Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mara kwa mara nimekuwa nikijizuia kuandika chochote hapa JF chenye ubashiri kwa woga wa kuonekana ni muongo au mzushi, lakini baadaye ule ubashiri wangu (niliobakia nao akilini) kwa sehemu kubwa umekuwa ukitokea!
Na kwa kuwa JF ndio umekuwa mtandao wenye kueleweka au kuaminika zaidi hapa Tanzania kwa sasa hususani kwenye mwelekeo wa kuchambua yanayoendelea sasa au kubashiri yajayo, nimeona nami niandike kile ninachokiona akilini mwangu kuhusu yajayo kwenye fainali za mashindano ya mpira wa miguu ya FIFA kwa mwaka huu 2022 kule Qatar.
Natabiri timu ya taifa ya Argentina ikitwaa kombe la dunia.
Japokuwa mimi siyo mchambuzi wa mpira, lakini kwa haraka sana kuna vitu viko wazi mno kuona mwelekeo wa kombe hilo kwenda Argentina safari hii, na hapa ni baadhi.
1. Kilele cha hitimisho la historia ya soka kwa Leon Messi kwenye mashindano ya kombe la dunia. Mashindano haya huenda yakawa ndio shauku ya juu kwa Messi kufanya maajabu yake katika kuelekea kuhitimisha ubora wake kisoka.
Huyo mwamba pamoja na kuwika mnoo duniani, hakuwahi kuiongoza Argentina kutwaa Ubingwa wa Dunia. Jambo hilo linamuumiza sana, na atataka kulimaliza ili kuweka historia ya siku zote katika soka. Aliweza kufanya maajabu yake kwenye Copa America mwaka jana, huwezi kushindwa kufanya hivyo tena kwenye hii world Cup ya 2022.
2. Argentina wanakwenda kwenye mashindano haya wakiwa ni mabingwa watetezi wa kombe la Amerika ya kusini (Copa America) ambalo walilitwaa mwaka jana.
Kiuhalisia mashindano ya Copa America yaliyopita yalikuwa na ushindani wa hali ya juu na msisimko wa aina yake (bahati mbaya vyombo vya habari havikuyapa uzito mkubwa kama yale ya Ulaya kwa sababu za kibiashara), na bingwa wake lazima alikuwa ni tishio.
3. Kilele cha mafanikio ya kizazi cha dhahabu kwa timu ya taifa ya Argentina. Kikosi cha Argentina cha sasa huenda ndiyo kikosi bora zaidi cha Argentina chenye majina, vipaji na muunganiko wa kitimu kuliko vizazi vingine kadhaa vilivyopita na kushindwa kutwaa Kombe la Dunia.
2022 Tukutane Qatar.