Usiyoyajua kuhusu Senegal

Usiyoyajua kuhusu Senegal

Biashara
Almost mazao yao yote wanaimport kutoka nje. Matunda ni gharama sana.
Mchele unahitajika sana. Vitunguu...

Ni watu wanaopenda madini. Kama una biashara hiyo ni nzuri.

Kazi
Kama unafahamu kifaransa na una elimu nzuri kupata kazi ni rahisi si watu wa chap chap kama WaTz so ni easy kukubalika.

Mifugo....
Ujenzi
Mawasiliano
Consultation...

Fursa zipo nyingi kama utajua Kifaransa na una mtaji wa kuanzia.

Kuanzisha kampuni ni rahisi sana na procesa ni fasta.....
 
Ni kama maeneo mengi yapo kwenye ujenzi endelevu. Nilikatiza maeneo ya Ile beach kuelekea Ubalozi wa Marekani, Kuna jamaa wanapiga jani wapo kihuni ila hawana madhara.

Nilijuta kutokufaham Kifaransa
Yes nchi inajengwa kila sehemu.....

Wahuni wa huku si wakabaji.... Ni nadra matukio hayo kutokea ingawa yapo...
 
Habari,
Nchi nyingi zina utaratibu, mila na desturi za maisha. Kutokana na kuzunguka sehemu mbali mbali leo nmeonelea nikuambie yale yahusuyo Senegal ambayo ni tofauti kidogo na nchi yetu ya Tanzania.....

VISA ya Senegal kwa Mtanzania ni on arrival. Ukishaingia Senegal hamna anayekufuatilia ilimradi uwe na passport yako. Visa ikiexpire haubugudhiwi na yeyote. Labda uchokoze mamlaka....
Ila ni vyema kugonga VISA ikiisha.


1. DINI
Upande wa dini waislamu ni asilimia 90 na wakristo ni asilimia 10.
Hii kwa kiasi kikubwa ni nchi iliyojaaliwa kuwa na waislam wengi pamoja na kuwa ilitawaliwa na wafaransa.
Tamaduni za waislam hapa ni tofauti sana na kwetu.

●Wana mji wao mtakatifu unaitwa Touba. Huko asilimia kubwa ya huduma ni bure na ni mji unaojitawala. Huko wanapatikana masheikh wakubwa na watu wanaoitwa Marabuuu... Wanamiliki madrasa ambazo watoto kuanzia wadogo wanalelewa huko.

●Uislam ni mtindo wa maisha kwao ni utamaduni wao. Wanauishi uislamu na uislamu unaishi ndani yao.

●Wanaswali sehemu yoyote muda wa kuswali utakapomkutia. Si barabarani, beach, kituo cha daladala au sehemu yoyote. Usishangae kukuta sehemu wanawake wanajiuza halafu kuna mtu katandika mswala wake anaswali bila bugudha.

●Wanawake waislamu hawavai hijab, nkabu wala chochote wao vazi lolote twende. Ikifika muda wa swala atatoa mtandio wake na kanga atajisitiri anaswali.... Same kwa wanaume. Senegal mpaka wahuni wanaswali.

●Asilimia kubwa hamna ubaguzi wa dini.

2. AMANI
Ni nchi yenye amani kwa kiasi kikubwa na utulivu siasa zao za kistaarabu ingawa kwa sasa Rais aliyepo anamtia kashkashi mpinzani wake Osuman Sonko kashapewa kesi za kutosha.... Siku wakiandamana wapinzani ujue shughuli zinafungwa town.

3. UHALIFU
Kuna asilimia ndogo sana ya uhalifu unaweza kusahau simu yako maeneo kama kariakoo au club au gym na ukaikuta pale pale. Sisemi hakuna wizi ila ni asilimia chache sana.
Magari mabovu yamezagaa mitaani lakini hutaona mtu kachomoa side mirror wala chochote...

4. MAKAZI
Mji mkuu Dakar ni mji wa gharama kubwa sana. Bei ya ardhi haikamatiki. Mji umejaa wote na nyumba zinazojengwa ni maghorofa tu. Ukiwa na kiwanja unajenga chote mpaka kwenye mpaka na mwingine anakuja kuunga nyumba yake. Asilimia 95 ya nyumba hazina fense wala parking. Kiwanja kinajaa nyumba.

Kukodi nyumba ni gharama sana kwa Senegal ukifananisha na TZ.

Nyumba nyingi kwenye makazi ya watu wa hali ya kati na uswahilini hawapigi plasta. Ukiangalia ujenzi wao utadhani ni majengo dhaifu ila wao system ya ujenzi wao ni tofauti na bongo.
Dakar imeathiriwa sana na chumvi. Hawatumii bati zinaoza.

Kwa sasa kuna ujenzi unaendelea wa satelite city eneo la djamniado ili ku offload Dakar city centre... Tuseme kama Dar na kibaha hv... Mji mpya unajengwa......

5. VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI
Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani na raia. Hawana shida na yeyote. Ukikosea wanakurekebisha. Usipowagusa hawana habari na yeyote. Unaweza kukaa miezi hata kusimamishwa na traffic usisimamishwe. Unaweza safiri Dar to Mbeya hakuna wa kukusimamisha.

Usishangae kukuta mwanajeshi na raia wote wamevaa gwanda wanapiga story.
Au konda kavaa gwanda za jeshi (si za nchi yao) na hakuna shida.

6. MIUNDOMBINU
Barabara za mjini zimejengeka vilivyo. Kuanzia flyover, bypass n.k ujenzi unafanyika kila sehemu.
Wana barabara za kulipiwa ambazo zinamilikiwa na serikali, kampuni binafsi na wafaransa.....

Alternative way zipo ila foleni sana. Ukifika chagua kupita barabara za kulipia...

Umeme na maji ni nadra kukatika.

Pia Dakar ina udhaifu mkubwa kwenye miundombinu ya mifereji. Ukija kipindi cha mvua utapachukia. Maji yanajaa sana barabarani na kwenye makazi ya watu. Nadhani pia kwa kuwa wapo karibu na bahari....

7. MICHEZO
Wananchi wa Senegal wanapenda kufanya mazoezi sana. Usishangae beach zao kujaa watu wanafanya mazoezi. Barabara zimejaa watu wanafanya mazoezi. Wao ni mazoezi na mazoezi na wao.

Tofauti yao ni kwamba hawaendi viwanjani kuangalia michezo. Pamoja na kuwa na viwanja vingi. Wachezaji wengi wanatoka kwny academies... Hata ligi zao si maarufu kwa wasenegal wengi.

Ndio maana timu ya taifa inafanya vyema kuliko klabu....

8. VYAKULA
Bora umnyime chochote msenegal kuliko mkate. Ukienda mgahawani cha kwanza ni mkate kabla ya kula. Mkate ni deal.

Wana vyakula vingi maarufu kama Chepujam n.k.
Hakuna ugali na wanaushangaa

Kitunguu kwao kipo kwenye kila mlo.
Wanapenda kahawa sana na sukari.

9. STAREHE NA POMBE
Hivi vinapatikana sehemu zinazokaliwa na watu wa nje. Sehemu kama almadies, mji wa St. LUOIS. Sehemu kubwa ya Senegal hawauzi pombe. Klabu zao zinafunguliwa saa 6-9 Jumatatu asubuhi saa 1 unakutana na makundi ya vijana wanatoka klabu.

sigara zake makasha yana picha za kutisha sana .

10. LUGHA
Waliosoma wanajua kifaransa, wananchi wengi wanaongea WOLOF ingawa si wote.
Lugha ya ofisini ni kifaransa...

11. UWEPO WA WATU KUTOKA EAST AFRICA
Jamii ya watu kutoka East Afrika ni wachache sana. Unaweza kukaa miezi 6 ukakutana na mmoja. Watanzania almost hakuna bora Wakenya.

Msanii maarufu wa East Afrika ni Diamond Platnum. Na watu wanamjua Shilole na nyimbo yake ya Chura kuliko hata Ali Kiba.

Wanamkubali sana Magufuli.

Zanzibar ni maarufu sana.

Sheikh Sharif anajulikana sana na ni maarufu mno.

Simba inajulikana kuliko Yanga kwanza Yanga hawaijui kabsa... Big up kwa Simba wanawakilisha.

12. UVAAJI WA HIRIZI, SHANGA VIUNONI WAZIWAZI NI KAWAIDA
Usishangae kukutana na mtu kajitwisha hirizi yake na hana muda na mtu. Hii inanikumbusha yule mchezaji wa Simba Pape N'daw kutoka Senegal alikutwa na hirizi kwenye moja ya mechi. Kwao ni kawaida kama bangili.
Au mwanamke kavaa shanga zake kiunoni na top na wala hamna muda na watu hawashangai.
Pia ni nadra kuona mwanaume anapishana na mwanamke na kumuangalia.

13. KAZI MWISHO IJUMAA
Ni nadra sana kukuta ofisi imefunguliwa jumamosi yani hata kwa ofisi za madalali weekend wanafunga tofauti na kwetu kwenye real state agencies wao weekend ndio biashara inanoga.

14. SHULE
Wanafunzi wa shule nyingi hawavai uniform ni mara chache sana. Shule hufungwa kipindi cha mvua. Yaani kuanzia july mpaka September.

Sijawahi ona watu wanaogopa maji kama wasenegal. Dereva akiona kadimbwi anageuza na hawapiti hapo. Sijui nini kiliwahi wakumba.
N.k n.k n.k

15. USAFIRI WA UMMA NA BINAFSI
Usafiri wa umma kwa Senegal yaani daladala na Tax ni magari yaliyochoka. Unaweza kushuka airport pale ukakuta Tax zimechoka hatari usifikiri utatafuta na kupata mpya hizo ndio zilizopo, atleast siku hizi uber yao (YANGO) wanaingiza gari mpya.

Daladala ndio usiseme.
Wanatumia pia farasi kama usafiri anafungwa tela.
Magari binafsi huwezi kuingiza gari kuu kuu mwisho miaka mitano.
Brand za magari ni EUROPEAN. Toyota ni za kutafuta na pia ni ghali kwa kuwa zinatoka Japan Mbali.

Magari yao ni LHD

AJALI
Senegal hata ukinunua gari leo kesho unaweza kuwa umechubuliwa. Raia hawajali kuhusu magari wao magari kuchubuana ni kawaida na sio kesi. Watu wanaweza gongana magari waaishia kusem INSHALLAH. Hao wanasepa hakuna kesi.

Madereva wa Senegal wanapenda kukimbiza sana magari. Sijui wanawahi wapi speed 120 kwao ni kawaida.

Dakar na ombaomba ni kama chanda na pete.

Nikiendelea kukumbuka nitaendelea kujazia kadri ya uwezo maana ni muda umepita tangu nipite pale.
Wamejitambua na kuwa mfumo wao wa dini na si utumwa wa kutwishwa kila kitu bila kufikiri. Mfano, huu uvaaji wa ninja ni utamaduni wa kiiran wala siyo uislam. Natamani wawe na mji wao wa kuhiji badala ya kupoteza fedha uarabuni kwa wabaguzi
 
Oh Kama specie ya kondoo waliyonayo wao ni tofauti na yetu, bhasi soko lazima liwe dogo. Ila kila kitu kinahitaji research at first place. Huwezi jua labda na Aina hii ya kwetu ikapendwa lakini kwa bei tofauti na hiyo ya specie waliyoizoea mkuu.
Hili neno umelirudia Specie, hapo si kukosea nadhani ulitaka kuandika Specie ni hela ya sarafu ila neno ulilotaka kuandika ni species (ambalo kwa wingi na umoja ni hilo hilo)
 
Sijawahi washuhudia....
Ila nishaona art katikati ya mji imechorwa kwa maneno "fuc* LGB**" inaelekea wamejaribu kujipenyeza ila wamekutana na misimamo mikali. Hata kama wapo ni wanajificha hatari huwezi kuwaona. Sidhani kama wanaweza kuwa na ujasiri wa kujionyesha hadharani. Hawa watu hawatawakwepesha.....
 

Attachments

  • 20230123_171015.jpg
    20230123_171015.jpg
    512.2 KB · Views: 10
Back
Top Bottom