.......uso kwa uso na mwana JF mwenzangu

.......uso kwa uso na mwana JF mwenzangu

Mamboz wana cc.........

mmh ngoja niwaambie yalonikuta maana nimejikuta nakutana Live na member mwenzangu bila kutarajia

mie ni mtu wa JF sana hata ofisini huwa wananiita mama wa JF sasa jana niko ofisin
kuna kaka mmoja tunafanya nae kazi..akawa ananiambia hebu nitajie jina lako la JF
nikamkatalia...kumbe na yeye ni member tena active tu

YEYE;akasema wewe utakuwa King'asti
H.O.E; hapana bana sio mimi ila ID yangu hata sikutajii.....
YEYE; King'asti nae mtata yule.....Ila huwa napenda kusoma comments zake
H.OE nikamwambia kumbe wawafaham watu enhe

Nikajua yameisha akaendelea

YEYE:au wewe ni Heaven on Earth
H.O.E:wala sio mimi...ndio nani huyo kwanza maana mi siwajui watu wengi JF
YEYE:Kadada fulani hivi kana majibu ya mkato hako...ila kanaonekana kako charming
H.O.E nikacheka tu nikasema sio mimi......(Sijui kwanini alikuwa anasema "KA")

akaendelea tu

YEYE: au wewe utakuwa amu
H.O.E nikamwambia bana hapana huyo nae ni nani...wote siwajui na mie sio active kihivo
YEYE:Mhh sio active wewe......Unanidanganya Live LIVE
H.OE:Ndio na wote ulionitajia sio mimi..na ID yangu sikutajii

maongezi yakaisha baadae alikuja kwenye desk langu sa mie nishajisahau akaona ID yangu
kachekaje huyo kumbe wewe ndio H.O.E lol...

na mie sijakubali ka umejua yangu na wewe hadi nijue ID yake kuja kunitajia Lahaula kumbe wakati
tunapishana kona za JF na huku Ofisini tunapishana pia....nimecheka sana alivyonitajia ID yake........
na huku tunatanianaga sana.....ni mtu wa karibu pia ...Nilifurahi sana tu

basi siku hizi ananiita H.OE akinitext ndio anasema Heaven on earth......
Ila nilicheka sana tu

Long Live JF





Ndio unamjua leo,wengine humu tunajuana Prrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr... Source Preta ...
 
Last edited by a moderator:
Binti , Srade yako tamu!
Ina mvuto kiasi flani .
Btw naifananisha na mchuzi wa shatashata as known as rikoriko , kisha a certain mchuzi ukatengwa mezani hauna chumvi !
Mchuzi-pasua mtwe!
Kwa kumtaja huyo Member ndo chumvi yenyewe ujue!
Kwani kajisajili kwa jinale halisi ?
Si ni haya majina yetu mdosho tu? Asa unajigongajegongaje kumchana?
Hapa ni kama umetuchezea maeneo yetu ya misisimko pasi na kutupeak Kibo!
 
Hongera sana maana meno yote 32 nje kwa furaha.
 
Mimi sijawahi kukutana na Mwana JF hata mmoja wachilia mbali anayetumia JF... Nyie mna bahati sana..
 
hii tarehe uliyoweka thread nipo beach jioni mtu ambae sikutaka ajue id yangu humu kaijiua.
Yaaani akaanza kuniuliza jf unatumia jina gani?hapo nshasign out nimeingia as guest kumbe kasimu kangu kamebakia sehemu ya username imendikwa amu na sehemu ya password imeweka **** bado kuligin tu nikaenda back faster ili asiione kumbe too late.Nikamjibu naitwa Kongosho ha ha akaniambia amu acha utani bana khaaa nlichekaje sasa
 
Last edited by a moderator:
Asikwambie mtu bwana,kuonana marafiki wa jf kuna raha yake! Kwanza mtajiona ni watu wa kitofauti hata kama mpo ktk kundi la watu wengi,coz jf ipo kipekee sn.
 
Mimi sijawahi kukutana na Mwana JF hata mmoja wachilia mbali anayetumia JF... Nyie mna bahati sana..

pamoja, utajisikiaje siku ukikutana na mmoja wao ....?
 
Hee jamani kumbe na wewe H.O.E ni binamu yetu eti kabanga huyu ni binamu upande upi kwako?

bestito si umtaje basi huyo jf uliyenaye kazini kwenu?
 
Last edited by a moderator:
Yaani hako kapicha uloweka cha huyo mdada huwa naimagine na wewe upo hivyo hvyo kwa uzuri wa sura yako,napenda sana komet zako.

Koma mara 1 kumsifia Kitchuna wangu!
Tena usirudie! Wanamme tunajipinda kum'carol-lite wewe uje usifie kwa uso mkavu!
Koma .
Heaven on Earth hivi haka kajamaa unakafahamu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom