Katika sehemu nisizopenda kuishi ni hizo, kwanza usipo angaria unaweza ukadumaza akiri yako ukicopy lifestyle yao, pili kizazi chako kitakuwa mashakani, mana maisha wanayoishi wanayajua wenyewe tu. Niliwahi kuishi mitaa fulani baada ya mambo yangu kutokwenda sawa,nikapata chumba cha 30k permonth, kilikuwa na kisebure kidogo
Usiku kucha mikiki mikiki, kuna watu wanaingia ndani saa sita usiku hadi saa nane, kutoka saa kumi za usiku, sa kumi kelele tayari zishaanza, maredio yanafunguriwa,kelele za watu bafuni, wenye pikipiki wana anza kupiga resi hizo michina yao, vurugu tupu kuanzia saa kumi kasoro hadi panakucha.
Wanawake wanalaza watoto saa tano hadi saa sita usiku,vile vidogo miaka mitatu minne kulala saa nne,saa tano kawaida,mara kitoto kianze kupigwa saa nne za usiku.Siku moja usiku mida ya saa tano mdada mmoja mwenye vitoto viwili akaanza kukichapa kitoto chake mida hiyo karibu na dirisha langu, kitoto kinalia sauti yote inaishia kwangu,aisee nilitoka nikamwangariaaa ila nikaona matendo yake yanafanana na yeye. Nikamuonya ,nikamwambia hawa watoto msidhani ya kwamba watapishana na nyie kwa malezi haya, hata kama ni umasikini sio ivo,mtoto miaka miwili yupo kodo hadi saa nne za usiku?,nilikalipia sana,eti anasema " amejinyea" kishindwe kujinyea kwa malezi hayo?!, vitoto vinaweuka bado vidogo.
Vyoo ndoo usisema,yani upo chooni mwingine wa juu yako anakutazama yote,kuna mitaa ya mwanza ilivyo na miamba yake usiombe uishi uswahilini.
Vituko ni vingi mno, watu akiri zao kama vile hazipo sawa, kwa kweli kama hukuwahi kuishi maisha hayo utapata shida sana. Niliteseka mno, mtu anakuja saa nane usiku anawasha redio kwa sauti kubwa hadi asubui, ukimwambia ni ugomvi, dah nilinyosha mikono, wadada kudanga ndo sifa ya mjini, kuna siku nilishinda pale nilijionea vituko, watu wanatambiana kwa kudanga, ila mimi walikuwa wananiheshimu kutokana na ukimya wangu pia na kuwa busy na mambo yangu.
Baada ya kodi yangu kuisha nilihama pale na kwenda kwenye uahueni kidogo .
Sent using
Jamii Forums mobile app