Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Ghassani kasha weka ruhusa
kwa masharti yafuatayo:

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
Harith Ghassany
info@kwaherikwaheri.com
SOMA HAPA KWANZA
Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani.

Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo:

Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi • binafsi ya kitabu
Kutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo • wa kitabu
Kutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi•
Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: Creative Commons — Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States — CC BY-NC-ND 3.0 US
Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi.
Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu.
Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao.
Kwa vile walengwa wa mfumo huu wa Free Electronic Downloading ni Wazanzibari na Watanganyika wa kawaida, basi ipo haja kwa wale wenye uwezo, wakiwa ndani ama nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa mchango wa kuvinunua vitabu ama kupitia mtandao wa kitabu, http://kwaherikwaheri.com, au moja kwa moja kutoka Lulu na kuwafikishia walimu na wanafunzi walioko kwenye skuli na vyuo vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Skuli, vyuo, maktaba, taasisi na watu binafsi wanaweza kumuandikia moja kwa moja mwandishi kupitia mtandao wa kitabu http://kwaherikwaheri.com ikiwa watahitaji kupata msaada wa wafadhili watakaojitokeza kusaidia. Wafadhili ambao hawatopenda majina yao kujulikana, wamuarifu mwandishi. Majina yao yatahifadhiwa na mwandishi anatanguliza shukrani za dhati kwa ukarimu wao.
Mwandishi pia anatanguliza ombi na shukrani maalum kwa watakaoweza kusaidia kuviwezesha vituo vya mitandao vilivyopo Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara kutoa muda maalum wa huduma za mtandao kwa bei nafuu kwa ajili ya wale watakaopenda kukisoma, kukichukua na ama kukihifadhi kitabu hiki kwenye vyombo vyao.
Kuanzia hivi sasa, Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kimo machoni mwako. Fungua kurasa zake, zama na zamia kwenye bahari yake na ibuka na lulu zilizomo ndani yake.
Mnakaribishwa nyote—walio karibu na walioko mbali.

http://kwaherikwaheri.com
 
Nimesoma hoja zako na nitakujibu hivi.

Ni mtafiti gani ambaye amefanya tafiti na akaja na majibu kuwa Zanzibar hawafaidiki na Muungano?

Kinyume chake Ni mtafiti yupi amewahi kuja na andiko kuwa Tanganyika inanufaika zaidi kuliko Zanzibar.

Sina hakika Ila nasikia Bakhresa Ana nasaba na Uzanzibari. Tufanye wewe ndio bwana Bakhresa na unatokea Zanzibar na Huku Bara Asimame Mo Dewji sababu kwao singida.

Tufanye utafiti wa manufaa ya biashara na uwekezaji Kama kigezo Cha kunufaika na Muungano.

Kwa jicho la hisia Kama ulivyoandika na kusema bara wanafaidi ukiwatizama Bakhresa na Mo Nani kanufaika na fursa ya biashara zaidi ya mwenzake?

Jibu jepesi tu ukileta ubaguzi wa aina yeyote Bakhresa atapoteza pakubwa kuliko Mo. Na kamwe Mzanzibar mwenye maono mapana anaitumia fursa ya idadi kubwa ya watu wa Tanzania bara kufaidi fursa ya Muungano.

Kigezo Cha pili Cha utafiti kiwe kumiliki ardhi.

Je , Ni watNganyika wangapi Leo wakija Zanzibar Wana uwezo wa kununua na kumiliki ardhi huko visiwani,

Je, Ni wazanzibar wangapi wanaweza kuja bara leo hii na kumiliki ardhi .

Ukifanya survey ya hisia Kama yako jibu lipo wazi kwamba sisi hatunufaiki na ardhi ya Zanzibar, kinyume chake wazanzibar wanamiliki mpaka mashamba makubwa Sana na nyumba wamejenga hukuhuku. Eg kigamboni.


Sio vizuri kulaumu ingia ndani fanya tafiti,halafu utoke kifua mbele vinginevyo hizo Ni hisia na tutaheshimu hisia zako kwa sababu ya Uhuru wa kutoa maoni . So hoja ya sisi kunufaika Ni dhaifu na inafia hapa.

TFF & MISAADA

Naanzia mbali kiduchu, Siku tulipoungana ndio siku Zanzibar alipoteza kiti chake UN.

Athari ya kupoteza kiti inaonekana FIFA . Ili uwe mwanachama wa FIFA lazima uwe na kiti UN . Huu ndio msumari wa kwanza kwenu, ili utambuliwe CAF nao Ni lazima Uwe na Kiti AU.

Ninyi hamna sifa hiyo,mwenye nayo Ni Tanzania. Anayetambuliwa FIFA &CAF Ni TFF .

Zanzibar mliamua kujitegemea michezo, Sasa mnataka fedha za TFF za Nini?
Jibu Ni moja tu, rudisheni michezo kwenye Mambo ya Muungano. Kero za michezo zitaisha.Kisha vunjeni ZFF na rasmi TFF ipewe mamlaka ya bara na visiwani. Kabla ya hili iandikwe Memorandum ya mgawanyo wa Mali hisa zenu Kama BOT. Immediately mtapata misaada ya michezo bila kelele na malalamiko.

Misaada duniani hakuna, Kila mtu anapambana na Hali yake, Sasa hivi Kuna mikopo ya unafuu unakuja kwa mgongo wa misaada unapewa pesa unatoa fursa za kibiashara kwa waliokupa pesa.

Nimetafiti misaada ya bure nikagundua michache Haina masharti magumu Kama ya ushoga lakini kiasi chake Ni kidogo Sana haizidi 5B

Pesa hizi hata Bakhresa anaweza kuwapa bure na asiwadai.

Mwisho niseme hata sisi Tanganyika tuna madai yetu, ndio maana kwenye mapato tumeamua Kila akale alipopeleka mboga.
 
Itabidi lianzishwe jukwaa maalum kwa ajili historia ya Zanzibar na Tanganyika.
Kisha humo yawekwe madini adhimu Kama haya .
Nakuhaidi nitadownload n akukisoma nipate madini adhimu ya Zanzibar
[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Itabidi lianzishwe jukwaa maalum kwa ajili historia ya Zanzibar na Tanganyika.
Kisha humo yawekwe madini adhimu Kama haya .
Nakuhaidi nitadownload n akukisoma nipate madini adhimu ya Zanzibar
[emoji106][emoji106][emoji106]
Sasa tuendelee na Chaguo la Raisi kwa wazanzibari.
Raisi tumtakae awe hivi.:
1.Mzalendo wa kuipenda, kuitetea na kuilinda Dola ya Zanzibar na Maslahi yake ndani ya Muungano.

2.Asiwe Mbaguzi wala mtesaji wa watu wasiokuwa na hatia.

3.Asimamie ajenda ya Mamlaka kamili na Muungano wenye usawa kwa Pande zote.

4.Adumishe udugu wetuwa damu na Oman,Tanganyika, China, India,Yemen, Somalia,Indonesia na Commoro ambazo zote nchi hizo zina muingiliano mkubwa na Zanzibar tangu Zama na Zama

5. Atuahidi kutupatia katiba mpya itakayoharamisha ubaguzi wa aina yoyote na kuwa kosa la jinai kwa mwenye kuusema,kuutangaza au kuutetea ubaguzi wa kijinsia,kikabila,kirangi na kimadhehebu.

6.Alete mtengamano wa kitaifa(Commission of truth and reconciliation) utakao ruhusu kila mwenye makovu ya uovu aliofanyiwa na chombo chochote kiwe cha dola au mtu binafsi tokea Mapinduzi hadi leo aje hadharani mbele ya tume aueleze na kuridhiana ,kusameheana au kupeleka kesi yake mahakamani.

7. Atuahidi Tume huru ya uchaguzi , mahakama huru, na Uhuru wa kujieleza bila ya vikwazo kwa kila raia na kulindwa haki za kila raia wa Zanzibar na hakizake zipewe kipaumbele dhidi ya raia wa nchi yoyote duniani. Kama ilivyo nchi za wenzetu Arabuni, au India, au Uk.

NB;Ifahamike kuwa

Mgombea Uraisi yoyote yule awe wa chama chochote kile akituahidi kutuchimbia mafuta, Gesi, na Kujenga viwanda vya samaki bila ya kubadili Mfumo wa siasa(Muundo wa Muungano) huyo anatudanganya, kama walivyotudanganya watanguklizi wake.

Nashauri Tusimuunge mkono Ngo,heri tubaki bila kupiga kura ikiwa wote watakuwa na muelekeo huo wa kutudanganya.

HII NDIO ZANZIBAR TUITAKAYO KWA RAISI AJAYE LAZIMA AJIPANGE HIVYO.
 
Nimefurahi kuona ukiitathimini Zanzibar muitakayo. Mijadala mipana Kama hii huwa Haina wawakilishi wazuri kwenye vyama vya siasa.

Kwa sababu wengi waliopo au wanaoshiriki siasa hawana maono mapana Kama yako. Thamani yenu sio vitu au ahadi zisizotekelezeka thamani yenu tunu za utu wenu.

Kwa sababu Mimi na wewe hatupo kwenye ulingo wa siasa tuingie rasmi kutafuta nafasi za uwakilishi,ubunge na usheha.
Wewe una kitu kikubwa Sana ambacho wanasiasa wa Zanzibar wanakikosa. Kwanza mstahamilivu mwenye kusikia ya wenzako na pia unajibu hoja na sio personality. Angelikuwa mtu mwingine angelinishambulia Mimi binafsi na sio hoja.
Nimefurahi umeshiriki kuichagiza ndoto yangu na Sasa unanifanya nijiulize hata hao niliowaota kwenye ndoto wanazo fikra zenye mazuri Kama yako?

Wanasiasa wa bara na visiwani wanasukumwa kushiriki siasa kwa manufaa ya kibiashara, umaarufu wa pesa, historia ya familia, na aghalabu mapenzi ya kuleta maendeleo Kama ulivyoona wewe. Wenye maono Kama wewe wanapigwa fitna , wanahasadiwa na kufukuzwa kwenye vyama vya siasa.

Ngoja kesho ifike tuone Nani atakuwa wa kwanza kuichukua fomu pale kisiwa ndui. Kisha tumsikie sababu za yeye kuomba apeee bendera ya CCM Kama Mgombea.

Nayachukua maoni yako Kama Azimio namba moja kwenye ndoto yangu. Kisha nitaanza kuoanisha mawazo yako na hao wanasiasa wanaochukua fomu tukiona hawana uelekeo tutaandika mada ya kuwafungua mawazo wananchi ili wajue kuwa tatizo sio mtu Bali hakuna mwenye ndoto za kuyatatua matatizo ya Zanzibar kwa angle ulizotizama wewe.
Wakati Ni Mwalimu mzuri na tiketi na popcorn na juisi huku tukiwatizama watia Nia na sisi kazi yetu Ni kuwachambua kwa kina mmoja mmoja
 


Shanti , kuna suala la ulinzi ambalo Juma Duni aliwahi kulizungumzia.

Zanzibar haina mpaka na Uganda, Congo , Zambia, Malawi, Rwanda , Burundi.

Jeshi la kazi gani zaidi ya kuitia gharama Zanzibar tu???

Matatizo ya mpaka ni ya Tanganyika si ya Zanzibar.

Ulinzi wa Zanzibar unatosha kufanywa na KMKM , Polisi, na Mgambo. Hayo majeshi ni kuwaulisha vijana wetu , kwa ugomvi usiowahusu huko Tanganyika na kuitia nchi umasikini.

Ni wakati wa Zanzibar kuwa na mamlaka yake na kuondokana na hali hii kama nchi nyingi za visiwa zilivyo
 
Hizo ndio dharau zisizo saidiakatika taifa hili. Wengi kati yenu hamujijui wala hamujitambui.na hii inakuja sababu akili ndogo. Hivo nyinyi hamuna historia ya taifa lenu?. Sisi wazanzibari asilia tunajijua na tunajitambua. Huu UKOLONI wenu umekwisha sasa hivi. Bila ya vyombo vya usalama, sisi tulikwisha waambia zamani kuwa ukoloni tumeukataa. Haiwezekani kutawaliwa na mwafrika mwenzetu na kejeli juu.
 
wacha porojo mzee peleka porojo hizo kanisani hivi hong kong ni nchi?? au Palestine? wacha ubaraa mzee
 
wacha porojo mzee peleka porojo hizo kanisani hivi hong kong ni nchi?? au Palestine? wacha ubaraa mzee
Huyu anaongelea nini?
Au karukia gari kwa mbele?
Usiifananishe zanzibar na Palestina au Hon kong.
Hii ni jamuhuri ya muungano wa hiari.
Nyerere atakutosheleza kiu yako wewe.
 

Attachments

  • NYERERE ANAJUA KUWA TANZANIA IMEUNDWA NA NCHI 2 HURU .mp4
    15.5 MB
Update:

Dr.Mabodi ameonekana kupitia habari ya saa mbili usiku leo akitangaza kuwa zoezi kuichukua fomu ya Urais Zanzibar limefunguliwa na mkutano wenye kuamua mgombea utafanyika dodoma.
Hii Ni kwa sababu mgombea wa CCM anateuliwa na Halmashauri kuu ya Chama ambayo inakutana makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi pale dodoma.
Modes mnisaidie kuedit mbugi imeanza rasmi na tuone ndoto ikitimia au ikipotea
 
UPNDE WA APINZANI JEE HUJASIKIA FUNUNU?
MAANA SISI WENGINE HUWAGA HATUKO KARIBU NA SIASA ZA MITAANI, WLA KWENYE MAGAZETI.
 
Km ambavyo TUNDU LISSSU alivyotabiri udikteta na umekua
 
Mkuu kwa Zanzibar bado sana hawako tayari kutawaliwa na mwanamke,bado wanamfumo dume,ila kwa rais huenda akawa mwinyi au shamte vuai hawa wawili sana asilimia ,80% ya kuukwaa urais wa zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app

Nalandana nawe hiyo hoja yako itamsumbua sana Samia wakati wa kugombea na hata CCM watapata tabu kumnadi ila mleta mada ametabiri vizuri.
 
UPNDE WA APINZANI JEE HUJASIKIA FUNUNU?
MAANA SISI WENGINE HUWAGA HATUKO KARIBU NA SIASA ZA MITAANI, WLA KWENYE MAGAZETI.
Mungu akipenda nitashusha Uzi wa upinzani muda si mrefu
 

The opposite is very true, Mwinyi will preside over Zanzibar in the interim of 5yrs before he becomes the URT President this is for sure. Best wishes Broo, I wanna be there so God keep alive to witness all this. I submit.
 

The leader of URT baada ya Magufuli mtake msitake ni mwanamtandao achana na hao vituko, our son/daughter whatever name will be on political holiday as we strategize. They gonna be fully fledged prepared and as well as dismantled almost every blockage by 95%. hizo hiiii.....twafwaa....hii okolachi....bakyitegede zote hola.
 
Nchi zetu hizi zenye demokrasia kiduchu bado sana kuongozwa na mwanamke. Tujenge kwanza misingi ya demokrasia na utawala bora ndipo wapewe nchi wanawake. Bado sana Afrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…