Utabiri mechi ya Horoya vs Raja marudiano

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Kwa kuangalia vigezo tofauti ikiwemo mbinu na history za timu hizi mbili wanapokutana Guinea, naiona mechi inaweza kuisha kwa ushindi mwembamba kwa Guinea.

Mpira una mambo mengi ukiachana na ubora wa wachezaji kuna swala la mbinu pia. Raja mpaka sasa kwenye kundi lao ndio timu pekee ambayo haijaruhusu goli na ndio timu pekee kwenye kundi lao ndio ina magoli mengi, ila Horoya ni wamewekeza zaidi kwenye nidhamu, mbinu na ufundi.

Mpaka sasa Raja wameshakuwa na uhakika wa kufuzu, wakiwa wamebakisha game moja ya nyumbani hivyo wanaenda kucheza na Horoya pasipokuwa na tension kubwa sana, huku Horoya wao wakibebwa na History nzuri pindi wakicheza na Raja hapo Guinea, mechi itaisha kwa Horoya kushinda au sare. Ni vile navyoona mimi, kila mtu na muono wake.
 
Attachments

  • IMG_20230226_082538.jpg
    IMG_20230226_082538.jpg
    50.2 KB · Views: 4
Kama ikitokea Horoya akamfunga Raja, naamini huo ndio utakuwa mwisho wa Simba kwenye mashindano, kwasababu mpaka hapo Horoya atafikisha pointi 7, akiwa na game moja nyumbani dhidi ya Vipers, ambao nao naamini hawatatoka Guinea salama.

Simba Sc hata kama atashinda game zake zote za nyumbani, atafikisha pointi 9, hataweza tena kumfikia Horoya, hapo ndipo tutazikumbuka zile nafasi za wazi Bocco alizochezea kule Guinea tukaishia kufungwa 1-0.
 
Yaani raja mechi inayofuata ndo itaamua raja akiregeza tu kamba tumeisha otherwise asare Ili horoya wawe na points 5 then sisi tushinde Kwa vipers tuwe na 6 then horoya akija tupige tuwe 9 sisi yeye hata akienda kushinda kwa vipers awe na 8
 
Kumbe kabla ya kukutana jana, wameshakutana mara nne na kila mmoja kashindia kwake mechi mbili mbili. Ila chochote kinaweza tokea, history hachezi mpira, ila kwa nidhamu walionesha Morocco wanaweza kuambulia chochote pengine. Jana nilitegemea 3+ kwa Raja
 
Na ndio itakavyokua...wala usizunguke
 
Kwa kuangalia vigezo tofauti ikiwemo mbinu na history za timu hizi mbili wanapokutana Guinea, naiona mechi inaweza kuisha kwa ushindi mwembamba kwa Guinea.

Mpira una mambo mengi ukiachana na ubora wa wachezaji kuna swala la mbinu pia. Raja mpaka sasa kwenye kundi lao ndio timu pekee ambayo haijaruhusu goli na ndio timu pekee kwenye kundi lao ndio ina magoli mengi, ila Horoya ni wamewekeza zaidi kwenye nidhamu, mbinu na ufundi.

Mpaka sasa Raja wameshakuwa na uhakika wa kufuzu, wakiwa wamebakisha game moja ya nyumbani hivyo wanaenda kucheza na Horoya pasipokuwa na tension kubwa sana, huku Horoya wao wakibebwa na History nzuri pindi wakicheza na Raja hapo Guinea, mechi itaisha kwa Horoya kushinda au sare. Ni vile navyoona mimi, kila mtu na muono wake.
Sivyo uwazavyo mkuu. Raja lazima apiganie kuongoza kundi, hivyo hawezi legeza hata kidogo huko nyumbani kwa horoya, maana akilegeza akakaa vibaya akapigwa anajua horoya anaweza kuongoza kundi, na unajua ukiwa wa pili kwenye kundi kuna hatari kubwa ya kukutana na mbabe mwenzako hatua inayofuatia, nani anapenda hayo mambo ya kukutana na nbabe mwenzako hatua za awali namna hiyo.
 
Hii timu ilikuwa ya kupata point 3 away. Ingekuwa Simba ya kina Luis. Vipers ni ndugu zetu hawana cha kupoteza. Wakawakazie hawa kwao watoe hata droo tu
 
Yaani raja mechi inayofuata ndo itaamua raja akiregeza tu kamba tumeisha otherwise asare Ili horoya wawe na points 5 then sisi tushinde Kwa vipers tuwe na 6 then horoya akija tupige tuwe 9 sisi yeye hata akienda kushinda kwa vipers awe na 8
Hili kundi Simba na timu yetu hii hii, ingetakiwa tu-draw ugenini kwa Horoya, Vipers afe nje ndani, Horoya aje kufa Dsm, na Raja apate sare Dsm.

Maximum pointi 11 kwenye hili kundi kwa Simba ilikuwa inawezekana kabisa.
 
Kumbe kabla ya kukutana jana, wameshakutana mara nne na kila mmoja kashindia kwake mechi mbili mbili. Ila chochote kinaweza tokea, history hachezi mpira, ila kwa nidhamu walionesha Morocco wanaweza kuambulia chochote pengine. Jana nilitegemea 3+ kwa Raja
Hapa iwe iwavyo, Horoya asimfunge Raja Guinea, Simba itakuwa habari imekwisha.
 
Sivyo uwazavyo mkuu. Raja lazima apiganie kuongoza kundi, hivyo hawezi legeza hata kidogo huko nyumbani kwa horoya, maana akilegeza akakaa vibaya akapigwa anajua horoya anaweza kuongoza kundi, na unajua ukiwa wa pili kwenye kundi kuna hatari kubwa ya kukutana na mbabe mwenzako hatua inayofuatia, nani anapenda hayo mambo ya kukutana na nbabe mwenzako hatua za awali namna hiyo.
Horoya alishafanya hivyo mara mbili mbele ya Raja kule Guinea, na msimu uliopita ndio timu pekee iliyompa Horoya point tatu hivyo Horoya wanaweza kufanya tena hivyo kwenye marudiano.
 
Mimi naona mnapiga makelele.
Hii Simba yetu ya sasa haitishi ni simba koko. Inahitajika overhaul ya kikosi kizima.
 
Horoya hana uwezi wa kumfunga Raja, labda waamue tu
Kwenye mpira wa miguu huwa hakuna neno hawezi, kwenye mpira chochote kinaweza tokea. Horoya kucheza vile away dhidi ya Raja inaonekana kwenye mbinu sio haba wanajitahidi, usije kushangaa wakatpata sare hapa Tanzania kwa forward za Simba wanapata nafasi badala ya kutandika shuti anarudisha nyuma
 
Hii timu ilikuwa ya kupata point 3 away. Ingekuwa Simba ya kina Luis. Vipers ni ndugu zetu hawana cha kupoteza. Wakawakazie hawa kwao watoe hata droo tu
Samahani hivi huwa mawazo yako haya hasa kwenye tasnia ya mpira unayotoa kichwani kweli au Kwenye MAKALIO??
 
Kwa kuangalia vigezo tofauti ikiwemo mbinu na history za timu hizi mbili wanapokutana Guinea, naiona mechi inaweza kuisha kwa ushindi mwembamba kwa Guinea.

Mpira una mambo mengi ukiachana na ubora wa wachezaji kuna swala la mbinu pia. Raja mpaka sasa kwenye kundi lao ndio timu pekee ambayo haijaruhusu goli na ndio timu pekee kwenye kundi lao ndio ina magoli mengi, ila Horoya ni wamewekeza zaidi kwenye nidhamu, mbinu na ufundi.

Mpaka sasa Raja wameshakuwa na uhakika wa kufuzu, wakiwa wamebakisha game moja ya nyumbani hivyo wanaenda kucheza na Horoya pasipokuwa na tension kubwa sana, huku Horoya wao wakibebwa na History nzuri pindi wakicheza na Raja hapo Guinea, mechi itaisha kwa Horoya kushinda au sare. Ni vile navyoona mimi, kila mtu na muono wake.
Mimi naona simba tutoke tu tujipange vizuri kwa mwakani kwa mpira tunaocheza sasa huko mbele tutatia aibu sana.
 
Huwa sipendi mambo ya mpira wa nafasi yàko utegemee matokeo.ya mwingine ila basi tu
 
Back
Top Bottom