Uswahilini na starehe za kulazimisha

Ukienda dukani ufunge mlango, hata ukienda kuoga/ kukata gogo ufunge mlango la sivyo umeumia
Na usiku ukilala simu ufiche uvunguni mwa kitanda

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Marufuku kuchat hadi usinzie.
 
Hahah...
Mutu mubaya wewe
Kama hujaishi uswahilini basi bado hujaishi. Niliishi nyumba flani yaani yule Bibi alikua mwanga sijapata kuona, sema alikua ananipenda sana maana sikua na demu wala mademu. Akiamua kunizingua siku hio silali aiseeee, miaka ile ndio radio za FM zinaanza naamka naanza kusikiliza maombi. Hadi nikaokoka kwa lazima na kula kitimoto.
 
Mihogo ya kuchoma na embe za pilipili.. Nimepamiss Gomz aseee...
Shida vijana wanasema matusi mbele ya watu wazima na watu wazima hawajali.
Mtoto anavuta bangi mbele ya mzazi mzazi hajali..
Wakati na ukubwa huu mama ananiambia nisijaribu kugusa bia ila wengine hadi ugoro wanapiga mbele ya wazazi
 
Utumbo wa kuku maini na firigisi.
Tamu hatari. Na kichwa cha kuku.
Karibu uswazi
Tamu sana hizi basi tu huku mikoani hawajui haya mambo. Hivyo vitu tunamtupia nyau.
Tazara hapo tuliwahi kula mafirigisi na utumbo wenye pilipili. Zile pilipili sijui zimeungwa nini maana zilikua tamu unaweza lia ugali japo silagi pilipili ila nilipenda.
Lini utakuwepo Dsm tukale mafirigisi
 
Mimi maisha ya uswazi napenda tu zile kelele na kulivyochangamka kiujumla kiasi kwamba unaweza ukatoka hata saa sita usiku ukatembea bila wasiwasi kabisa,, Huwa sipendi sehemu ambayo ipo kimya saa mbili usiku tu tayari kila mtu kajifungia ndani ya geti lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkoa gani huo hawakaangi miguu ya kuku, utumbo, firigisi, vichwa, maini? Utakuwa unaishi mitaa ya kishua au mahali ambapo bado hapajachangamka wewe.

Bila kusahau vimiskaki vya shilingi 100, 100. na chachandu pembeni.

Unanunua mshikaki, unachovya kwenye chachandu hapo hapo kwenye libakuli unakula ukiwa umesimama.
Karibu sana huku uswazi nipo nimejaa tele.

Hata leo vers
 
Kuna tofauti ya chachandu na pilipili.? Hata sijui maana situmii vitu vya kuwasha.
Nipo huku kigoma sio mjini sana, huwezi kuta mtu kakaanga hayo mafirigisi. Eti hawana uhaba wa mboga..hata ukichoma utakula ww. Miskaki na aupu za mia mia zipo. Ahombo unakaa nalo siku nzima
 
Chachandu ndio pilipili.
Mjini lazima watakuwa wanakaanga[emoji3][emoji3]
 
Yale ni maisha wanayoishi kwakua hawana namna jaman wakipata not hamuwaoni uswazi.Yale sio maisha ya kujisifia.
Trust me,pale uwanja wa fisi manzese,hatokaa atokee rais wa nchi hii pale kama mtoto anazaliwa pale na kukulia pale mpaka utu uzima.

Mazingira yana influence sana afya ya akili ya mtoto.
Maisha ya uswaz ni ya kijinga sanaa.
Napafahm na nimeish sana huko nikiwa single but nilipoamua kuzaa na kulea wanangu niliamua kuhamaaaa
 
Hao wanga mimi ndio huwa napenda kuishi nao karibu, huwa nawanyuka kwa maombi hadi wanakaa sawa...

Majibu yake unayapata mchana kwa minuno na misonyo [emoji16]
 
Hao wanga mimi ndio huwa napenda kuishi nao karibu, huwa nawanyuka kwa maombi hadi wanakaa sawa...

Majibu yake unayapata mchana kwa minuno na misonyo [emoji16]
Yule Bibi alikua ananuna na siku hio kutwa nzima hamtaonana, hata ushinde hapo hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…