SHANTI
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 296
- 365
Pazia la kuichukua fomu za kugombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi huenda likafunguliwa Rasmi muda wowote kuanzia mwezi Juni 2020.
Sina hakika na ndoto yangu, Ila haya ndio niliyoyaona ndotoni.
Nawaona wanaume wawili wakichuana vikali sana, kiasi kwamba wanarandama kwa sifa na haiba inayorandana Kila pahala. Wasomi Hawa wawili wa kiwango cha juu wanazidiana sifa moja tu.
Mmoja ameishi na kukulia Zanzibar na mwingine ameishi na kukulia Dar es Salaam.
Wanaume hao Ni Profesa Makame Mbarawa Mnyaa na Dkt. Hussein Mwinyi.
Naona ukungu mzito watu wengi wanabishana hapana huyu hajakulia na kuishi huku iweje tumkabidhi jukumu zito hivi wakati ana kila nasaba na watu wa bara. Safari hii hatukubali lazima tufanye tutakavyo sisi na sio wao.
Naiona busara kubwa ikitumika kumaliza mgogoro huu kwa turufu ya jinsia. Unazuka mjadala kama ndio hivyo basi wakose wote na akae mwanamke ili kuondoa dhana ya upendeleo na visa vya nani ni nani.
Namuona mwanamke mwenye sauti ya mamlaka na akitokea kwenye kiti chenye maamuzi mazito akikubali kubeba gharama za kuinusuru chama na mpasuko. Namfananisha na Samia Suluhu Hassan. Nyota yake Ni Kali sana na ndiye anayewatuliza wanaume hawa wawili kwa kuvaa kiatu cha kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM huko visiwani Zanzibar.
Ndoto yangu haiishii hapa, namuona Mwenyekiti na kamati yake wanajifungia kwa muda na hawa wanaume wawili Kisha wanakubaliana kitu.
Siku chache baadaye nawaona wanaume hawa wanaongozana hadi Dodoma.
Namuona Mwenyekiti wa wa CCM anapitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu kuwa ndiye mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Nawaona wajumbe wa CCM wanaenda chemba kunong'onezana na kisha Mwenyekiti wa muda anamtangaza Dr. Hussein Mwinyi kubeba bendera ya Chama kama Mgombea mwenza wa Magufuli.
Ndoto inaendelea nawaona wajumbe wakimtaja Profesa kama Makamu Rais wa Zanzibar.
Nawaona wakitoka na nyuso za furaha Kila mmoja.
Usingizi unakatika nashtuka najiuliza ni kweli au ni mawaa ya ndoto.
Ngoja tusubiri media confirmation, mimi nishamaliza ndoto yangu.
Updates :
Dr.Mabodi ameonekana kupitia habari ya saa mbili usiku leo akitangaza kuwa zoezi kuichukua fomu ya Urais Zanzibar limefunguliwa na mkutano wenye kuamua mgombea utafanyika dodoma.
Hii Ni kwa sababu mgombea wa CCM anateuliwa na Halmashauri kuu ya Chama ambayo inakutana makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi pale dodoma.
Modes mnisaidie kuedit mbugi imeanza rasmi na tuone ndoto ikitimia au ikipotea
UPDATES
MEDIA CONFIRMATION # 1
HABARI ZA HUSSEIN MWINYI KUCHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR
MEDIA CONFIRMATION #2
PROFESA MAKAME MBARAWA MNYAA ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR
MEDIA CONFIRMATION #2
PROESA MAKAME MBARAWA ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR
MEDIA CONFIRMATION #2
PROFESA MAKAME MBARAWA MNAA ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR
UPDATES
MIEZI KAHAAA MBELE NDOTO INATIMIA KWELI NA SAMIA ANAAPISHWA KUWA RAIS WA JMT