Utabiri wa Kijinga- Kinachoenda kutoka Kenya hivi karibuni

Utabiri wa Kijinga- Kinachoenda kutoka Kenya hivi karibuni

ICC tushukuru Mungu ipo.. Ungekuta saa hizi nchini Kenya, fisi wameshiba mizoga..
 
Mkuu, kwa uelewa wangu hii mihimili mitatu ya nchi inafanya kazi sawa, ndiyo maana jaji mkuu anapaswa kupigiwa salute na IGP kama alivyo spika wa Bunge, hivyo basi, Jaji mkuu hapaswi kuomba ulizi toka kwa rais, yeye anaviagiza vyombo vya ulinzi wa ndani ya nchi, isipokua jeshi bila kupitia rais wa nchi, mamlaka hayo amepewa kikatiba, mara kwa mara unamsikiaga Job Ndugai, huku kwetu akiamrisha polisi wamtafute wabunge fulani fulani na kuwapeleka kwenye kamati za bunge, hata mwananchi wa kawaida akilikosea heshima bunge, spika anao uwezo kisheria kuliagiza jeshi la polisi kumsaka na kumkamata ili apelekwe mbele ya bunge, bila kuomba kibali cha rais, lengo ni kuifanya mihimili hii iwe huru isitegemee fadhila za rais.

Kuhusu hotuba aliyotoa Maraga, kwanza katiba inamruhusu, kama inavyoruhusu mihimili ile mingine miwili, lakini anapozungimza ajikite kuzungumzia muhimili wake tu mazungumzo yajikite katika kuelimisha wananchi katika suala zima la kuheshimu katiba na utawala bora, kufuatia matamshi yaliyotolewa na rais na naibu wake, yaliyopelekea wafuasi wao kuandamana na kutoa vitisho, lisingekuwa jambo la busara kukaa kimya, kwa sababu ni vizuri akawafahamisha wananchi na dunia nzima nini kinaendelea na baadhi ya hatua alizochukua.
Maagizo kwa vyombo vya ulinzi yanatolewa na Amiri Jeshi Mkuu sio Jaji Mkuu wala Spika.

Linapokuja suala la ulinzi ni lazima mihimili hiyo iwasiliane na mhimili wa tatu unaosinamiwa na Rais. Kupigiwa salute haimaanishi kutoa amri.
 
Maagizo kwa vyombo vya ulinzi yanatolewa na Amiri Jeshi Mkuu sio Jaji Mkuu wala Spika.

Linapokuja suala la ulinzi ni lazima mihimili hiyo iwasiliane na mhimili wa tatu unaosinamiwa na Rais. Kupigiwa salute haimaanishi kutoa amri.
Sio kweli, soma kazi, majukumu na madaraka ya Spika wa bunge, unadhani Job Ndugai anaposema ninawaagiza polisi wamtafute na kumkamata mbunge fulani popote alipo wamlete Dodoma, hayo madarka kayatoa wapi?, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, waziri, kama wanayo madaraka hayo, vipi wakuu wa mihimili ambao wapo level ya rais wasiwe na madaraka?
 
watanzania wamemwaga povu kweli aisee...kama hukubaliani na mtoa mada inabidi upite kimya kimya...sio kusema kuwa wakenya wanawachukia watz...nani amesema hilo? kuna vuta nikuvute kati ya hizi nchi mbili ila haijafikia chuki...tungekuwa tulisha pigana kitambo ila twaishi kwa amani tu...peace
Haya mambo ya kuchukiana huwa nayaona mitandaoni tu! Sijawahi kupata shida nikiwa nai kwa sababu ya utanzania wangu, na sijawahi kuona mkenya akipata shida hapa tz kwa sababu ya ukenya wake. Provided kuwa wote wametimiza matakwa ya kisheria ya kuwa kwenye nchi husika!
 
Maombi ya Mdanganyika hata huwa haifiki kwenye ceiling board..... Mjiombee wenyewe... By the way Danganyika itaanguka before our eyes..... You are more unstable than you think..... We are here let's wait and see.
 
Wakipigana mzigo wa wakimbizi utakuja kwetu kwa hiyo tuwaombee wapite kwa amani
Mbona wakimbizi wenu kutoka zenji walikimbilia kenya? Au ndo mkuki kwa nguruwe.Tz ndo inapaswa kuombewa sio kenya...
 
Wasalamu ndugu zangu. Poleni na majukumu.

Nimekaa na kutafakari sana juu ya mwenendo wa Sasa za Kenya kwa hivi Sasa hasa baada ya kuonekana dhahiri kuwa mhimili wa Mahakama na ule wa Serikali wana uhasama. Yote haya ni kwa sababu ya kufutwa kwa matokeo ya Urais.

Jana tumeona Haki Mkuu David Maraga akilalamika hadharani huku akilituhumu jeshi la polisi kwa kushibdwa kutoa ulinzi kwa Majaji wa Mahakama ya juu.

Lakini pia tumeona kile kinachoitwa kuwa ni shtaka la kutaka DCJ Mwilu na Isaack Laneola wachunguzwe kwa kile kibachodaiwa kuwa ni kuwa na mawasaliano kati yao na watu wa NASA ikihusishwa na suala zima la kesi ya matokeo ya urais.

Maoni yangu juu ya hayo mambo mwili:

1. CJ David Maraga anazidi kufanya makosa. Yule ni Mwanasheria tena nguli. Ndiye reference ya mambo yote ya kisheria kwa Kenya sahivi. Hakupaswa kufanya press ya aina ile ya kulituhumu jeshi la Polisi na serikali. Haya ni makosa makubwa. Alipaswa kuongea na Rais Uhuru Kenyatta na kumueleza juu ya uhitaji wao wa ulinzi na kumuambia kuwa IGP ameshindwa kutekekeza maombi yao. Rais Kenyatta akishindwa kuwapa ushirikiano ndio angetoka before the public. But kile alichokifanya sio sawa. Amegeuka kuwa mwanasiasa badala ya kusimamia professionalism.!!

2. Tuhuma dhidi ya DCJ na Laneola kama ni za kweli huenda Mahakama ya nchini Kenya ikaingia kwenye tope zito. Na hii huenda ikafanya wananchi wakapoteza imani nayo. Lakini pia heshima ambayo ilikuwa imejijengea hivi karibuni kimataifa huenda ikafutika.

Sasa kutokana na malalamiko ya Maraga huenda watu wenye nia ovu wakatumia mwana huo kuwadhuru Majaji halafu Jubilee na serikali yake wakahusishwa. Hii ikitokea, believe me hali ya kisiasa itachafuka kwa sababu akina Raila watapata loop hole ya kulazimisha serikali ya nusu mkate.

Tuendelee kuwaombea wakenya katika kipindi hiki kigumu.

Naomba kuwasilisha.

Maraga na kundi lake hawatambui kuwa Hon Uhuru ni Rais na kamanda mkuu wa majeshi ndiyo maana hakuhudhuria kikao cha ufunguzi wa bunge wala hakumtuma muwakilisha kama heshima, sasa angaliomba ulinzi kwa mtu ambaye hamtambui! yaonekana yupo na NASA! Licha NASA walienda wachache, maanake Raila anamtambua Uhuru kuwa ni Rais!
 
Mkuu tofautisha hili ni jukwaa la siasa la Kenya sisi watanzania tuna jukwaa letu la siasa, kwa hiyo heshimu maoni yake na umjibu kwa busara
Busara IPI kenge wewe, yeye si ndio ameanza kuita forums za Tz za kijinga. Kwani hawawekagi habari za Tz humu Kenya forum. Embu tulia
 
Maombi ya Mdanganyika hata huwa haifiki kwenye ceiling board..... Mjiombee wenyewe... By the way Danganyika itaanguka before our eyes..... You are more unstable than you think..... We are here let's wait and see.
Me siwaombei mabaya, but nchi yetu itasimama na itakuwa bora sana na mfano wa kuigwa, haitakuja anguka. Can u elaborate from your point of view how we're more unstable
 
Back
Top Bottom