Lukwangule
Senior Member
- May 25, 2009
- 157
- 2
MOPAYA MADI
Mtaalamu wa kodi aliyeona
fursa katika ung’arishaji viatu
Na Beda Msimbe
NI nadra sana kukutana na mtu ambaye amehitimu fani nyeti ya Usimamizi wa Kodi na Forodha kufanya shughuli ambayo ni kinyume na taaluma yake, akaifanya kwa nguvu zote na kwa mapenzi yake yote.
Wiki hii katika pitapita zangu nilikutana na Mopaya Madi kwenye hafla moja akiwa mmoja wa watu waliobahatika kupata fedha za tuzo, nikamuuliza kulikoni.
Aliniambia kwamba ingawa ametunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Kodi na Forodha katika Chuo cha Kodi pale Mwenge, Dar es Salaam, yeye amejikita katika kazi anayoipenda, ujasiriamali unaotanuka na sasa ameajiri watu sita, mwenyewe akiwa wa saba.
Mtaalamu huyu wa kodi anasema amekuwa mng’arishaji viatu. Si kwa bahati mbaya bali kwa maamuzi yake mwenyewe, kwani kwake ni fursa nzuri ya biashara kama zilivyo biashara nyingine.
Anasema alipomaliza chuo aliamua kwenda katika taasisi ya Vicoba Sustainable Development Agency iliyopo Kijitonyama na kukopa fedha zilizomsaidia kuanzisha Mop-professional Shoe Shiner, yeye akiwa mtendaji mkuu.
Kampuni hiyo yenye kuajiri watu sita imeanza kuwa na matawi katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam.
“Hii ni fursa ya biashara ambayo ipo wazi sana. Ni fursa kama fursa nyingine na nimeiona, nikasema kwanini nisianzie hapa, na naona ninaenda vyema,” anasema Madi.
Mng’arishaji viatu ni mtu ambaye anatumia akili na maarifa yake katika kufanikisha uzuri wa kung’aa kwa kiatu kwa kusafishwa kitaalamu tabaka kwa tabaka.
Ni kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na watoto wa kiume na kwa wakazi wa miji mbalimbali ni kazi ambayo huleta kipato kikubwa kwa familia mbalimbali.
Pamoja na watu kubeza kazi hii, baadhi ya matajiri wengi au tuseme watu waliofanya vyema katika maisha walifanya kazi ya kusafisha na kung’arisha viatu.
Watu kama akina Mahmoud Ahmed ambaye ni mwimbaji wa Ethiopia, James Brown yule mkali wa muziki wa Soul (The Godfather of Soul) alikuwa anaimba huku akisafisha viatu na kudansi kwenye mtaa wa Georgia wa 9th Street huko Augusta na mwaka 1993 barabara ilipewa jina la "James Brown Boulevard" kwa heshima yake.
Wang’arishaji viatu wengine ni Luiz Inácio Lula da Silva ambaye baadae alikuwa Rais wa Brazil, Alejandro Toledo ambaye alikuja kuwa rais wa Peru na Malcolm X ambaye alifanya kazi ya kung’arisha viatu katika klabu ya usiku ya Lindy Hop mjini New York City.
Madi anasema kwamba alitokea kupenda kazi ya kung’arisha viatu baada ya kuona watu maarufu wakitokea katika eneo hilo tena wakiwa hawana chembe cha shaka katika maisha yao.
Ni kawaida kuwaona wang’arishaji viatu wakiwa katika mitaa wakiendesha shughuli zao na wengi wakionekana waliopigwa maisha, lakini Madi na wenzake wako poa sana na hata kazi yenyewe iko vizuri na yenye unadhifu mkubwa.
Madi anasema kwamba kazi hii ni maarufu sana duniani hasa katika mataifa ya Uingereza, Marekani na India maeneo ya Mumbai.
Kama wewe ni mtanashati, utaona kwamba sio tu kung’arisha viatu kunakupa nafasi ya kuonekana uzuri wako lakini pia kazi hii hutunza ngozi ya kiatu na kuifanya ikae kwa muda mfupi.
Alipomaliza chuo mwaka 2017 alifikiri na kuona hana sababu ya kuendelea kutafuta ajira serikalini, wakati kwa usomi wake anatakiwa kufanya uamuzi unaogusa maisha yake na si kusubiri serikali.
“Hatuhitaji kusubiri serikali, tunahitaji kutambua tulichofunzwa na kutafuta fursa ambayo ipo na kuitumikia. Niliona fursa ya kung’arisha viatu na katika hili nimefanikiwa,” anasema Madi.
Kijana huyu ambaye mwaka jana alipatiwa tuzo kutoka CitiBank ya dola za Marekani 2,000 kwa kuwa mjasiriamali kijana ambaye anatumia huduma za fedha kutoka taasisi ndogo za fedha. Anasema ni lengo lake kusonga mbele katika biashara hiyo na kutanuka zaidi.
“Tupo Kijitonyama mpakani, tuko maeneo mengine kadhaa, lakini ni kazi nzuri inayolipa na pia inayowezesha maisha kuendelea,” anasema Madi.
Madi alizaliwa Songea mwaka 1993 na kusomea shule ya msingi ya Matogoro iliyopo Songea 2007/2010 na kumalizia elimu yake ya sekondari Shule ya Bakili Mluzi iliyopo Mbweni 2012.
Aliingia chuo 2013 na kumaliza mwaka 2016 na mwaka uliofuata akaanza shughuli ya kuzalisha mali kupitia ung’arishaji viatu.
Akitoka kwa baba Madi Idd na mama Devotha Mkuwa, mng’arishaji kijana huyu alitoa ushuhuda wake wa mambo kumnyookea akiwa katika uzinduzi wa tuzo za CITI Bank ambazo zinafanyiwa kazi na kampuni nyingi zinazokopesha fedha kwa wajasiriamali wadogo.
Nilipomhoji anajisikiaje kuhusu kazi yake anasema kwamba kama ‘graduate’ ni lazima ajue namna ya kutatua jambo linalomkabili yeye au jamii inayomzunguka.
Kwa kuona fursa, ilikuwa rahisi kwake Agosti 2017 kuingia katika kazi ya ung’arishaji si kwa kubahatisha bali kwa kutambua na kuona haja ya kusongambele kwa kuwa mjasiriamali.
Anasema kwamba kazi hiyo imempa kibali na heshima miongoni mwa ndugu zangu na wasomi wenzangu, kwani juhudi binafsi zimesababisha mabadiliko makubwa katika shughuli zangu na katika jamii na familia.
Anasema kwa mafanikio hayo aliweza kushiriki katika tuzo ya Citibank na kuibuka mshindi.
"Nilifanikiwa katika mashindano ya Citi bank kwa kuwa niliangaliwa biashara yangu wakaona inavyokua toka nilipokopa katika vikoba wakaangalia faida ambazo wateja wamezipata kutokana na kukua kwa biashara na nimezalisha ajira…shughuli yangu imepanda kutoka kuwa na ajira ya mtu mmoja na kuajiri watu sita na ambao si watu wa familia moja,” anasema.
Anasema katika ushiriki wake kulikuwa na masharti mengi lakini alikidhi masharti hasa ikitambulika kwamba yeye ni kijana.
Wazo la kuwa na tuzo za wajasirimali za Citi (CMA) lilijadiliwa mwaka 2004 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) wakishirikiana na Citi Foundation na Global Student Alliance ambao kwa pamoja waliunganisha nguvu kuonesha ni kwa namna gani asasi za kifedha zinaweza kuimarisha ujasirimali katika jamii maskini duniani na kuhamasisha wajasiriamali wadogo kutumia taasisi hizo.
Tuzo za CMA zilizinduliwa katika nchi nane mwaka 2004 na kutokana na mafanikio yake zilitanuliwa na kuingizwa nchi 30 ilipofika mwaka 2005 ikiwa pia ni kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa ambazo zilitangaza mwaka huo kuwa mwaka wa taasisi ndogo za kifedha.
Huyo ndiye mjasiriamali aliyesoma chuo cha kodi badala ya kuendeleza usimamizi amegeukia biashara ya kung’arisha viatu na inavyoonekana inalipa.
Mwisho