Usiyoyajua kuhusu Senegal

Usiyoyajua kuhusu Senegal

Katika pitapita zangu niliwahi kusikia huko West Africa kuna msosi maarufu sana hapo na duniani kwa ujumla unaitwa "JOLLOF RICE" kuna Msenegal nilikuwa nae Nairobi nikamuuliza hili suala na igredients za msosi husika akaishia kuniambia nigoogle.Lakini nilivyogoogle nikaona viungo vinavyowekwa humo ni vya kawaida tu licha ya kuwa ni msosi maarufu duniani kutokea Africa,na baada ya kugoogoe zaidi nikaona nchi zote za west Africa zinatengeneza msosi huu lakini Niigeria na Ghana ndio kwa sana..Vipi uwepo wa msosi huu hapo Senegal na je ni kama pilau au biriani tunalokula huku Tabata!?
Ni kama biriani au tuseme pilau... Ila wanaweka viungo zaidi. Wanachanganya samaki nyama humo humo....

Ni kizuri. Kina pilipili kwa mbali.
Ni kitamu.
 
Ulivyosema ni asilimia 100 nilikuwa Dakar kikazi mwaka jana mwezi wa Saba ..kuvaa hirizi kwao kawaida kabisa .daladala ni chakavu Sana nitaweka picha .Dakar pale ni magorofa tupu na hakuna fence kama ulivyosema nyumba zimebanana .kwenye msosi kitunguu ni Kila kitu Yani ni kama mboga kuu kwao .Barabara zao ni nzuri sana ..nk
Hakika mkuu. Tulipishana kidogo sana.
 
YOFF LAYENE MOSQUE... Upo baharini uwanja huo hujaa sana siku kama ya kesho....
20230322_161408.jpg
 
Naenda Senegal mwezi wa 9, vipi hawazingui airport? Maana niliendaga Nigeria niliombwa Rushwa nikajuta.
Ukiwa na invitation letter hawazingui.
Muhimu uwe na address unapoenda.
Invitation letter.
Passport safi....
Sometime ukiwa na mizigo mingi mfano bidhaa watakuomba chochote max usd 50...

All in all utaingia tu.
Tax mpaka Dakar center ni 20000 CFA kutoka airport.
 
Back
Top Bottom