawahi kufika.
Supermarket nyingi ni AUCHAN mfaransa. Pia kuna CASSINO SUPERMARKETS na nyingine nyingi.
Nipatapo wasaha kurejea nchi ile nitazunguka zaidi...
Very good country.
Then kwa mtu uliyempa hii story akienda akakumbana na Mambo tofauti huon ushampoteza. Siku zote ukifanya utafiti njoo na ubaya na uzur ucje na upande mmoja tu. Maana hapa tupo kujifunza. Na hili hukuliandika huku kwaajili yako ni kwaajili yetu pia. Tunajifunza kila cku kwenye hasi na chanyaSina interest na mabaya yao mkuu.
Hpn mkuu kwenye swala la jesi skip tu mnk Lina utata umejaza chumvi nyingi SanaMkuu nidanganye nipate nini?
Wapi nimesema mimi nimevaa jezi ya simba? Siwezi kuvaa na sitavaa.
Nimesema jezi ya simba wanaifahamu.....
Wee ndio umekurupuka kujumuisha panya road na uislamu at unasema sehemu inayokaliwa na waislamu Hakuna ualifu Nani kakudanganya wee kijana wa mnyazi munguSasa kwa akili yako zanzibar kuna panya road??? Na hiyo Tanzania uliyoutolea mfano kwani nchi ya kiislam??
Umekurupuka!!
.mkuu Ni serious hili hyo mbno ilinipita naomba link nifatilie Jambo HiloHukusema Rais wa Senegal alivyomwambia Rais Ruto alipotaka kuingia kwenye mkutano wa AU.
"Wewe hatukuruhusu kuingia kwenye huu mkutano. Rudi nyumbani kwako,una matatizo ya Uchaguzi kule,nenda kayatanzue yale matatizo kwanza. Zifungue server,kama wanavyosema Wapinzani. Yule kiongozi wa Oppostion anasema umeiba kura. Kwanza,hata sijui kama ni sahihi kumwita yule kuwa ni kiongozi wa Opposition. Yule,labda ndiye rais.
Unaiba kura halafu unadhani utaingia hapa? Sijali kama unanitazama kwa kukunja sura."(Hii sentensi aliirudia mara mbili,tatu in the course of his talk)
Wachina wanalelewa na Serikali, miaka ijayo sijui hali itakuwajeMziki wao ni mzuri sana ukichagizwa na namna wanavyocheza....
Mji wa Dakar una matajiri haswa. Barabara zao zimejaa magari ya kifahari latest. Majumba ni ya kifahari kwenye sehemu za kishua....
Wasenegal wanapenda kuendeleza vya kwao.
Wawekezaji wengi ni wazawa.
Jamii za wahindi, wachina si wengi kama Tanzania.
Wasenegal hawapendi kulipwa kidogo. Wao kazi ndogo hela nyingi....
Ukweli uko hivyo na hiyo haiwezi kubadilika,, kama umenuna pasuka,, nchi nyingi zenye waislam wengi na zinazofuata tamaduni za uislam kama hii Senegal aliyoitolea mfano mleta uzi,, kuna usalama mkubwa mno,, si kwamba naingiza udini la hasha,, isipokuwa huwezi kuizungumzia Senegal pasi na kutaja imani yao kwa kuwa asilimia 90 ni wa imani moja,, south Africa ndio nchi inayoongoza kwa wakristo Africa na marekani ndio nchi inayoongoza kwa wakristo duniani na ndizo zinazoongoza kwa uhalifuWee ndio umekurupuka kujumuisha panya road na uislamu at unasema sehemu inayokaliwa na waislamu Hakuna ualifu Nani kakudanganya wee kijana wa mnyazi mungu
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Bora umenimbia huyo mweu alinibishia at sehem zinazokaliwa na waislamu Hakuna ualifu akwwende temekeHuku Dar panya road wanatoka uswahilini, na uswahilini wakazi wengi ni waislam.
Huna data wew unajidanganya Kisha unalitetea dini yenu ya mnyanz badilikeni waleeni watot wenu kwa njia sahih mnadekeza watot Kisha mnakuja kuisifu Senegal kuwa waislmu wake Ni mwaaminifu ,Ni waaminifu kwa kuwa waliwalea watot kimaadiliUkweli uko hivyo na hiyo haiwezi kubadilika,, kama umenuna pasuka,, nchi nyingi zenye waislam wengi na zinazofuata tamaduni za uislam kama hii Senegal aliyoitolea mfano mleta uzi,, kuna usalama mkubwa mno,, si kwamba naingiza udini la hasha,, isipokuwa huwezi kuizungumzia Senegal pasi na kutaja imani yao kwa kuwa asilimia 90 ni wa imani moja,, south Africa ndio nchi inayoongoza kwa wakristo Africa na marekani ndio nchi inayoongoza kwa wakristo duniani na ndizo zinazoongoza kwa uhalifu
Ndio maana aliwa Rip akina Saannane,Azory,Kanguye na wenzao!Umesikia kabisa huko hakuna wezi na wanapenda amani na wanapenda vyao,na ndio Magufuli alivipambania
Wewe ndio umechomekea hilo la Jiwe hakuna lolote.Hapana. Si watu wa kufuatilia siasa za Tanzania. Ila kwa namna moja au nyingine baadhi wanamjua.
Lengo la uzi ni kueleza yale yaliyo ground tukiachana na gugo....
Hujashangaa CHURA ya Snura ni maarufu huku?