SoC02 Ustawi wa afya zetu unategemea mazingira safi na salama

SoC02 Ustawi wa afya zetu unategemea mazingira safi na salama

Stories of Change - 2022 Competition

Blue Marble

Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
25
Reaction score
16
Nawasalimu wote kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania!

Awali ya yote nipende kumshukuru mwenyezi Mungu kwa afya njema anbayo imenipa fursa hii ya kuandika haya kwa manufaa ya ustawi wa nchi yetu Tanzania na dunia kwa ujumla.

Bila kupoteza wakati, suala la afya bora na mazingira safi ni mtambuka katika ustawi wa mwanadamu yeyote yule katika dunia hii. Ripoti ya benki ya dunia ya mwaka 2018 inasema uchafuzi wa mazingira umeongezeka kwa miongo michache iliyopita hasa kwenye nchi masikini na Tanzania ikiwemo. Mfano, mwaka 2015, inakadiliwa vifo milioni 9 vya watoto wachanga duniani kote ambavyo ni sawa na asilimia 16 ya vifo duniani vilisabishwa na uchafuzi wa mazingira ambavyo ni zaidi ya vifo vilivyosababishwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, magonjwa ya upumuaji na malaria kwa ujumla wake na asilimia 90 ya vifo hivi vinavyosabishwa na uchafuzi wa mazingira vinatokea kwenye nchi masikini na Tanzania ikiwemo na waathirika wakubwa ni jamii ya watu wenye maisha duni na wanaoishi kando kando ya mito, mabondeni na kwenye makazi holela hasa kwenye majiji na Dar es salaam ikiwa kama mfano dhahili. Suala la uchafuzi wa mazingira lina athari kubwa kwenye ustawi wa afya zetu lakini bado limepewa kisogo kwenye sera na katika baadhi ya ngazi kubwa za maamuzi.

HL56--9r-zhUM1eLwX8UlZw_0GTv73b0GFGKgwhm1uHQGn9oWfY0IwKU1XplmToIwuInqavmZJS3AspEDqvuC8VudZEev0nkc7Usn7KmO0slasG0kt9KCwG0BSklKVREnqeprOvpy51lw4wJ27qSHg

Katika grafu hii inaonyesha uchafuzi wa mazingira ndio chanzo kikubwa cha vifo duniani.Takwimu hizi zilitolewa na shirika la afya duniani (WHO)mwaka Pi7.

Mfano, tukiangazia suala la uzalishaji wa taka ngumu nchini Tanzania ni mkubwa sana mfano mwaka 2012 ilizalisha taka ngumu kiasi cha tani 2425 kwa siku na tafiti nyingine zinaonesha kiwango hiki kinaongezeka kila siku, kwa tafiti zilizotolewa na baraza la takwimu nchini (NBS) mwaka 2017, zinaonyesha kuwa Tanzania inazalisha taka kiasi cha tani 4700 kwa siku na kwa kadri nchi yetu inavyokua kiuchumi na uzalishaji wa taka unaongezeka na inakadiriwa kufika 2025 tutakuwa tunazalisha tani 12000 tani za taka kwa siku ni mara tano ya kiwango kilicho kadiliwa mwaka 2012. Kwa kuakisi hali hii tutakuwa na mtihani mkubwa sana kukabiliana ongezeko hili kubwa la taka kwakuwa mpaka sasa bado hatujapata muarobaini wa kiasi hiki ambacho ni kidogo ukilinganisha na kiasi kilichokadiriwa tukifika mwaka 2025.

Achilia mbali madhara ya taka hizi ngumu kwenye mazingira ya bahari, mito ,misitu na kwa wanyama. Pia zimeongeza mzigo mkubwa kwa nchi kiuchumi katika kuondoa taka hizi na madhara yake yamekuwa makubwa kiasi cha kupelekea mpaka mwaka 2013 Makadirio ya gharama za kiuchumi yanayotokana na vifo vya watoto wachanga Tanzania vinavyosababishwa na uchafuzi wa mazingira yalikuwa zaidi ya dola za kimarekani 28,700 milioni (Roy, 2016). Athari za kuishi katika mazingia machafu sio tu kwenye afya zetu bali athari hizi pia ni mwiba moja kwa moja kwenye uchumi wetu kwa kuwa gharama nyingi zinawekezwa katika kukabiliana na magonjwa haya badala ya kwenda kuwekezwa kwenye miradi mingine ya kimaendeleo.

Pia, mwaka 2013, gharama zinazohusiana na afya, matumizi ya maji yasiyo salama na hali mbaya ya kimazingira katika nchi yetu ya Tanzania (poor hygiene and sanitation) inakadiliwa kuwa ni dola za Marekani bilioni 10 (Roy, 2016). Inakadiliwa kuwa magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa maji na chakula mfano homa za matumbo, kipindupindu na malaria yana athiri mamia ya wakazi wa mijini na vijijini nchini kutokana na mifereji kuziba na taka, matumizi ya vyoo vya shimo na madimbwi ya maji machafu ambayo ndio chanzo cha mbu kuzaliana na kueneza malaria, magonjwa ya ngozi na homa ya dengi na kuisabishia serikali kutumia gharama kubwa kukabiliana na mahonjwa haya kama takwimu zilivyoonyeshwa hapo juu. Waathirika wakubwa wa hali hii ni watu wanaoishi kwenye makazi duni ambao mafuriko wakati wa mvua ni sehemu ya maisha yao, hapa ndipo maji yanayotirishwa kutoka kwenye vyoo na madampo ya taka kwenda kwenye mifereji, mito, kwenye makazi mabondeni na baharini, hii inatokana na ubovu au kutokuwepo kabisa kwa miundombinu ya maji taka na mifereji inayo ruhusu maji haya kupita na kusabisha kutuama hivyo kupelekea kusababisha maafa ya magonjwa na mafuriko kwa wakazi wengi hasa wanaoishi mijini. Hali hii imekuwa hatari kwa afya ya wakazi wa maeneo haya na maeneo haya ndiyo yenye hatari kubwa na dhaifu katika kupelekea mlipuko wa magonjwa mbali mbali mfano Kipindu pindu, homa a matumbo (typhoid), malaria, saratani na magonjwa ya ngozi.

Pia hali hii imepelekea kuongezeka kwa watu wenye magonjwa tajwa hapo juu na hii inapelekea uhaba wa miundombinu ya afya kutokana kuongezeka kwa wagonjwa ambao chanzo kikubwa cha magojwa yao ni uchafuzi wa mazingira. Mwaka 2007, asilimia 60 mpaka 80 ya wagonjwa walioenda hospitalini Tanzania magonjwa yao yalitokana na matumizi ya maji yasiyo salama na uchafuzi wa mazingira kwa ujumla ( Taarifa hizi ni kutoka baraza la takwimu la taifa (NBS 2015)...
View attachment Waste situation_2.jpg
Swali kubwa kwa wadau wa mazingira, serikali,sekta binafsi, mashirika na jamii kwa ujumla, je tunawezaje kuondokana na hali hii? Je, ni jitihada gani za haraka zichukuliwe kuondoa adha hii ambayo imekuwa mwiba kwa ustawi wa afya ya jamii na mazingira yetu kwa ujumla. Binafsi napenda kutoa mapendekezo na ushauri wa nini kifanyike ktokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi na jamii katika uhifadhi wa mazingira ili tuweze kupata tafakari juu ya kuondokana na uchafuzi wa mazingira kwenye jamii zetu.

Jambo la kwanza ni kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, athari za uchafuzi wa mazingira kiafya, kimazingira, kijamii na kiuchumi na elimu hii itolewe kwa ushirikishwaji mkubwa wa jamii hasa wale waathiria wakubwa wa uharibifu wa mazingira na elimu inayotolewa iakisi uhalisia wa mazingira yao, hii ni chachu kubwa katika kuongeza ushiriki na uwajibikaji wa jamii katika utunzaji wa mazingira yao.

Uhamasishaji wa mazoezi kufanya usafi kwenye fukwe, mito, sehemu za wazi, mabondeni na kwenye mifereji. Zoezi la usafi wa kijamii kwenye maeneo tajwa ni muhimu kwa kuwa ndio njia pekee ya kuondoa taka zilizojaa kwenye maeneo haya, huku jitihada za kutoa elimu zikiendelea ili kupunguza kasi kama sio kuzuia kabisa kuendelea kutupwa taka kwenye maeneo yetu. Kufanya usafi wa kijamii ni ishara ya uwajibikaji na uraia mwema katika kutoa mchango katika maendeleo ya ustawi wa jamii zetu. Pia usafi wa kijamii ni hamasa na sehemu ya kukusanya takwimu na taarifa za hali ya uchafuzi ili kutafuta utatuzi wa kudumu wa uchafuzi wa mazingira kwa kuwatambua wachafuzi wakubwa na kutafuta namna bora ya kuwashirikisha katika kuondoa changamoto hii, pia taarifa hizi ni muhimu kwa serikali katika kufanya maamuzi kwenye namna bora ya kuhakikisha tatizo la uchafuzi wa mazingira linakwisha kabisa.

Uwepo wa miundombinu imara katika kudhibiti suala la uchafuzi wa mazingira kama uwepo wa huduma bora ya uzoaji wa taka, kuweka mazingira wezeshi ya uchambuzi wa taka kuanzia kwenye kaya, ili kurahisisha zoezi la urejelezaji wa taka, uwepo wa madampo ya kisasa ya kutupa taka, viwanda vya urejelezaji wa taka ili kuhakikisha taka zote rejelezi haziendi dampo na viwanda vya utengezaji wa mboji inayotokana na takaozo za mabaki ya vyakula na mazao.Hii itapunguza kiasi kikubwa cha taka zinazoenda dampo, ambazo zinamchango mkubwa katika uzalishaji wa hewa ya ukaa (METHANE) ambayo inachangia uharibifu wa utando wa ozone na kusababisha kuongezeka kwa joto duniani na kuleta mabadiliko ya tabia nchi ( climate change).
View attachment Waste situation in Dar es salaam.jpg
Ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika kutatua changamoto ya uchafuzi wa mazingira, suala la uchafuzi wa mazingira na athari zake zipo katika kila sekta kuanzia kwenye mazingira, uchumi, miundombinu, elimu, afya, teknolojia nk. Hivyo kutafuta suluhu yake pia lazima sekta zote zihusike kikamilifu, pindi sekta moja inaposhindwa kushiriki hatuwezi kutatua changamoto hii, hivyo wito wangu kwa serikali yenye mamlaka ya kufanya hili la kuunganisha sekta hizi, iweze kuendelea kuboresha mazingira katika ushirikishwaji mkubwa wa sekta zote linapokuja suala la maamuzi yanayohusu mustakabali wa utunzaji wa mazingira ili tuweze kupata matokeo chanya.

Mwisho nitoe wito kwa wadau wa mazingira, serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali kuona suala la madhara ya uchafuzi wa mazingira ndio chanzo kikubwa cha mlipuko wa magonjwa mengi kwenye jamii zetu na lazima tuone kuna uhusiano mkubwa sana baina ya afya bora na usafi wa mazingira yetu, kama ikitokea vinginevyo ndio maana tunaona watu wetu wanapata adhabu ya magonjwa, mafuriko na uharibifu mkubwa wa mali zao. Hivyo kwa uongozi wetu tuwasaidie watu wetu kwa kuwapa taarifa za kutosha na sahihi juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kama ndio kichocheo kikubwa katika kujenga jamii yenye afya safi na salama na hilo ndilo liwe neno katika kuziba mwanya wa ufinyu wa taarifa na takwimu uliopo kwenye vyanzo na kiwango cha athari za uchafuzi wa mazingira katika nchi yetu ya Tanzania.
View attachment Waste 2022.jpg
Mandhari ya mazingira yetu ya fukwe yangependeza kwa muonekano huu na si vinginevyo!

Ombi langu kwa wana jamvi hapa, naomba kura zenu katika andiko hili, natanguliza shukrani kwenu watu wanguvu 🙏🙏🙏


Alamsiki!
 

Attachments

Upvote 2
Back
Top Bottom