Uswahilini kuna fursa

Uswahilini kuna fursa

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
262
Reaction score
577
Kwa eneo la uswahilini katikati ya mji ambapo jamii inayoishi wengi ni waswahili, wamama, wanafunzi, watoto wengi sana, wafanyabiashara na wajasiriamali, jamii ya watu wanaopenda mambo ya miziki na cd za kikorea, jamii ya watu wanaopenda sherehe na birthday.

Eneo kama hilo unaweza kufanya biashara gani: Taja biashara kuu 7
 
Supu ya utumbo, vichwa vya Kuku, Miguu ya Kuku, Condom, kuwa mganga wa kienyeji..

Mengine wataongezea wenzangu.
Kuwa manju wa ngoma za mchiriku, usasambuaji (kwa mabinti), biashara ya kukodi matarumbeta ya kwenda kusutia na kwenye mafumanizi, supu ya pweza, urembo, simu za Itel, Infinix na TECNO, genge safi la vyakula...the opportunities are endless kwa kweli!
 
Kuwa na turubali na viti vya kukodi, kuwa na mziki wako kutegea anaolewa nani?....

Daaah fursa kama hizo na kuwapaka madada rangi kwenye kucha....
 
Kwa eneo la uswahilini katikati ya mji ambapo jamii inayoishi wengi ni waswahili, wamama, wanafunzi, watoto wengi sana, wafanyabiashara na wajasiriamali, jamii ya watu wanaopenda mambo ya miziki na cd za kikorea, jamii ya watu wanaopenda sherehe na birthday.

Eneo kama hilo unaweza kufanya biashara gani: Taja biashara kuu 7
1 genge

2 duka la lejaleja

3 banda la kuonyeshea mpila maigizo

4 kijiwe cha kahawa lakini kiwe kamili

5 banda la kufundishia chekechea

6 mama rishe supu chapati asubuhi mchana ugali na wali

7 mihogo ya kukaanga

zingatia bei yako iwe rafiki
 
biashara ya mama ntilie apa zingatia wingi wa chakula na sio ubora,

fungua sehemu ya play station maana watoto hawapendi shule

duka la mangi

banda la mpira

kibanda cha kurusha miziki, muvi na kukodisha cd za muvi za kibongo na za nje.
 
Kwa eneo la uswahilini katikati ya mji ambapo jamii inayoishi wengi ni waswahili, wamama, wanafunzi, watoto wengi sana, wafanyabiashara na wajasiriamali, jamii ya watu wanaopenda mambo ya miziki na cd za kikorea, jamii ya watu wanaopenda sherehe na birthday.

Eneo kama hilo unaweza kufanya biashara gani: Taja biashara kuu 7
Kuuza maharage yalichemshwa tu na mtu akinunua anaweza kwenda Kula kwa kuyaunga na kitunguu au nyanya au Kula Kama yalivyo

Kuuza chapati
 
Kwa eneo la uswahilini katikati ya mji ambapo jamii inayoishi wengi ni waswahili, wamama, wanafunzi, watoto wengi sana, wafanyabiashara na wajasiriamali, jamii ya watu wanaopenda mambo ya miziki na cd za kikorea, jamii ya watu wanaopenda sherehe na birthday.

Eneo kama hilo unaweza kufanya biashara gani: Taja biashara
Sasa mbona kama unaleta janja janja,najua unatumegea fursa zilizopo kumbe unataka tukupe fursa zinazopatikanamo🤔
 
Back
Top Bottom