mariavictima
Senior Member
- Jul 8, 2010
- 179
- 39
Nimeona nilete hii mada hapa JF ijadiliwa na pengine itapatiwa ufumbuzi maana naamini kuwa wahusika au Owners wa Tumaini Hospital ni wadau pia wa JF. Hivi mnaweza kuamini kuwa hospitali kubwa kama Tumaini haina kipimo cha X-ray? Inakuwa usumbufu mkubwa sana pale unapotakiwa kupigwa X-ray na kuambiwa uende hospitali nyingine ukafanye hicho kipimo halafu ulete majibu kwao Tumaini. Wanaoteseka na kusumbuka zaidi ni wagonjwa wanaotumia Bima ya afya kwani wengi wanaitegemea hospital ile. Hebu uongozi badilikeni na muweke vipimo vinavyoendana na hadhi ya hospitali yenu. Mbona mnapata pesa nyingi sana????