Nilitamani jina langu liwemo tuongezeke wenye akili Yanga ila nilipoota kuwa Power Dynamos leo atamkanda Simba 5G kwa bila Chamazi nimeona Bora nisiongezwe!
Jana Key day nilikosa bukta ningepandisha juu sijui mabinti damdam wa FA ilikuwaje!
Sasa Moloko Day inakuja sote wanayanga tutableach nywele!
Kweli kwa boli wanalopiga Yanga kuzidi Real Madrid na Barcelona sijui Al Nasr , lazima mashabiki mizuka itupande na tuonekane hamnazo, hakuna Raha kama timu yako kupiga boli la uhakika , kushinda mechi na kubeba makombe! Kufa kiume haikubaliki Yanga!
Sasa hata Yanga ikipangiwa kucheza na Asec Mimosas makundi mashabiki tutaenda na mabasi 50 huko Ivory Coast na tutashinda!
Hii Yanga Pira GAMONDI imezidi sifa Sasa hata Brazil , Argentina au Ufaransa wakija tunawapiga, Makolo hatuwataki kucheza nao tena kiwango chao duni mpira wao wa vurugu , kukamia mechi, uchawi wa kukafini maiti na rafu, hakuna fomesheni wala possession, kucheza derby na wao inashusha kiwango na thamani ya Yanga, derby yetu Sasa wanayanga tunataka iwe na Al Ahly au Wydad , Makolo papatu papatu fc tupa kule!
Leo Simba ni kweli itapasuka 5 - 0 mi kama kawa nawatakia Kila la kheri Power Dynamos, nimekaa zangu pale gizani Buza kwa Mpalanger nawasubiri mbumbumbu fc waje kushtaki baada ya kutolewa klabu bingwa Africa Leo!
Viva Power Dynamos, tunyamazishieni Makolo, nia mnayo, sababu mnayo na uwezo mnao! Leo Power Dynamos watakuwa kamili 11 uwanjani Makolo hawatafurukuta maana hupenda ushindi au droo za kimagumashi! Kama Kuna kolo wizard anabisha akafie mbelembele huko!!