Utabiri: Spika ajaye wa bunge la JMT atakuwa mwanaccm asiyekuwa mbunge, Dr Tulia ataendelea kuwa NS iwapo atamshinda Sugu

Utabiri: Spika ajaye wa bunge la JMT atakuwa mwanaccm asiyekuwa mbunge, Dr Tulia ataendelea kuwa NS iwapo atamshinda Sugu

Musifurahie vyeo na nafasi kwa sababu ya mishahara minono na marupurupu makubwa bali furahini kwa sababu mnatenda haki na kusimamia Katiba .

Wazungu walikua wanawaza Kuwanyonya waafrika tu bila kujua kuwa kuna zaidi ya fedha na Mali baada ya kufa. Je, fedha na mali walizojilimbikizia zinawasaidia baada ya kufa ??

Watanzania tujifunze kutenda haki.
Tukiondoa hofu ya Mungu kwenye nafsi zetu tutajiona bora kuliko wengine na hatutaona umuhimu wa kutenda haki na kuwajali wengine.

Kama Uchaguzi mwaka huu hautawapa watanzania Fursa ya kuchagua viongozi wao wanaowapenda hasa madiwani na wabunge basi hakuna haja ya kuwa na uchaguzi.; tusipoteze fedha kwa uchaguzi utakaojenga Chuki na kuimarisha dhulma kwa kuwafurahisha watu wasiomuogopa hata Mwenyezi Mungu.

Ni bora Bunge livunjwe Muda wake ukifika na tuendelee kuwatumia watendaji waaminifu wa serikali kujenga nchi na kuleta maendeleo ya wananchi.
Tujipange kwanza kabla ya kukimbilia kwenye uchaguzi wakati uchumi wa dunia umeyumba.

Wabunge sioni la maana linalotokana na maamuzi yao zaidi ya kuwa na sheria za muda mfupi kutokana na mawazo yao yasiyotizama taifa hili kwa miaka 100 ijayo wakati wa wajukuu zetu.

Mwezi wa sita bunge livunjwe na serikali iendelee kutuletea maendeleo kwa miaka miwili mbele wakati serikali ikiwa inaandaa mpango mzuri wa uchaguzi na kudhibiti janga la Korona.

Wabunge wapewe kiinua mgongo chao wakapumzike kwao.
"Stay at home."

Maendeleo hayana chama.

Bunge ambalo halina mawazo tofauti na Yale ya serikali linatupotezea Kodi zetu bure.

Nawashauri wapinzani wawe wa kwanza kuiomba serikali mwezi wa Sita muda ukifika ,Bunge livunjwe kama kawaida na kuwalipa wabunge Viinua mgongo vyao .Kisha uchaguzi usitishwe kulingana na hali ya kiuchumi na kiafya.

Hatuwezi kuwaza wanasiasa tu walioshiba wakati serikali INA majukumu makubwa ya kupigania Usalama wa nchi ,afya za wanyonge,ajira ,elimu, uchumi, na ujenzi wa miundo mbinu.
Futa uchaguzi mpaka 2022.

Wabunge kaa pembeni .Wakuu wa mikoa ,wilaya na makatibu wa Wizara na wakuu wa idara waendelee na mipango mikakati ya nchi na kusimamia maendeleo.

Bunge limekua kichala cha kupiga pesa ndio maana kila mmoja anakimbilia huko.
Eti mpaka katibu wa wizara anawaza ubunge, mkuu wa mkoa na heshima yote anayopata na madaraka makubwa aliyonayo anawaza ubunge. Ajabu kabisa .
Nimepita wilaya nyingi hakuna mbunge anayeonekana kabisa zaidi ya Mkuu wa Walaya na Mkoa.
Mh. Rais hawa wabunge wa vyama vyote hakuna wanachokusaidia zaidi ya kutafuta maslahi yao.
Wanashindwa kuorganize watu kujiletea maendeleo yao kama walivyofanya wabunge wa mwanzo enzi za mwalimu hasa wa mikoa ya Kilimanjaro.

Mh Rais ,Makamu wa Rais , Majaji ,Katibu mkuu kiongozi ,Makatibu wa Wizara ,Wakuu wa Mikoa na wilaya na wakuu wa Idara ya Ulinzi na Usalama na Takukuru wanafanya kazi nzuri. Wanatosha kusimamia maendeleo na Usalama wa nchi yetu.
Tusipoteze fedha kwa blaah blah za wabunge na madiwani wanaolenga maslahi yao.
Tujipange kwanza kimaendeleo mpaka watakapojua wajibu wao kama viongozi wa kuwaelekeza watu namna ya kujitafutia maendeleo yao kabla ya kuilaumu au kuitegemea serikali .
Tujipange na kupunguza majimbo na idadi ya wabunge . Pia tufutilie mbali Viti maalum kwa maslahi ya taifa letu sio kuwafurahisha mabeberu kwa kujitwika mzigo mzito wa matumizi makubwa ya Bunge kwa kupiga makofi tuu.
Wakafanye kazi nyingine; kama wao wanauwezo kweli wa kupanga mipango ya nchi wapange yakwao kwanza .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom