Ustahimilivu wa Digitali Unawawezesha Watoto Kunufaika na Matumizi ya Mtandao

Ustahimilivu wa Digitali Unawawezesha Watoto Kunufaika na Matumizi ya Mtandao

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Ustahimilivu Mtandaoni Watoto.jpg

Ustahimilivu wa digitali kwa watoto ni ujuzi ambao watoto wanahitaji ili kudhibiti na kustahimili changamoto za ulimwengu wa mtandaoni kwa usalama. Ni uwezo wa kutofautisha mema na mabaya katika maisha ya kidigitali, kufikiri kwa umakini, kufanya maamuzi mazuri, na kufahamu hatari na matokeo ya matendo yao.

Kuwajengea watoto ustahimilivu wa kidigitali ni njia bora ya kuhakikisha watoto wako salama mtandaoni na wanaweza kufaidika kutokana na fursa ambazo mtandao hutoa.

Ustahimilivu hutengenezwa kupitia vipengele kama vile: kuelewa anapokuwa hatarini, kujua nini cha kufanya ili kutatua changamoto, kujifunza kutokana na uzoefu, na kuwa na usaidizi (support) ufaao ili kukabiliana na changamoto.

Watoto walio na ustahimilivu wa digitali wana uwezekano mdogo wa kufanya au kurudia makosa, lakini pia uwezekano ni mdogo kwa wao kuathirika kiafya ya akili kwa muda mrefu.

Hivyo basi, ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwajengea watoto wao ustahimilivu kwa kuzingatia yafuatayo.

1. Kumfundisha mtoto kujiwekea mipaka
Mtoto wako anapoanza kufurahia kutumia kifaa chake kuperuzi, ni muhimu kumfundisha kuweka mipaka ili kudhibiti muda anaotumia mtandaoni. Hii inamfundisha kuwa mtumiaji mwenye udhibiti wa matumizi yake wenyewe, na kufahamu ukweli kwamba kuna ulimwengu nje ya skrini.

2. Mpe mtoto ujuzi wa kufanya maamuzi sahihi
Ni muhimu mtoto afundishwe na kukuzwa uelewa wa masuala kama vile kudhibiti mipangilio ya faragha kwenye kifaa chake, kuelewa tofauti kati ya marafiki na wageni (strangers) mtandaoni, jukumu lake kama raia wa kidigitali na kwamba kile anachofanya mtandaoni kinaweza kuwepo milele, na kwamba ustahimilivu wa digitali unahusu zaidi uwezo wa kudhibiti tabia zake.

3. Jenga tabia ya mawasiliano nyumbani
Mzazi akianzisha mazoea ya kujadili shughuli za mtandaoni za mtoto tangu umri mdogo itakuwa rahisi kuhimiza mazungumzo haya yanapokuwa magumu zaidi baadaye. Ni vema watoto wakatambua kwamba wanaweza kwenda kwa mzazi bila hofu ikiwa wanahitaji usaidizi.

4. Himiza uhuru kwa kijana wako
Kukuza kujitambua (self-awareness) kwa mtoto wako ni muhimu sana. Ni vema akajifunza kujadili masuala yoyote anayokabiliana nayo kwa uhuru kabisa na, ikihitajika, kutafuta usaidizi kutoka kwa mzazi, rafiki, au mtu yeyote anayeaminika.

5. Tumia zana za udhibiti wa maudhui
Kama mzazi uko katika nafasi nzuri ya kuelewa ukuaji wa kihisia na kijamii wa mtoto wako. Kwa kutumia zana ya udhibiti wa maudhui (Parental Control tools), unaweza kuratibu matumizi yao ya mtandaoni ili kumruhusu mtoto wako kufikia intaneti kwa kiwango ambacho kinalingana na kiwango chake cha ustahimilivu wa digitali. Hata hivyo, zana hizo zinapaswa kuwa kama safu ya kwanza ya ulinzi tu, lakini wazazi bado wanapaswa kuzungumza kuhusu changamoto za watoto wao.

Watoto ni wastahimilivu kiasili. Wanaweza kujifunza kusonga mbele baada ya matukio yasiyowapendeza lakini wanahitaji usaidizi na mwongozo ili kuvuka nyakati hizi za majaribu. Ulimwengu wa mtandaoni kuna wakati unaweza kuwa ni shimo la vitisho, uonevu, na sehemu hatari kwa usalama wa mtoto.
 
Back
Top Bottom