DAT BOY SU
Member
- Nov 15, 2017
- 29
- 30
Wana jamii nimetafakari hiki kitu nimeona sio vibaya kama tukashare mtazamo na wanazengo. Ndugu yetu mwandishi nguli humu ndani aliwahi kupost nyuzi moja kuhusu Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar Ndugu Paul Makonda kuwa anafaa ama anaweza kuja kuwa namba moja wa nchi yetu kwa siku za usoni baada ya huyu wa sasa kumaliza muda wake, alijaribu kudadavua sababu kedede sifa pamoja na mapungufu yake kwa mtazamo wake yeye na mwisho wa siku akasema anaweza amanafaa kuwa namba moja wetu.
Miezi, siku nyingi zimepita tangu atoe mawazo na mtazamo wake juu ya RC wa Dar sijui kama bado mpaka leo kama atakuwa amebadilisha au bado yupo na mtazamo wake ule ule, sababu mwenyewe yupo atakuja kutueleza.
Kama sijakosea mwaka na miezi kadhaa imepita tangu kaka yetu Mayala atoe mawazo yake. Majuzi tu hapa mkuu wa mkoa wa dar alikuwa na mazungumzo na viongozi wetu wa kiroho (Dini), hapa mkoani baada ya mazungumzo yale Askofu Mkuu Mstaafu Kardinal Pengo alinukuliwa akisema kuwa Ndugu RC Paul Makonda anafaa na ana uwezo wa kuja kumrithi Mh. Rais aliyepo madarakani baada ya muda wake kwisha na kutoa sifa kemkem kwa RC kuwa ni mtu sahihi kwa nchi yetu hapo baadae.
Mgongano huu wa mawazo wa watu hawa maarufu je umetokea kwa bahati mbaya au ndo nyota njema huonekana asubuhi kwa RC wetu anyway lets wait and see.