Usuli

Usuli

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
Tumekuwa tukitumia neno la kiingereza 'feedback' pengine kwa kutofahamu neno halisi la kiswahili. Wengine wanasema ni 'mlisho nyuma'.
Jumatano nimemsikia mtaalam wa lugha ya kiswahili akieleza ufasaha wake.
Neno 'feedback' kwa kiswahili ni Usuli.

Kwahiyo unaweza sema ' Ogah, nipe usuli wa kikao cha jana'.
 
Hivi nani huwa anatunga haya maneno, nijuavyo mimi lugha huwa haitungwi inatokea naturally, basi mwenzenu nilpoona neno usuli kwenye headline nikategemea kukutana na picha ya ajabu, neno hili linashabihiana sana na msuli, sasa linakuwa kama kisifa fulani hivi. e.g JAMAA NA USULI HUYO!!!
 
Nafahamu kuwa yapo maneno fulani yanaazimwa kutoka katika makabila au lugha kutokana na matumizi yake.
Kwa mfano 'kuteta' ni neno la kipare likiwa na maana kusema. Kujikanganya, linatokana na kujichanganya lakini katika lafudhi ya kisukuma, ukienda kwetu bonde utasikia 'waona vihi', au mbwanga. Mbwanga limetumika kama kijana, na limeingia kwasbabu matumizi yake ni makubwa hasa kanda ya kaskazini Wapare, wasambaa, wabondei na wazigua.
 
Tumekuwa tukitumia neno la kiingereza 'feedback' pengine kwa kutofahamu neno halisi la kiswahili. Wengine wanasema ni 'mlisho nyuma'.
Jumatano nimemsikia mtaalam wa lugha ya kiswahili akieleza ufasaha wake.
Neno 'feedback' kwa kiswahili ni Usuli.

Kwahiyo unaweza sema ' Ogah, nipe usuli wa kikao cha jana'.

Maneno mengi ya kiswahili yanachakachuliwa na watu wanaojaribu kukitoa kiswahili kwenye asili yake na kukipeleka kusikokuwa na ladha ya matamshi ya kiswahili, tazama kama hili "mlisho nyuma" halina kabisa ladha kama "usuli".

Jokofu? halina ladha, kwa nini isiwe thalaja neno linalo-tokana na theluji ambayo ni (snow) kiswahili fasaha na thalaja ni kitengeneza theluji.
 
Du! mi nkajua feedback ni mrejesho. Sasa mrejesho ni nini!
 
Back
Top Bottom