Usiyoyajua kuhusu Senegal

Usiyoyajua kuhusu Senegal


Kwenye huu uzi nilijaribu kuongelea hilo.
Mkuu nimesoma uzi wako hakika ni kweli tupu..... Watanzania hatusafiri na tukisafiri tunawaza kurudi home muda wote. Tuna home sickness.... Na ukisafiri kila mtu anakuuliza "Unarudi lini?"
 
Aina ya kondoo wao ni tofauti na wa kwetu....

Ni wakubwa sana....
Oh Kama specie ya kondoo waliyonayo wao ni tofauti na yetu, bhasi soko lazima liwe dogo. Ila kila kitu kinahitaji research at first place. Huwezi jua labda na Aina hii ya kwetu ikapendwa lakini kwa bei tofauti na hiyo ya specie waliyoizoea mkuu.
 
Kuna jamaa yangu alikwenda kufanya kazi Senegal (UN) akamuacha Mke wake TZ. Si nikamtembelea wakati nimeenda katika mkutano. Sikuamini alikuwa ashatekwa na msenegalise mama ambaye walikuwa ofisi moja. Kibarua kilipoisha alirudi na sandarusi tu. Ikabidi tumpigie magoti nke yake ya hapa ili asiadhirike. Wasenegalise wanawake, we acha tu.
Ni silka ya wanawake wengi wa Afrika Magharibi lazima mwanaume uwe ngangari. Sasa wanaume wenyewe hawa wakitanzania wa kulialia kuteswa na mapenzi type za akina lavalava desh desh mabishololo watawawezea wapi wanawake wa Afrika Magharibi.
Wanawake wa huko lazima uwe ngangari la sivyo utapelekwesha puta sana.
 
Kule inabidi utumie mfumo dume.
Ni silka ya wanawake wengi wa Afrika Magharibi lazima mwanaume uwe ngangari. Sasa wanaume wenyewe hawa wakitanzania wa kulialia kuteswa na mapenzi type za akina lavalava desh desh mabishololo watawawezea wapi wanawake wa Afrika Magharibi.
Wanawake wa huko lazima uwe ngangari la sivyo utapelekwesha puta sana.
 
Mkuu nimesoma uzi wako hakika ni kweli tupu..... Watanzania hatusafiri na tukisafiri tunawaza kurudi home muda wote. Tuna home sickness.... Na ukisafiri kila mtu anakuuliza "Unarudi lini?"
Hii ipo damuni ,, ona Tu hata watumishi wa serikali hapahapa Tanzania wanapambama kila kukicha kutafuta uhamisho kurud Mikoa waliyozaliwa
 
Jemima,
Hizo ni propaganda tu si kila muislamu ni mbaya na si kila mkristo ni mzuri.

Binafsi nimeshuhudia watu hawa hawana shida tena ukimuambia ni mkristo anafurahi.
Makanisa yapo na hamna anayekubagua.

Wanaishi na uislamu kama tamaduni yao kuliko imani.....
Uislamu upo ndani yao.....
Uislam wa kweli ni Lifestyle zaidi kuliko Dini. Ukristo ni Dini zaidi kuliko Lifestyle. Mimi ni mkristo ila nimegundua hili jambo.
 
Mziki wao ni mzuri sana ukichagizwa na namna wanavyocheza....

Mji wa Dakar una matajiri haswa. Barabara zao zimejaa magari ya kifahari latest. Majumba ni ya kifahari kwenye sehemu za kishua....

Wasenegal wanapenda kuendeleza vya kwao.
Wawekezaji wengi ni wazawa.
Jamii za wahindi, wachina si wengi kama Tanzania.
Wasenegal hawapendi kulipwa kidogo. Wao kazi ndogo hela nyingi....
Mkuu ipo sahihi sana. Kuna fovumentary ya African Indian, hii wameeleza kuwa upoingia ndani from Indian ocean wahindi wanapungua sana. Tegemea saja kuwaona wahindi along the indian ocean napo ni EA na SA
 
Habari,
Nchi nyingi zina utaratibu, mila na desturi za maisha. Kutokana na kuzunguka sehemu mbali mbali leo nmeonelea nikuambie yale yahusuyo Senegal ambayo ni tofauti kidogo na nchi yetu ya Tanzania.....

VISA ya Senegal kwa Mtanzania ni on arrival. Ukishaingia Senegal hamna anayekufuatilia ilimradi uwe na passport yako. Visa ikiexpire haubugudhiwi na yeyote. Labda uchokoze mamlaka....
Ila ni vyema kugonga VISA ikiisha.


1. DINI
Upande wa dini waislamu ni asilimia 90 na wakristo ni asilimia 10.
Hii kwa kiasi kikubwa ni nchi iliyojaaliwa kuwa na waislam wengi pamoja na kuwa ilitawaliwa na wafaransa.
Tamaduni za waislam hapa ni tofauti sana na kwetu.

●Wana mji wao mtakatifu unaitwa Touba. Huko asilimia kubwa ya huduma ni bure na ni mji unaojitawala. Huko wanapatikana masheikh wakubwa na watu wanaoitwa Marabuuu... Wanamiliki madrasa ambazo watoto kuanzia wadogo wanalelewa huko.

●Uislam ni mtindo wa maisha kwao ni utamaduni wao. Wanauishi uislamu na uislamu unaishi ndani yao.

●Wanaswali sehemu yoyote muda wa kuswali utakapomkutia. Si barabarani, beach, kituo cha daladala au sehemu yoyote. Usishangae kukuta sehemu wanawake wanajiuza halafu kuna mtu katandika mswala wake anaswali bila bugudha.

●Wanawake waislamu hawavai hijab, nkabu wala chochote wao vazi lolote twende. Ikifika muda wa swala atatoa mtandio wake na kanga atajisitiri anaswali.... Same kwa wanaume. Senegal mpaka wahuni wanaswali.

●Asilimia kubwa hamna ubaguzi wa dini.

2. AMANI
Ni nchi yenye amani kwa kiasi kikubwa na utulivu siasa zao za kistaarabu ingawa kwa sasa Rais aliyepo anamtia kashkashi mpinzani wake Osuman Sonko kashapewa kesi za kutosha.... Siku wakiandamana wapinzani ujue shughuli zinafungwa town.

3. UHALIFU
Kuna asilimia ndogo sana ya uhalifu unaweza kusahau simu yako maeneo kama kariakoo au club au gym na ukaikuta pale pale. Sisemi hakuna wizi ila ni asilimia chache sana.

4. MAKAZI
Mji mkuu Dakar ni mji wa gharama kubwa sana. Bei ya ardhi haikamatiki. Mji umejaa wote na nyumba zinazojengwa ni maghorofa tu. Ukiwa na kiwanja unajenga chote mpaka kwenye mpaka na mwingine anakuja kuunga nyumba yake. Asilimia 95 ya nyumba hazina fense wala parking. Kiwanja kinajaa nyumba.

Kukodi nyumba ni gharama sana kwa Senegal ukifananisha na TZ.

5. VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI
Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani na raia. Hawana shida na yeyote. Ukikosea wanakurekebisha. Usipowagusa hawana habari na yeyote. Unaweza kukaa miezi hata kusimamishwa na traffic usisimamishwe. Unaweza safiri Dar to Mbeya hakuna wa kukusimamisha.

Usishangae kukuta mwanajeshi na raia wote wamevaa gwanda wanapiga story.
Au konda kavaa gwanda za jeshi (si za nchi yao) na hakuna shida.

6. MIUNDOMBINU
Barabara za mjini zimejengeka vilivyo. Kuanzia flyover, bypass n.k ujenzi unafanyika kila sehemu.

Umeme na maji ni nadra kukatika.

7. MICHEZO
Wananchi wa Senegal wanapenda kufanya mazoezi sana. Usishangae beach zao kujaa watu wanafanya mazoezi. Barabara zimejaa watu wanafanya mazoezi. Wao ni mazoezi na mazoezi na wao.

Tofauti yao ni kwamba hawaendi viwanjani kuangalia michezo. Pamoja na kuwa na viwanja vingi. Wachezaji wengi wanatoka kwny academies... Hata ligi zao si maarufu kwa wasenegal wengi.

Ndio maana timu ya taifa inafanya vyema kuliko klabu....

8. VYAKULA
Bora umnyime chochote msenegal kuliko mkate. Ukienda mgahawani cha kwanza ni mkate kabla ya kula. Mkate ni deal.

Wana vyakula vingi maarufu kama Chepujam n.k.
Hakuna ugali na wanaushangaa

Kitunguu kwao kipo kwenye kila mlo.
Wanapenda kahawa sana na sukari.

9. STAREHE NA POMBE
Hivi vinapatikana sehemu zinazokaliwa na watu wa nje. Sehemu kama almadies, mji wa St. LUOIS. Sehemu kubwa ya Senegal hawauzi pombe. Klabu zao zinafunguliwa saa 6-9 Jumatatu asubuhi saa 1 unakutana na makundi ya vijana wanatoka klabu.

sigara zake makasha yana picha za kutisha sana .

10. LUGHA
Waliosoma wanajua kifaransa, wananchi wengi wanaongea WOLOF ingawa si wote.
Lugha ya ofisini ni kifaransa...

11. UWEPO WA WATU KUTOKA EAST AFRICA
Jamii ya watu kutoka East Afrika ni wachache sana. Unaweza kukaa miezi 6 ukakutana na mmoja. Watanzania almost hakuna bora Wakenya.

Msanii maarufu wa East Afrika ni Diamond Platnum. Na watu wanamjua Shilole na nyimbo yake ya Chura kuliko hata Ali Kiba.

Wanamkubali sana Magufuli.

Zanzibar ni maarufu sana.

Sheikh Sharif anajulikana sana na ni maarufu mno.

Simba inajulikana kuliko Yanga kwanza Yanga hawaijui kabsa... Big up kwa Simba wanawakilisha.

12. UVAAJI WA HIRIZI, SHANGA VIUNONI WAZIWAZI NI KAWAIDA
Usishangae kukutana na mtu kajitwisha hirizi yake na hana muda na mtu. Hii inanikumbusha yule mchezaji wa Simba Pape N'daw kutoka Senegal alikutwa na hirizi kwenye moja ya mechi. Kwao ni kawaida kama bangili.
Au mwanamke kavaa shanga zake kiunoni na top na wala hamna muda na watu hawashangai.
Pia ni nadra kuona mwanaume anapishana na mwanamke na kumuangalia.

13. KAZI MWISHO IJUMAA
Ni nadra sana kukuta ofisi imefunguliwa jumamosi yani hata kwa ofisi za madalali weekend wanafunga tofauti na kwetu kwenye real state agencies wao weekend ndio biashara inanoga.

14. SHULE
Wanafunzi wa shule nyingi hawavai uniform ni mara chache sana. Shule hufungwa kipindi cha mvua. Yaani kuanzia july mpaka September.

Sijawahi ona watu wanaogopa maji kama wasenegal. Dereva akiona kadimbwi anageuza na hawapiti hapo. Sijui nini kiliwahi wakumba.
N.k n.k n.k

15. USAFIRI WA UMMA NA BINAFSI
Usafiri wa umma kwa Senegal yaani daladala na Tax ni magari yaliyochoka. Unaweza kushuka airport pale ukakuta Tax zimechoka hatari usifikiri utatafuta na kupata mpya hizo ndio zilizopo, atleast siku hizi uber yao (YANGO) wanaingiza gari mpya.

Daladala ndio usiseme.
Wanatumia pia farasi kama usafiri anafungwa tela.
Magari binafsi huwezi kuingiza gari kuu kuu mwisho miaka mitano.
Brand za magari ni EUROPEAN. Toyota ni za kutafuta na pia ni ghali kwa kuwa zinatoka Japan Mbali.

Magari yao ni LHD

AJALI
Senegal hata ukinunua gari leo kesho unaweza kuwa umechubuliwa. Raia hawajali kuhusu magari wao magari kuchubuana ni kawaida na sio kesi. Watu wanaweza gongana magari waaishia kusem INSHALLAH. Hao wanasepa hakuna kesi.

Madereva wa Senegal wanapenda kukimbiza sana magari. Sijui wanawahi wapi speed 120 kwao ni kawaida.

Dakar na ombaomba ni kama chanda na pete.

Nikiendelea kukumbuka nitaendelea kujazia kadri ya uwezo maana ni muda umepita tangu nipite pale.
Vpi mkuu, hapo jirani Gambia, ulifanikiwa kufika pia!?
 
Back
Top Bottom