Utabiri wa Likud kuhusu tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva umetimia

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,943
Reaction score
37,839
1785850860804.png

Kutoka kwa Jongwe Misuti Taita

"Wanga kule na huku nawapa dole la kati"

Huu ni mstari kutoka kwenye wimbo wake unaoitwa Moto Chini.

Leo ameonekana kutoa ujumbe kwa mashabiki wote wanaopinga au kujaribu kuipoteza BongoFlava Honors, akisema wale anaowalenga wanajijua wenyewe.

Kwa ufupi amesema, "matako yao yanajijua wenyewe" na akatoa ishara ya dole la kati kwa wale anaodai wanapambana kuipoteza BongoFlava Honors.

1785850860804.png
 
Daah inasikitisha sana na ndiyo maana SUGU kaona ameingiliwa kwenye Sector yake.

"Dili la Malaria ,Dili la Malaria nani alianza?" Noma sana.
Ila sugu apunguze ego, kama kukataa kushiriki tamasha la miaka 30, naona kama amezingua, kwasababu kwenye show anazoandaa amekua akipata support kutoka kwa wasanii wote mpaka wanaotofautiana naye kiitikadi, sasa yeye kuwakataa wenzake haijakaa sawa kabisa. Afu pia misimamo yake ya kisiasa asichanganye na Music ataharibu
 
Alikuwa sawa kabisa kukataa chukulia kampuni ya pepsi imwalike kampuni ya coca kwenye uzinduzi wa kinywaji chake uonaona iko sawa ivyo ndo ilivyotokea kwa sugu walikuwa wap kusupport hao wasanii mpaka walipo muona sugu kaanzisha
 
Unachanganya mambo mawili tofauti kabisa: ushindani wa kibiashara na sanaa.

Pepsi na Coca-Cola ni washindani wa moja kwa moja kibiashara, hivyo ni kawaida mmoja kutomualika mwenzake kwenye uzinduzi wa bidhaa yake. Lakini hapa tunazungumzia maadhimisho ya miaka 30 ya Bongo Fleva, si kampeni ya CCM wala ya CHADEMA.

Mbona na wasanii wengine wenye misimamo au uanachama wa CCM wamekuwa wakishiriki kwenye matamasha kama Bongo Fleva Honors kwa moyo mmoja bila kugeuza sanaa kuwa uwanja wa siasa? Hapo wanatenganisha kazi ya sanaa na siasa za vyama.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba Sugu mwenyewe aliwahi kumzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kupanda jukwaani kwenye show ya Profesa Jay akisema jukwaa la sanaa halifai kuingiza siasa. Kama aliamini hivyo kipindi kile, leo inakuwaje yeye mwenyewe anaingiza siasa kwenye tukio la kuadhimisha historia ya Bongo Fleva?

Kama kweli msimamo wake ni kutenganisha sanaa na siasa, basi alipaswa kuhudhuria kama msanii anayeheshimu historia ya muziki, si kuifanya sherehe ya Bongo Fleva ionekane ni ya chama fulani.
 
Hukuona 30 ya bongofleva waliingiza siasa hadi wakazomewa ndio wakaacha? Maana walikuwa wamepanga liwe la kisiasa na sugu alisema alikuwa anajua lengo lao kabla
 
Kea sababu ni Mkinga ndio apewe uwaziri? Nipe sababu ya maama na ya msingi ya kufanya Sugu apewe uwaziri
Hufahamu hawa wanaopigania na viongozi wa chadema ndiyo top appointed wenyewe,unafikiri ataokotwa mtu kutoka mbali,hapana ni wao kwanza,wakishajaa labda ndiyo wengine waingizwe,hizi ndizo hulka za binadamu toka enzi na enzi.
 
Back
Top Bottom