Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,335
- 1,967
Uswazi noma, kama ulifikiri uswahilini hakuna starehe umekosea sana, maskini jeuri wapo huko, hawapo tayari kushindwa, ni kama vituko, lakini ndio starehe yenyewe. Utawaambia nini!? Nyumba ya kupangisha inakaribu vyumba 10, ina Choo 1 cha nje, hakina mlango, hakikupauliwa kidogo sana, hakuna nafasi hata ya kujigeuza.
Bwana fulani anamiliki chumba 1 tu, anatoka chumbani kwake amejifunga msuli au upande wa kanga kiunoni kifua wazi, mbele katangulia mkewe na ndoo ndogo yenye maji na kata au kopo anasindikizwa bafuni kwenda kuoga, aende kimyakimya basi, la hasha; anaongea balaa, tena kwa sauti kubwa, huko bafuni mlango ndio huo upande wa kanga aliojifunga kiunoni, kichwa na kifua vyote vinaonekana kwa nje, hana haraka hana hofu yaani kwa raha zake.
Ukute sasa kuna wapangaji wenzie wanasubiri atoke na wao waingie. Ha,ha, haaaa!! mpita njia lazima utafurahi tu, yaani kama wapo kijiweni zogo lake si kitoto na wake zao hawapo nyuma kuwasapoti. Kwakweli maisha ya uswazi yanahitaji mazoea sana.
Siku moja nilikuwa nakatisha mtaa fulani nikawa nasikia mziki mkubwa, nilipokuja kukiona hicho kiredio sikutaka kuamini jinsi kilivyo kidogo, nikabaki tu najiuliza "Hivi wale matajiri wenye miredio mikubwa ndani ya majumba yao lakini wanasikiliza kwa sauti ya chini wao hawajui starehe?"