Kati ya taasisi hizo mbili hapo juu,nani ana mamlaka ya kuamuru mdai na mdaiwa wakapime DNA?
Kuna mwanamke ana claim mimi ni baba wa mtoto wake na ameshapeleka shauri Ustawi wa Jamii,na wamenipa muda wa kujifikiria,
Nataka tukapime DNA ila ofisa wa Ustawi amekula mlungula ili atu force tukapime BLOOD GROUPS,
Naomba msaada
Huwa nawaza na kukosa jibu ni kwanini watu tuliopo duniani tupo jinsi tulivyo! Kweli huwa sipati jibu
Najaribu kutafakari na kujiuliza ni nini kinatokokea mpenzi uliyekuwa unampigia simu kwa bashasha na maneno matamu kama asali ya nyuki wadogo (wale wasiouma) leo hii mnaishia kulumbana na kutokuelewana?
Mpenzi uliekuwa unamvua nguo hata wakati mwingine bila ridhaa yake anakubali ili tu amridhishe mpenzi wake!! Kweli dunia haina huruma!! Leo hii ni mpaka Mahakamani na DNA Test?
Nikiwa kama kaka yako na ninaekutakia maisha mema huko mbeleni, kama utapenda naomba nikushauri!
Maisha sio yale tunayo yaona kwa macho au kuyagusa kwa mikono yetu, yale tuyaonayo ni asilimia ndogo sana hata 10% ya maisha halisi haifiki.
Najua kabisa utakuwa unaye mpenzi mwingine! ambaye kwa sasa amechukua nafasi kubwa katika mawazo yako! na ndio maana huyo wa zamani "Unaemuita mwanamke" unaona si lolote, lakini naomba utambue kuwa yeye ni kiumbe hai na anayo nafsi kama wewe na kuwaza na kuumia, kama wewe unavyoumia alivyokwambia ana mtoto wako!!
Najaribu kujiuliza ni mara ngapi umemvua nguo? ni mara ngapi amefanya mema sana kwako? Tafakari
Omba hekima ya mwenyezi Mungu ikutawale, na kaa na huyo mwanamke uongee nae kwa urafiki kabisa huwezi kuamini atakwambia ukweli wote kama mtoto ni wako au la,(Wanawake ni warahisi sana kujieleza ukijua wapi pa kushika) Naomba ukipenda unijibu (Je ulikuwa na mpando wa kumuoa? kama ni hapana je yeye alikuwa anajua hilo kabla hajaingia kwenye mahusiano na wewe? ningependa unijibu hapa JF kwa manufaa ya wote au unipm kama hutataka nikujibu hapa upenuni!
Naamini kabisa DNA hata ikisema huyo mtoto ni wako kwa sababu dhamira yako ni kuyakwepa majukumu hutakubaliana na matokeo yake. utaishia kusema mashine yenyewe feki!
bado natafakari kwa nini dunia haina huruma!!