Ustaarabu: Unapoomba kufikia au kukaa kwa rafiki au ndugu hakikisha unakaa kwa muda ule tu mliokubaliana

Ustaarabu: Unapoomba kufikia au kukaa kwa rafiki au ndugu hakikisha unakaa kwa muda ule tu mliokubaliana

Kati ya very basic etiquette ambayo vijana wa kitanzania tunatakiwa kujifunza ni how not to overstay our welcome.

Unapoomba kufikia au kukaa kwa rafiki au ndugu for whatsoever reason hakikisha unakaa kwa muda ule tu mliokubaliana na kuondoka, siku 3 isigeuke wiki 3 au mwezi na iwapo kuna sababu zinakulazimisha kukaa zaidi ya muda wa makubaliano, toa taarifa in advance na sema tena ni lini unategemea kuondoka, don't just stay and assume they are okay with it and they will understand.

Utu uzima huja na vitu vingi, majumbani kwa watu ni private space, hata kama ni kwa rafiki au ndugu yako wa karibu ni muhimu kutambua kuwa watu hawa kuna namna wanakuwa wameadjust sehemu ya utaratibu wao wa wa maisha ya kila siku(normal routine) ili kuaccomodate uwepo wako kwao.

Kuondoka kwako katika muda mliokubaliana unampa fursa ya kuendelea na utaratibu wa maisha yake as soon as possible na inakupa fursa ya kukaribishwa vyema utakapohitaji msaada huo wakati mwingine. Utamaduni huu wa watanzania wa kusaidiana na kukirimiana ni vizuri utumike vyema.
We si umfukuze tu,
Unatufokea sisi kwani tumefikia kwako?
Tafadhali bana.
 
Binafsi kwangu wageni hawaishi Na hawapungui..napenda wageni japo wanachangamoto zao (haswa upande wa mume)wavivu ..wenye majungu na wanafiki wote najua kuishi nao kilingana na tabia zao..ilibidi kuongeza nyumba ya nje ili kuepusha kuvuruga utaratibu wa. Watoto kulala na wageni ili waale kwa raha zao..hatujawahi kupungukiwa japo twawezq kaa na wageni mpaka 3,4 ,na wengine wakisomeshwa..Wengine wakijitafuta kimaisha..ndugu zangu once ukipata nafasi ya kusaidia ndugu saidia kama uwezo unaruhusu..huwezi jua baraka zako na kesho yako itakuwa wapi ..uchoyo na roho mbaya havisaidii
 
Yani kwa mjomba kwa kaka yake mama nikae siku tatu hapana mwezi unatosha ndio niondoke
 
huyo jamaa naye ni bwege, anaona hana chumba halafu anampeleka ndugu yake akabane watu bila aibu
Jamaa alinikera sana, halafu huyo ndugu yake mwenyewe mchafu anajua kulala tu lkn hata siku moja hakujaribu hata kufagia chumba
 
Kuna miaka nilipanga gheto mahali, sasa Ile nyumba kuna mpangaji mwenzangu alileta kijana wake kutoka kwao(nafikiri alikuja kumtafutia kazi)

Jamaa akaniomba yule kijana awe analala room kwangu kwa muda wa wiki moja wakati yeye akimtafutia sehem ya kulala.

Jamaa yeye alikua na familia hivyo asingeweza kulala nae, me nilikua single.

Aisee ilipita miezi na sikuona dalili zozote za yule kijana kuhama gheto kwangu. Ilinipa usumbufu mkubwa sana kwa sababu nilikua siwezi tena kulala ghetto na demu wangu.

Mwisho wa siku niliamua tu kuhama
Aaah mi ningemchana mwenyeji wake amtafutie mahali pengine pa kupumzisha mbavu zake
 
Inategemea na uwezo wa kiuchumi na nafasi uliyonayo kwenye nyumba.
Ni utamaduni wa kiafrika kusaidia extended family,marafiki kwenye mahitaji mbalimbali.
Tabia za umimi na ubinafsi tunaiga tu kutoka kwenye mataifa ya Magharibi na kujifanya wazungu.
Katika jamii karibia zote za kiafrika kumkaribisha mtu chakula na mahali pa kulala sio jambo la kujadili.Ni part and parcel ya utamaduni wetu.Kama kweli kuna changamoto za kiuchumi tutumie lugha za kufariji kwa wanaohitaji kusaidiwa kwenye nyakati mbali mbali za maisha.
 
binafsi huwa wananiudhi wale wanaoenda nyumban kwa mtu bila taarifa
katokea mtaa wa pili huko anakuja hodi nimekuja kuku salimia
huwa najiuliza wanamaana gani kwenda kwa mtu bila kutoa taarifa tena usiku saa 2na mawasiliano ya muhusika anayo
utawasikia wanaambizana huko ukienda kwa mtu usitoe taarifa ili ukute uhalisia wa maisha
yake sijui ndio kuchunguzana huku
usiombe wafanyakazi wenzio wajue unapoishi utapata tabu sana
wanawake tuna shida
 
Kuna miaka nilipanga gheto mahali, sasa Ile nyumba kuna mpangaji mwenzangu alileta kijana wake kutoka kwao(nafikiri alikuja kumtafutia kazi)

Jamaa akaniomba yule kijana awe analala room kwangu kwa muda wa wiki moja wakati yeye akimtafutia sehem ya kulala.

Jamaa yeye alikua na familia hivyo asingeweza kulala nae, me nilikua single.

Aisee ilipita miezi na sikuona dalili zozote za yule kijana kuhama gheto kwangu. Ilinipa usumbufu mkubwa sana kwa sababu nilikua siwezi tena kulala ghetto na demu wangu.

Mwisho wa siku niliamua tu kuhama
Mimi nashukuru Mungu, sinaga aibu nakuchana ukweli , bhana nakupa sku mbili sepa
 
Jamaa alinikera sana, halafu huyo ndugu yake mwenyewe mchafu anajua kulala tu lkn hata siku moja hakujaribu hata kufagia chumba
Kyna wageni ni changamoto we Acha tu ,mgeni anafika unamkabidhi chumba self analala peke yake wa kiume..akiamka hatandiki hasafishi chumba hasafishi ndoo ya bafuni mchafu balaa..unamkabidhi mashuka blanketi neti safi kabisa siku anaondoka anakurupuka kama kafukuzwa chumba hakitamaniki..si mashuka neti wala blanketi hawezi jifunika mwingne akifika..najiuliza hawa watu hawakufunzwa kwao ama?suala la usafi binafsi mpaka mtu asomee pia?au ndo mfumo dume?mtu anakula peke yake sahani utaikuta asbh hapo hapo mezani asbh aloo kuna mambo yanakera basi tu utafanyaje...niliwahi kuwakomoa wageninwenyeji wanaokuja likizo kwa mfumo huu sikufua blanketi wala shuka siku mmoja wao anafika nkampa chafu vile vile alipiga chafya usiku mzima asbh aliamka akafua na siku anaondoka alifua akaacha kila kitu safi kuuanzia nilikomesha staki ujiga katika suala la usafi kama kwenu hukufunzwa ulimwengu ndo mm lazima nikufunze na ufate utaratibu wa nyumban kwangu kama ninavyotaka
 
Wageni ni baraka ila wasiwe wachawi na wenye tabia za hovyo..!!
Once unapokuwqbna space jua utapokea kila aina ya wageni mpaka wa hovyo utawapata ni kujua tabia zao na namna ya kumhandle kila mmoja kulingana na Hulka yake ..mwingine hatambui ulimwengu wa sasa si wa watot kulala na wageni akiona mtoto analala peke yake na who wanalala 2 atapercieve neg ..utaitwa mchoyo na majina mengine mabaya..
 
Back
Top Bottom