Usomi, Mapenzi kwa Chama, Uadilifu na Michango yako haitakupa ubunge, CCM ina wenyewe

Usomi, Mapenzi kwa Chama, Uadilifu na Michango yako haitakupa ubunge, CCM ina wenyewe

kasanga70

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
227
Reaction score
517
Niwashauri vijana wenzangu. Kama hela yako ni ungaungamwana tafadhali sana nenda kaongeze mtaji kwenye biashara yako, kawape maskini au kampe mamaako atakuombea na kukukumbuka daima.
Mimi nimeshiriki uchaguzi ngazi za mkoa, jimbo na wilaya nimwanachama hai wa ccm na sina mpango wa kuhama,maana sioni chama mbadala chenye uwezo au machinery ya kuongoza nchi mbali na ccm but chukka hizi facts zitakusaidia sana mdogo wangu:
1. Ccm ni litaasisi likubwa sana hivo hadi wewe upate ubunge au udiwani wewe ni nani? Kujulikana tu haitoshi.
2.Unaweza kuwa mwadilifu msomi na CV yako imeshiba, kada mzuri lkn haikugarantee kupata chochote ndg yangu ccm ina wenyewe.
3.Mchakato wa uchaguzi utakuhitaji uwe unajua mambo mengi kuzidi umri wako mfano, uchawi, shirki, figisu, ukatili, rushwa na ushawishi kwa wenye nguvu hata sio wajumbe, utawezaaa?
4.Unaweza ukawa ni mchangiaji na mwanachama mzuri sana lkn linapokuja suala la uchaguzi chama kina safu za watu wao wakiwemo watoto wa viongozi, matajiri wakubwa wenye ushawishi, waliokipigania chama hasa kwenye maishu makubwa makubwa sasa wewe mburula tu kajamba nani utaweza ndugu yangu?
5. Mwisho,najua unawaza labda mama ataona fomu yangu hata anipe ukuu wa wilaya.....hahaha ngoja nichekee, uchaguzi ulopita wa ubunge na ndani ya chama kuna majina yaliishia tu kwenye makabati pamoja na sifa tele tulizonazo....na hata yakifika huko kuna swali moja tuu watajiuliza "huyu ni nani kuna mtu anamfahamu"? Imeisha hiyooo hakuna cha ukurugenzi, wala nini hiyo hela unayoenda kuchukulia fomu kasaidie familia yako utanikumbukaa....!
 
Wewe sema hukupitishwa tu, usitufanye sisi wote tuwaogope mapacha wa chama, hata Firauni alikuja na akapita, sembuse hawa wasiokuwa na akili?



 
Back
Top Bottom