Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Rais wa zanzibar ni maalim seif hamad.
Kama uchaguzi utakuwa huru na HAKI.
 
Yule jamaa ana "laana" ya JKN; Kama alishindwa kupata nomination visiwani 1985 ili we sehemu ya cabinet; basi kama ambavyo EL na Mzee Malecela walikosa sifa za kupenya 5bora; ndiyo same principle inayomfanya huyo "kipenzi cha wapiga kura wa kisiwa chake" kukosa sifa. Bahati mbaya mtoa laana alishatangulia mbele za haki

Mtoa laana naye Laanatullahi si mungu si mtume , Iman petro hakutegemea maisha yake kupanda helicopter na aliipanda. Madhali unaishi umtegemee Allah tu
 
It's normal kwa watoto waliokulia Ikulu, kuja kuwa marais, hivyo ikitokea baada ya Mwinyi akaja Mwinyi, tulikuwa na Karume, akaja Karume, jirani tuna Kenyatta na Kenyatta, DRC Kabila na Kabila, . Kati ya nchi 54 za bara la Africa, nepotism kwenye urais nimetokea mara 38! Na sio Africa tuu,hata US kulikuwa Adams na Adam's, na Bush na Bush, India Gandhi na Gadhi, Pakistani Bhutto etc.

2015 Makongoro aligombea.
Hivyo hakuna cha ajabu.
P

Mimi nawashangaa wanamapinduzi fake wa Zanzibar na vibaraka wa Tanganyika.

Tunaambiwa Uliondoshwa utawala wa kifalme lakini hadi leo ndio unaotumiwa ili wengine kunyimwa haki ya kuitawala znz.

Wakati huo wanapiganiwa waendelee kutawala ni koo za kifalme.

Kumbe ufalme wa Ali Hassan Mwinyi kutoka mkuranga ndio wenye haki kutawala, ufalme wa Ali Karume kutoka Malawi ndio nao unatetea.

Yako wapi Mapinduzi ya wakwezi na wakulima?

Wazanzibar tumekua wapumbavu kiasi gani kufikishwa hali hii.

Hivyo akitoka Ali Hassan utakuja wa dr Shein.

Naona aliyekosa bahati wa kujenga ufalme ni Salmini na Mzee Abdulwakili wazaliwa halisi wa visiwa.
Hii laana ya CCM na kanisa Katoliki itaisha
 
Suala la account ya pamoja, kweli bado ni changamoto, kwasababu serikali ya JMT ndio serikali ya muungano kwa mambo yote ya muungano, at the same time, serikali hii hii ya JMT ndio serikali ya Tanganyika kwa mambo yasiyo ya muungano hivyo kwa wizara zote za muungano zina a single budget kwa muungano na Tanzania bara, mfano wizara ya elimu kwa elimu ya msingi sio ya muungano ni Tanzania bara, na wizara hiyo hiyo kwa elimu ya juu ni ya muungano, kwenye budgeting inaandaliwa budget moja.

The same applies kwa mapato, TRA inakusanya mapato yote ya shughuli za muungano na shughuli za Tanzania bara.

Ili ifunguliwe account ya pamoja, ni lazima mapato yote ya muungano yatenganishwe na mapato ya Tanzania bara, halafu hayo mapato ya muungano ndio yafunguliwe account ya pamoja ambayo Zanzibar pia nitachangia. Baada ya kuyajua mapato ya muungano, inatakiwa iandaliwe budget ya kuendesha muungano, mapato ya muungano yasipotosha kugharimia kuendesha muungano, then serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar zinachangia kwa uwiano wa asilimia 4.5% Zanzibar na asilimia 95.5% Tanzania bara.

Ili hili liwezekane kwanza lazima tuwe na serikali 3, serikali ya Tanzania Bara, serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar. Mapato yote ya muungano yatatenganishwa na kuweka account ya pamoja ambayo ndio sasa itagharimia muungano.
Jaji Warioba ni muongo?!- BLW halikupendekeza serikali tatu!-Mhe.Pandu Ameir Kificho!.

Solution ya kudumu ya kero ni ni kuwa na serikali moja.
Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, Then "Twende kwenye Serikali Moja!".

P
Good Explaination Mr. P
Lakini ujuwe hilo suala la A/c ya pamoja ni takwa la kikatiba, limo ndani ya katiba ,yamkini waliyafikiria yote hayo,ila sasa kuna ukweli fulani unaepuwa hapo, Ujuwe kuwa kuna mmoja anadhulumiwa, si mchezo, yatoshs kwa hilo kusema kuwa hakuna nia safi kwa upande unaotakiwa kutekeleza jambo hilo wala hawaoneshi nia ya kulifanyia angalau udadisi na kubaini kuwa haiwezekani walete option nyingine,
Any way Umejaribu kulifafanua, lakini sinahaja ya kuwakosoa walioliweka humo ndani ya katiba, nikiamini ni weledi wa kupanga na kujuwa .Illa naona Tuhuma tuu za ubaya na ubabe haziwaepuki.
 
N

Naomba ushauri, kisiasa makamu wa raisi TZ na raisi wa Zanzibar nani zaidi?
Ukitamka Jamhuri ya Muungano Tanzania, protokali inambeba Makamu wa Rais wa JMT ambaye Ni Samia SULUHU Hassan .
Tizama shughuli zenye sura ya JMT utakubaliana Nami kuwa Makamu wa
Rais anamzidi Rais wa Zanzibar.

Mfano: Sherehe za Muungano zote, ukipata wasaa ingia YouTube halafu tizama kuingia na kutoka viongozi utaona wanavyoingua na kutoka Rais wa Zanzibar huenda anaanza kuingia then ,Majaliwa halafu Samia na wa mwisho JPM .
Kinyume chake kutoka anaanza JPM, Samia,Majaliwa .....Rais wa ZNZ

Kwenye Sherehe za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar protokali inageuka.

Hapa protokali inampendelea Rais wa ZNZ , ataanza kuingia Samia SULUHU na ...... Kisha Rais wa Zanzibar atakuwa wa Mwisho kuingia kwa sababu ndiye Rais na bendera ya Rais ikisimama inamtambua yeye ndiye mkubwa wa itifaki.

Mengineyo JMT

*Rais wa Zanzibar hawezi kutoa amri kwa majeshi ya Muungano kuingia vitani au ulinzi wa mipaka ya JMT

*Endapo Rais aliyeko madarakani ataugua kiasi Cha kushindwa kuliongiza Taifa Makamu wa Rais ataapishwa kuongoza Taifa na sio wa Zanzibar.

*Rais wa Zanzibar anaingua Kama waziri kwenye kikao Cha Baraza la mawaziri wa JMT. Ukitaka kujua tafuta picha za vikao vya ikulu halafu angalia mpangilio utaona Majaliwa na Samia wanakata kushoto na Julia halafu mbali kabisa utamuona Rais wa Zanzibar.

Hapo ndio utajua POWER inamaanisha Nini?
 
Unakumbuka utabiri wa 2015? Nadhani kadri tunavyoenda mbele ndivyo majitu ya ajabu ajabu yataendelea kuongoza nchi
 
Hii nimeipenda sana Mr.P
Sasa tunafikaje huko kwenye moja?
Hapo ndio msema kweli ?
Ikiwa kweli wazanzibari wanaona Muungano nimwema kwao na umewanufaisha sanaa hadi kuwa hawawezi kuuukosa,basi waulizwe kwa kura ya Maoni.

Najua jambo hili JMT hawataki hata kulisikia, hata kama ni kwa kuelekea serikali 1.

Unajua kwa nini?

Kwa sababu wanaogopa UKWELI UTADHIHIRI NA UWONGO UTAJITENGA.

Basi
Waulizwe wazanzibari ''serikali 2 kuelekea 1 au serikali 2 kuelekea 3''? na kura hiyo iwe free and fare isimamiwe na watu waadilifu kama jumuiya ya commonwelth hivi isiwe tume zetu hizi za ZEC au NEC machaguo ya Waheshimiwa wa CCM.

WAZANZIBARI TUKO TAYARI KULETA SERIKALI MOJA ,LAKINI KWA KURA YA MAONI ILIYO HURU
TUULIZWE 2--->3 au 2----->1 muone uhondo 😉🙏

[TABLE=collapse]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD valign="top"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
hakuna mfumo wa kijamii wala baba ake wakikubali wabara ndio yupi awe rais ndie anayetangazwa

Suala ni mwanamke yupi wa Zanzibar atakayekubali kuwa raisi??!! --- labda atokee Bara,🤣
 
Is Hussein Ali Mwinyi (Zanzibar 2020-2025)

Hussein Ali Mwinyi(Tanzania 2025-2030)

Wale mataga sifieni kwa machale Zama zitabadilika

Mnaweza kosa kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Deni la umeme lazima muwasamehe,wao wana madeni makubwa wanakudaini, lakini kwa sababu wao ni wastaarabu, kwavile wanakuchukulieni kama ndugu,wanakuwa hawapigi kelele Sana kuhusu madeni wanayokudaini..

Hivi unajua kuwa Benk of Tanzania (BOT) imeundwa kwa Pesa za Zanzibar,..

mkawaahidi Wazanzibari kuwa mtawalipa faida kwa kila kinachopatikana kutoka BOT

Je mnawalipa?je unajua ni kiasi gani Zanzibar inaidai Tanganyika?..

KuhusuDeni la umeme, Watanganyika hawajawasamehe Wazanzibari Deni hilo,isipokuwa wanapunguza deni wanalodaiwa..

Kwa wale? Wasiofahamu nini kinaendelea ndio,mnaambiwa kuwa Zanzibar imesamehewa deni la Umeme, lakini ukweli sio huo
Niliwahi kumsikia Juma Duni Haji akizungumza maslahi ya Zanzibar kwenye uwekezaji wa BOT.
Akisema Zanzibar wanamiliki hisa 11 na 89 Tanganyika.

Haya twende kwenye factor za uwekezaji. Gawiwo linatolewa baada ya mapato na matumizi.

Kama Ni kweli hebu jiulize Ni miradi mingapi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania serikali iliwahi kupata gawiwo lake kwa wakati kwa kipindi chote Cha miaka Hamsini na ushehee ya Muungano wetu.

Pili kwenye uwekezaji Kuna kugawana hasara na madeni yanayitokana gharama za uendeshaji. Je Ni Mara ngapi Serikali JMT iliwahi kupata hasara ya uwekezaji.

Je ,tukifanya tathimini ya ufilisi wa Amana na uwekezaji pale BOT bado Zanzibar wanamiliki 11?

Tatu ,michango na Gharama za uendeshaji wa serikali ya JMT Zanzibar anachangiaje? Bado anamudu kulipia gharama za ULINZI, kwa maana ya majeshi ya JWTZ na vikosi vyake?
Jeshi la polisi,Usalama wa Taifa.
Nakutolea mfano huu ili ujifunze kutokuwa na ushabiki Bali uwe unajenga hoja kwa misingi mbali mbali.

Ukija ukapewa hesabu za mapato na matumizi na hasara tuliyoipata, then maamuzi ya ufilisi yakafanywa na RITA na yumkini baada ya evaluation mkaambiwa kwa Hali Leo uwekezaji wa ZanIbar BOT sio wa 11% utafanyaje? Au ukiambiwa hamna kabisa utafanyaje?

Sioni dalili za kuongezeka kwa uwekezaji wa Zanzibar BOT kwa trend ya uchumi wetu baada ya anguko kubwa lililotokana na Vita ya KAGERA.

Saada mkuya anajua thamani ya uwekezaji wenu BOT lakini hakuwahi kusema kwa majivuni hivi nadhani alijua ukweli wa Mambo.

Nikusaidie tu pale BOT TRA wanashea akaunti ya Mapato kwa misingi wa UTAKULA ULIPOPELEKA MBOGA.

Fuatilia vizuri

*Ukinunua vocha bara ukaongea kiduchu bara Kisha ukaimalizia Zanzibar.
Mgawanyo Kodi ya Ile vocha utategemea dk ulizotumia bara na visiwani.

*Ukichanja kadi ya ATM bara Kodi Ni bara, ukichanja Zenji inabaki huko.

*Ukinunua Gari Zanzibar sajili na ulitumie hukohuko na ukinunua bara litumie hukuhuku kinyume chake uwe permitty ya muda yenye kuineaha kuwa utarudi upande mwingine baada ya muda other wise sajili upya.
Ndio maana Zenji kumiliki ndiga Ni rahisi kuliko bara.

*Diamond kafungua TV Zanzibar, bara kafungua kituo Cha kuzalisha vipindi.hapa Kuna KAMPUNI mbili tofauti.moja inamiliki Tv na nyingine inamiliki uzalishaji na watangazaji .

Haya ndio masharti ya TCRA na ZCRA
Fee ya leseni analipa Zenji, Kodi ya Mapato anakupa bara, jiulize kwa Nini hv.
Jibu Ni UTAKULA ULIPOPELEKA MBOGA.
 
Okello angawafyeka wote kabisa wa jamii ile!, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo!, alikuwa anakwenda kufanya kufanya genocide.
Hahahaaa nilijuwa utamsingizia Okelo pekeyake kwa dhambi hii ya mauwaji (Genocide) ili Tanganyika ya Nyerere na Kambona iwe safi, lakini si alikuwa na kikosi chake,
wale watu waliotokea SAKURA umewasahau, wengi wao tunaohapa zanzibar na vizazi vyao wanaishi hadi leo wapo maeneo ya KWAHANI,MAKADARA,JANGOMBE,MEYA ,MAGOMENI , SEBLENI NA kwengineko. Tena bado hadi leo wanajifaharisha kufanya Mambo yale na Okelo. Genocide,na ethnick cleansing ilifanyika hapa unguja kwa kisingizio cha Mapinduzi.Hata Mzee Karume Hakuridhia matendo yale kufanyika katika kiwango kilelakini kambi ya Sakura ilishapanga Ubaya Ule chini ya Mr X
Pascal Malizia hapo wewe unajua mengi
 
Nimefuatilia malumbano yako na Paskali, nimeona ipo haja ya wataalamu wa historian na waandishi wa kale watusaidie kupanua Nini kilijiri kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kizazi Cha leo na hususani jamii Forums tunaye YERRICKO NYERERE . nimesoma nakala ya kitabu chake Cha Ujasusi wa kidola na kiuchumi ukurasa 99 mpaka 159 amejibu kwa ufasaha Jambo mnalolibishania.

Nitoe Rai kwa moderator wamtafute Yerricko na kuzingatia Faida za imma wa Watanzania atoe idhini andiko lake la kwenye kitabu lisomwe na Kila mmoja bure ili kutuongea maarifa na Nini chanzo Cha Mapinduzi na hatma ya kifo Cha karume.

Nimeshindwa kuposti screen shot za kitabu kwa sababu lazima tuheshimu haki miliki ya uandishi wa Yerricko. Vinginevyo wote mko sahihi.

Nawasihi tuendelee na ndoto na kupeana mawazo mazuri Kila siku sababu sisi Ni watu wa fikra pevu.
IMG_20200531_111710_7.jpeg
IMG_20200531_111656_5.jpeg
 
Niliwahi kumsikia Juma Duni Haji akizungumza maslahi ya Zanzibar kwenye uwekezaji wa BOT.
Akisema Zanzibar wanamiliki hisa 11 na 89 Tanganyika.

Haya twende kwenye factor za uwekezaji. Gawiwo linatolewa baada ya mapato na matumizi.

Kama Ni kweli hebu jiulize Ni miradi mingapi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania serikali iliwahi kupata gawiwo lake kwa wakati kwa kipindi chote Cha miaka Hamsini na ushehee ya Muungano wetu.

Pili kwenye uwekezaji Kuna kugawana hasara na madeni yanayitokana gharama za uendeshaji. Je Ni Mara ngapi Serikali JMT iliwahi kupata hasara ya uwekezaji.

Je ,tukifanya tathimini ya ufilisi wa Amana na uwekezaji pale BOT bado Zanzibar wanamiliki 11?

Tatu ,michango na Gharama za uendeshaji wa serikali ya JMT Zanzibar anachangiaje? Bado anamudu kulipia gharama za ULINZI, kwa maana ya majeshi ya JWTZ na vikosi vyake?
Jeshi la polisi,Usalama wa Taifa.
Nakutolea mfano huu ili ujifunze kutokuwa na ushabiki Bali uwe unajenga hoja kwa misingi mbali mbali.

Ukija ukapewa hesabu za mapato na matumizi na hasara tuliyoipata, then maamuzi ya ufilisi yakafanywa na RITA na yumkini baada ya evaluation mkaambiwa kwa Hali Leo uwekezaji wa ZanIbar BOT sio wa 11% utafanyaje? Au ukiambiwa hamna kabisa utafanyaje?

Sioni dalili za kuongezeka kwa uwekezaji wa Zanzibar BOT kwa trend ya uchumi wetu baada ya anguko kubwa lililotokana na Vita ya KAGERA.

Saada mkuya anajua thamani ya uwekezaji wenu BOT lakini hakuwahi kusema kwa majivuni hivi nadhani alijua ukweli wa Mambo.

Nikusaidie tu pale BOT TRA wanashea akaunti ya Mapato kwa misingi wa UTAKULA ULIPOPELEKA MBOGA.

Fuatilia vizuri

*Ukinunua vocha bara ukaongea kiduchu bara Kisha ukaimalizia Zanzibar.
Mgawanyo Kodi ya Ile vocha utategemea dk ulizotumia bara na visiwani.

*Ukichanja kadi ya ATM bara Kodi Ni bara, ukichanja Zenji inabaki huko.

*Ukinunua Gari Zanzibar sajili na ulitumie hukohuko na ukinunua bara litumie hukuhuku kinyume chake uwe permitty ya muda yenye kuineaha kuwa utarudi upande mwingine baada ya muda other wise sajili upya.
Ndio maana Zenji kumiliki ndiga Ni rahisi kuliko bara.

*Diamond kafungua TV Zanzibar, bara kafungua kituo Cha kuzalisha vipindi.hapa Kuna KAMPUNI mbili tofauti.moja inamiliki Tv na nyingine inamiliki uzalishaji na watangazaji .

Haya ndio masharti ya TCRA na ZCRA
Fee ya leseni analipa Zenji, Kodi ya Mapato anakupa bara, jiulize kwa Nini hv.
Jibu Ni UTAKULA ULIPOPELEKA MBOGA.
Umeandikaa stori refu Sana..Cha muhimu ambacho hujakiandika ni kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili..Tangayika na Zanzibar

Katika huu Muungano nchi ya Tanganyika imejificha kwenye mgongo wa Tanzania,yaani ni sawa na kusema kuwa serikali ya Muungano Ni serikali ya Tanganyika...

FIFA,Mikopo,Misaada ya nje yote yanafikia kwenye Serikali ya Muungano ambayo ni serikali ya Tanganyika..

Kwa maana hiyo Zanzibar lazima iombe gawio la Msaada au mikopo ya wafadhili kutoka katika serikali ya Muungano aka serikali ya Tanganyika..

Tangayika inaraidika zaidi kwenye huu Muungano zaidi ya Zanzibar, Zanzibar ni nchi ndio watu wake Ni kidogo,Msaada mdogo tu unaweza kuibadilisha Zanzibar pakubwa Sana

Zanzibar haihitaji.Mungano, Tangayika ndio inayouhitaji.huu Muungano,period
 
Nimefuatilia malumbano yako na Paskali, nimeona ipo haja ya wataalamu wa historian na waandishi wa kale watusaidie kupanua Nini kilijiri kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kizazi Cha leo na hususani jamii Forums tunaye YERRICKO NYERERE . nimesoma nakala ya kitabu chake Cha Ujasusi wa kidola na kiuchumi ukurasa 99 mpaka 159 amejibu kwa ufasaha Jambo mnalolibishania.

Nitoe Rai kwa moderator wamtafute Yerricko na kuzingatia Faida za imma wa Watanzania atoe idhini andiko lake la kwenye kitabu lisomwe na Kila mmoja bure ili kutuongea maarifa na Nini chanzo Cha Mapinduzi na hatma ya kifo Cha karume.

Nimeshindwa kuposti screen shot za kitabu kwa sababu lazima tuheshimu haki miliki ya uandishi wa Yerricko. Vinginevyo wote mko sahihi.

Nawasihi tuendelee na ndoto na kupeana mawazo mazuri Kila siku sababu sisi Ni watu wa fikra pevu.
View attachment 1464289View attachment 1464290
Unganisaha na kitabu cha Ghassani ''Kwaheri Mkoloni Kwa heri Uhuru''
Kina mambo ya research ya kuihusu Zanzibar , lakini nadhani Pascal hakipendi kitabu hiki kwa sababu za Utanganyika tuu na kuukataa ukweli.
 
Ahsante ,niendelee kutoa wito kwa mods waombe idhini za waandishi wa hivi vitabu , waridhie maandiko yao kusomwa hadharani hapa jamii forum kwa Faida ya umma kujifunza walichokiandika.
Binafsi nitakitafuta kwa sababu umeniongezea njia ya kujifunza historia ya Zanzibar
 
Umeandikaa stori refu Sana..Cha muhimu ambacho hujakiandika ni kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili..Tangayika na Zanzibar

Katika huu Muungano nchi ya Tanganyika imejificha kwenye mgongo wa Tanzania,yaani ni sawa na kusema kuwa serikali ya Muungano Ni serikali ya Tanganyika...

FIFA,Mikopo,Misaada ya nje yote yanafikia kwenye Serikali ya Muungano ambayo ni serikali ya Tanganyika..

Kwa maana hiyo Zanzibar lazima iombe gawio la Msaada au mikopo ya wafadhili kutoka katika serikali ya Muungano aka serikali ya Tanganyika..

Tangayika inaraidika zaidi kwenye huu Muungano zaidi ya Zanzibar, Zanzibar ni nchi ndio watu wake Ni kidogo,Msaada mdogo tu unaweza kuibadilisha Zanzibar pakubwa Sana

Zanzibar haihitaji.Mungano, Tangayika ndio inayouhitaji.huu Muungano,period
Huyu Hapa Muasisi anaema kweli
 
Attachments

  • NYERERE ANAJUA KUWA TANZANIA IMEUNDWA NA NCHI 2 HURU .mp4
    15.5 MB
Back
Top Bottom