Ustaarabu: Unapoomba kufikia au kukaa kwa rafiki au ndugu hakikisha unakaa kwa muda ule tu mliokubaliana

Ustaarabu: Unapoomba kufikia au kukaa kwa rafiki au ndugu hakikisha unakaa kwa muda ule tu mliokubaliana

kinshwi

Member
Joined
Aug 22, 2016
Posts
22
Reaction score
39
Kati ya very basic etiquette ambayo vijana wa kitanzania tunatakiwa kujifunza ni how not to overstay our welcome.

Unapoomba kufikia au kukaa kwa rafiki au ndugu for whatsoever reason hakikisha unakaa kwa muda ule tu mliokubaliana na kuondoka, siku 3 isigeuke wiki 3 au mwezi na iwapo kuna sababu zinakulazimisha kukaa zaidi ya muda wa makubaliano, toa taarifa in advance na sema tena ni lini unategemea kuondoka, don't just stay and assume they are okay with it and they will understand.

Utu uzima huja na vitu vingi, majumbani kwa watu ni private space, hata kama ni kwa rafiki au ndugu yako wa karibu ni muhimu kutambua kuwa watu hawa kuna namna wanakuwa wameadjust sehemu ya utaratibu wao wa wa maisha ya kila siku(normal routine) ili kuaccomodate uwepo wako kwao.

Kuondoka kwako katika muda mliokubaliana unampa fursa ya kuendelea na utaratibu wa maisha yake as soon as possible na inakupa fursa ya kukaribishwa vyema utakapohitaji msaada huo wakati mwingine. Utamaduni huu wa watanzania wa kusaidiana na kukirimiana ni vizuri utumike vyema.
 
Mtu mmetoka kanisani anapitia tu njia kwako anakusalimu, khe kakaaa🤔......unaanza kujibalaguza kumuandalia chakula mnakula. Haondoki ananogesha stori😁 jua linazama mtu yupo inabidi uanze kuandaa mazingira ya dinner sasa 😂anaanza kujisemesha kumbe ni usiku
 
Akiwa ni rafiki wa kike mbona ni shigida shega
 
Ni kweli haswa mkiwa na utaratibu wa kubadili hadi aina za vyakula na vyombo mnavyotumia kula ili kumfurahisha mgeni. Kitu ambacho ni common kwa watanzania wengi

Kiufupi, ukitoa kwa wazazi kuna sehemu moja tu ninayoweza overstay kwa hiyo nikiwa na options zingine. Ni kheri nizitumie hizo kuliko kukaa kwa ndugu
 
Mtu mmetoka kanisani anapitia tu njia kwako anakusalimu, khe kakaaa🤔......unaanza kujibalaguza kumuandalia chakula mnakula. Haondoki ananogesha stori😁 jua linazama mtu yupo inabidi uanze kuandaa mazingira ya dinner sasa 😂anaanza kujisemesha kumbe ni usiku

Kwangu inategemeana na uhusiano nilio nao huyo mtu lakini pia kama nina ratiba zingine ambazo siwezi kuziendeleza. Vingine fresh tu maana malezi niliyokulia, chakula ni kitu cha mwisho kukifikiria kwa mgeni yoyote yule japo nilipoingia dar nikakutana na obsession flani ya watu katika chakula kutokana na ugumu wa maisha
 
Wewe umeona chakula tu??
Muda
Ratiba
Watu wana mambo yao ugeni uendaane na taarifa na ratiba
Unatakiwa ufue una mgeni utamuacha mpweke ukafue?
 
Wewe umeona chakula tu??
Muda
Ratiba
Watu wana mambo yao ugeni uendaane na taarifa na ratiba
Unatakiwa ufue una mgeni utamuacha mpweke ukafue?
Mbona ulivyovisema ndivyo nilivyovisema kuhusu mahusiano na ratiba binafsi. Huko mwishoni kuhusu chakula niliongelea generally 🙏🏽🙏🏽
 
Kuna miaka nilipanga gheto mahali, sasa Ile nyumba kuna mpangaji mwenzangu alileta kijana wake kutoka kwao(nafikiri alikuja kumtafutia kazi)

Jamaa akaniomba yule kijana awe analala room kwangu kwa muda wa wiki moja wakati yeye akimtafutia sehem ya kulala.

Jamaa yeye alikua na familia hivyo asingeweza kulala nae, me nilikua single.

Aisee ilipita miezi na sikuona dalili zozote za yule kijana kuhama gheto kwangu. Ilinipa usumbufu mkubwa sana kwa sababu nilikua siwezi tena kulala ghetto na demu wangu.

Mwisho wa siku niliamua tu kuhama
 
Tuseme ni ulaku, uchoyo au maisha ni magumu, why ujisikiea vibaya uwepo wangu kwako wakati sijaja kuhamia? Ndio maana sie wengine hatuna time na ndugu, jamaa na marafiki zetu tunafikia gesti hata kama tunao watu wa kufikia katika mji huo. Ya nini kukera watu kwenye maisha yao. Shwaini mkiugua hamtatuona, tutakuja mwishoni msibani mkifa. Bakini na maisha yenu
 
Pumbavu sana ! Watu wa siku hizi wamekuwa wachoyo na wabinafsi, wanajenga jumba kubwa lina kila kitu ndani halafu wanaishi yeye, mke wake, watoto wachache na kijakazi wao kisha hawataki ndugu kwendakwenda kuwatembelea wanajisikia vibaya wakati uwezo wa kula milo ya gharama yoyote wanayo. Isiwe taabu wabaki na mahekalu yao hatutaenda kuwatembelea na wakipata shida watafute watu wa kuwasaidia wasitusumbue sie ndugu zao. Wakiugua hatutaenda kuwajulia hali mpaka wafe ndio tutaenda msibani tukitaka. Waendelee kula bata zao watuache na maisha yetu hatutaki shobo tumechoka kuringiwa na kufedheheshwa
 
Mtu mmetoka kanisani anapitia tu njia kwako anakusalimu, khe kakaaa[emoji848]......unaanza kujibalaguza kumuandalia chakula mnakula. Haondoki ananogesha stori[emoji16] jua linazama mtu yupo inabidi uanze kuandaa mazingira ya dinner sasa [emoji23]anaanza kujisemesha kumbe ni usiku
Niliwahi kufanya hii, niliona uso wa mwenyeji umebadilika baada ya muda wa dinner kufika nikiwa pale. Bahati mbaya sana nilienda nikiwa najua ratiba ni ya kulala kutokana na umbali. Lakini sijawahi kurudia kabisa hii kitu
 
Kuna miaka nilipanga gheto mahali, sasa Ile nyumba kuna mpangaji mwenzangu alileta kijana wake kutoka kwao(nafikiri alikuja kumtafutia kazi)

Jamaa akaniomba yule kijana awe analala room kwangu kwa muda wa wiki moja wakati yeye akimtafutia sehem ya kulala.

Jamaa yeye alikua na familia hivyo asingeweza kulala nae, me nilikua single.

Aisee ilipita miezi na sikuona dalili zozote za yule kijana kuhama gheto kwangu. Ilinipa usumbufu mkubwa sana kwa sababu nilikua siwezi tena kulala ghetto na demu wangu.

Mwisho wa siku niliamua tu kuhama
huyo jamaa naye ni bwege, anaona hana chumba halafu anampeleka ndugu yake akabane watu bila aibu
 
Dunia imebadilika sna aiseee siku hizi mambo yamebadilika sana
 
Back
Top Bottom