Utabiri: Simba bingwa wa CAF 2023

Utabiri: Simba bingwa wa CAF 2023

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Natoa utabiri huu nikiwa na akili zangu timamu na upeo wa kutosha kuhusu mpira wa miguu.

Mwaka huu 2023 ndiyo mwaka historia mpya inaenda kuandikwa kwa Simba kuchukua kombe la CAF Champions League.

Najua kuna wapenzi wa Simba bado wanalilia kuona usajili mpya ili kuboresha timu ila ngoja nikwambie kitu. Inashangaza watu wanalilia wachezaji waondolewe ambao hata siyo tegemeo kwa timu.

Championship team katika mashindano yoyote, vilabu, taifa inahitaji wachezaji 13 hadi 15 tu wa kutegemea, yaani first 11 na sub 2 hadi 4 zinazoweza kuongeza nguvu pale inapohitajika. Simba timu hiyo wanayo.

Ambacho mimi ningefanya ni kuangalia jinsi ya kuboresha upande wa beki wa kushoto, mipira mingi inapotea kutokea kule. Ikibidi nngemsogeza Zimbwe mbele kama winger anaweza kufanya vizuri zaidi position hiyo. Kwa kuongezea tu Outtara ni mchezaji mzuri ni suala la kuangalia tunamtumiaje.

Ila wachezaji 15 wa kusumbua CAF tunao.
 
Nilitegemea Simba Ili wafike Angalau Nusu failani ya CAF.
Lazima uachane na wachezaji wafuatao.

Nelson Okwa.
Victor Akpan.
Sadio Kanute.
Mohamed Ottara.
Peter Nada.
Okra.

Wachezaji wa Nyumbani.

KIBU Denis.
Habib Kyombo.
Erasto Nyoni.
John Boko. Na
Gadiel Michael.

Hawa wachezaji Kwa sasa hawana Hadhi ya kuwa Simba.
Hawawezi kufika Nusu Fainali.
 
Nguvu moja [emoji23]
1673603879765.jpg
 
Kanute akupe kombe nitakufa siku iyo iyo
Kwenye timu inabidi uwe na mchezaji wa kutembeza buti tu kuwaweka wapinzani kwenye mstari. Ilichukua muda na mimi kumuelewa ila huyo haendi popote.
 
Nilitegemea Simba Ili wafike Angalau Nusu failani ya CAF.
Lazima uachane na wachezaji wafuatao.

Nelson Okwa.
Victor Akpan....
Usicopy na kupaste, hiyo ni spamming. Soma mada ujibu kulingana na mada husika.
 
Daah! Ngoja tuone,kwan sio hata lengo letu. Lengo ni nusu final, inatosha
Tukiishia hapo ni heri pia maana ni hatua ila unadhani tukifika fainali tutagoma kuingia kisa lengo letu lilikuwa nusu fainali?
 
Timu zinazoweza kushindania kombe lolote iwe CAF au UEFA lazima ziwe na top players nje ya hapo tuendelee kubishana Mambo yetu ya kipuuzi ya kwenda Dubai tu...., Timu inayoshindwa kufanya usajiri hata wa 300m ichukue kombe 😅😅. Utajikojolea amka usingizini...
 
Back
Top Bottom