Kwanza hakikisha hudoji lectures na unamuelewa lecturer vizuri. Na kama vipi usikae back benches ili usikie pindi vizuri.na mahudhurio ni muhimu maana sometimes kuna un announced quizzes zinazoshtukizwa muda wa kipindi so kama umedoji ndiyo unaanza kupoteza marks za course work.
Tenga muda wako wa kujisomea tena ikiwezekana kabla hujasahau topic aliyofundisha lecturer hakikisha unarudia na kuielewa zaidi, nenda Library, tumia Google or materials zozote zilizopo hakikisha umeelewa vizuri.
Nenda Discussion pia ili kujipima katika vitu mnavyodiscuss unavielewa, umevipitia, hakikisha unachangia ili vizidi kustick kichwani.
Pitia pastpapers, hii itakupa confidence kwamba ulichosoma unaweza kujibia mtihani, pia kuna baadhi ya maswali huwa yanarudiwa,nakumbuka nikiwa chuo kabla sijaingia lecture 1 hivi kuna past paper niliipitia ilikua na 20 qns, nikacheki majibu Google niliokua siyajui so nikawa nimeelewa hivi, hamad tumeingia pindi tu ticha kasema put everything aside bakiza pen tu kuna quiz duh kagawa quiz kufungua kitu kile kile nilichotoka kupitia nikatabasamu, nakumbuka i scored 20 out of 20 kwa mara ya kwanza chuo😂. Na kuna paper nyingine ilikuja ngumu hiyo nikapata zero yaani sifuri 0😂.
So seriousness inahitajika chuo katika kila unachofanya maana kina impact kwenye GPA yako utakayoondoka nayo ukimaliza. Hugongewi kengele wala hulazimishwi kwenda prepo or class ila ni muhimu mno kuzingatia ratiba yako.
All the best, kumbuka unategemewa na taifa lako ili uje undeleze kulijenga so kaza buti.💪