Pamoja na kukubali kuna uzembe wa kiuongozi pale TRA, THA na ofisi zingine nyingi tu, ila
Sababu nyingine ni wafanyakazi tena wadogo tu, hawataki kufanya kazi zao mpaka akuzungushe ushinde hapo.
Wengine hawafanyi kazi wako kwenye internet.
Tuweni wa kweli, naamini wengi humu JF tunaacha kazi na kuanza kujibu hoja za humu JF wakati wa kazi.
Mods wakitoa takwimu traffic kubwa JF ni wakati wa kazi, weekend watu ni wachache, hii inaonyesha kuwa na sisi wafanyakazi wa chini inabidi tuache mizaa tufanye kazi, tuache kulalamikia wakubwa tu tutimize wajibu wetu.